MAHORO;
Usiogope hata kidogo. Hautaitwa mwenge wa UHUNI kama unavyouita. Ule ni mwenge wa UHURU tuu kama ulivyoitwa na Mwasisi wake.
Huko katikati, wakimbizaji waliokuwa zaidi ni waume wenye wake zao au ndoa zao, wakapewa kazi hiyo ya kukimbiza huo mwenge. Miezi bila mke, wakajichukulia wake wa "Hit and Run" ndo wakazaliwa huko hao watoto unao wasema kwani kulikuwa hakuna kondom.
Leo, kwa sababu hakuna tena kizuizi, wanawake nao wanaukimbiza. Sasa sijui wanaruhusiwa kwenda na waume zao; lakini uchafu unaotendwa kwenye ngoma za kuulinda mwenge usizimike usiku kucha na hiyo ni lazima saana usiibiwe, kweli kama ni mke wangu, angerudi naye ningemweka tu kule Lumumba au makumbusho.
Mwenge ulikuwa na nia nzuri, ila sasa, madhara yake ni makubwa mno kama Viongozi wetu wanawapenda Watanzania, wauweke kule MAKUMBUSHO. Mbona gari ya rais ipo kule??
Tatizo, watawala hawana tena maono mapya. Kama ni kuukumbuka uhuru, tengenezeni kitu kipya.