Mwenge wa Uhuru upo kwa faida ya nani?
Jamani pamoja na kusoma primary,secondary school and then chuo lakini sijabahatika kujua umuhimu wa mwenge wa uhuru kwa Tz ya sasa.Nimejaribu kuulizia kwa baadhi ya wazee lkn wamekuwa wakinijibu kisiasa siasa tu.Kama kuna mtu aliye na weledi juu ya hii kitu anipe maelezo kwani elimu ni bahari.Ahsanteni
 
Si wewe peke yako tupo wengi, wala hakuna sehemu yoyote kwenye mtaala wa elimu yetu panazungumzia umuhimu wa mwenge, nadhani ifike wakati sasa tupigie kura swala la mwenge kwakuwa haieleweki nani wananufaika nao ukizingatia gharama zinazotumika kuuzungusha nchi nzima ni kubwa sana na output yake haionekani.
 
Kuna jamaa ye alinambia et kufungua miradi mbalimbali kwani sehemu ambazo mwenge haupiti miradi huwa haifunguliwi?
 
Unawapatia watu flani chakula mfano askari,mkuu wa wilaya na kugawa mipira ya kiume sijui kwa nini lady pepeta hawagawi?
 
Gharama za kukimbiza mwenge ni kubwa kuliko jumla ya miradi yote wanayofungua
 
... Wakuu, Najiuliza Sana Huwa Sipati Majibu.. Kuna Kitu Kimaitwa Mwenge Wa Uhuru, Sijui Mantiki Yake Ya Kuwepo Ni Nini. Hii Ni Kwasababu Kimatugharimu Pesa Nyingi Sana Huku Kila Kinapopita Eti Kuzindua Miradi Huwa Kunafanyika Ufuska Wa Hali Ya Juu Sana, Wakimbiza Mwenge Huwa Wanagawa Kondomu Kwa Watu Ili Ufuska Ufanyike Vizuri. Naskia Kuna Baadh Ya Viongozi Wametokana Na Ufuska Wa Mwenge. Sasa Siyo Sahihi Kuuita Mwenge Wa Uhuni? Kwani Umepoteza Sifa Ya Kuanzishwa Kwake? Na Kwasasa Hauna Maana Tena?. Naomba Maoni Yenu
 
Juzi Mbulu ulizindua mitaro,kilichonifurahisha sasa ni malalamiko ya kiongozi wa mbio hizo kuhusu mahudhurio ya watu,zaidi ya viongozi wa chama na serikali
 
Mungu uwahurumie wote wanaopigania kukimbiza mwenge kwa maslai yao.
 
MAHORO;
Usiogope hata kidogo. Hautaitwa mwenge wa UHUNI kama unavyouita. Ule ni mwenge wa UHURU tuu kama ulivyoitwa na Mwasisi wake.
Huko katikati, wakimbizaji waliokuwa zaidi ni waume wenye wake zao au ndoa zao, wakapewa kazi hiyo ya kukimbiza huo mwenge. Miezi bila mke, wakajichukulia wake wa "Hit and Run" ndo wakazaliwa huko hao watoto unao wasema kwani kulikuwa hakuna kondom.
Leo, kwa sababu hakuna tena kizuizi, wanawake nao wanaukimbiza. Sasa sijui wanaruhusiwa kwenda na waume zao; lakini uchafu unaotendwa kwenye ngoma za kuulinda mwenge usizimike usiku kucha na hiyo ni lazima saana usiibiwe, kweli kama ni mke wangu, angerudi naye ningemweka tu kule Lumumba au makumbusho.
Mwenge ulikuwa na nia nzuri, ila sasa, madhara yake ni makubwa mno kama Viongozi wetu wanawapenda Watanzania, wauweke kule MAKUMBUSHO. Mbona gari ya rais ipo kule??
Tatizo, watawala hawana tena maono mapya. Kama ni kuukumbuka uhuru, tengenezeni kitu kipya.
 
Huendalengo la kuanzisha mbio za Mwenge lilikuwa jema na la manufaa. La msingi ni jehayo malengo yalitokomelea wapi / yalitekwa nyara? Na nani aliyefanya uharamia huo?

 
Nchi yetu inachekesha sana! Hakuna vipaumbele hakuna nini ni bora liende tu, wizi, ufisadi na ubinafsi. Ukweli umebaki kuwa mwange nimradi wa kunufaisha wachache tu period.

Bado watawala wetu wana mawazo ya kutudanganya siye wadanganyika kuwa bado tunauhitaji utupe matumaini....wao wanajifungia ndani wakitucheka kwa uzuzu wetu...
 
... Naona Hakuna Wanaounga Mkono Mwenge Wa Uhuru, Kama Vip Uwekwe Makumbusho Iwe Kumbukumbu Tu
 
Mwenge wa uhuru umeleta changamoto kubwa,hususani kwa kuzindua miradi ya maendeleo yenye thamani ya mabilioni ya shiling
 
Back
Top Bottom