Nimevutiwa sana na hatua ya rais wa Jamhuri ya Muungaano ya Tanzania John Pombe Magufuli kufuta sherehe za uhuru wa Tanganyika na badala yake siku hiyo itumike kusafisha mazingira. Pamoja na pongezi hizo kwa Magufuli lakini kilio kikubwa cha wananchi kipo kwenye hili la mbio za mwenge wa uhuru. Kwa muda mrefu wapinzani na wananchi wa kada tofauti wamekuwa wakipinga gharama kubwa za fedha,muda na nguvu kazi inayotumika kugharamia shughuli za mbio za mwenge wa uhuru kuanzia unapowashwa mpaka unapozimwa. Kwa hiyo kama kazi iliyopo mbele yetu ni kupunguza matumizi yasiyo ya lazima serikalini basi futa kabisa haya masuala ya Mwenge wa uhuru. Nakutakia majukumu mema katika kutumbua majipu na kubwa na naomba umalize mkwamo wa kisiasa Zanzibar na kuturudishia mchakato wa katiba mpya tukianzia pale walipoishia tume ya mabadiliko ya katiba chini ya Jaji Warioba.
Pamoja katika ujenzi wa Tanzania mpya.
Naunga mkono hoja.
Mwenge hauna faida yoyote zaidi ya madhara kwa taifa.
Matumizi makubwa ya fedha za serikali bila tija.
Matumizi mabaya ya muda na rasirimali watu badala ya kutumika kwa uzalishaji.
Utoaji wa mianya ya wazi kwa wizi, rushwa na ufisadi ukizingatia hakuna auditing inafanyikaga juu ya miamala ya mwenge.
Uhamishaji na uenezi wa kazi wa maradhi ya kuambukiza kama ukimwi,na hivyo kupelekea vifo, matumizi makubwa ya fedha za kigeni kwa kuimport madawa, uzorotaji wa uzalishaji, upunguzaji wa nguvu kazi, uchumi tegemezi katika kaya za waathirika, na madhara yote ambayo huambatana na maradi kwa familia hadi taifa.
Hakuna mshikamano wa kitaifa unafanywa na mwenge kwa kuwa taifa haliwezi kushikamanishwa kwa igizo la siku moja kwa mwaka. Jambo la mshikamano wa kitaifa litafanikishwa kwa mikakati kama iliyokuwepo zamani ya kuwachanganya watu wanaotoka maeneo tofauti tofauti katika sehemu za kazi, mashuleni, kutopeleka viongozi sehemu walizozaliwa ambako kunaimarisha ukbabila na mgawanyiko wa kjamii, kuondoa ubaguzi katika huduma zote katika sekta ya uma, kutawanya mifumo ya maendeleo badala ya kuirundika sehemu moja, kuboresha huduma za jamii katika maeneo ya vijijini na kuimarisha usalama wa mipaka ya nchi yetu pamoja na ustawi wa binadamu ndani ya nchi, n.k n.k.
Mwenye haufanikishi lolote zaidi ya sanaa za kufungua miradi na kutamka kaulimbiu ambazo huisha siku mwenge ukitoka bila kufanikkisha lolote. Matangazo na vipaumbele vinaweza kusikika na kutekelezeka ziadi vikiratibiwa kitaalamu na kusimamiwa utekelezaji wake katika ngazi zote husika kitu ambacho hakiwezi kufanyika kwa makelele na makeke ya mwenge.
Kila eneo mwenge unakopita kuna serikali kuu na local government ambazo kama zingelikuwa ni kwa ajili ya mafanikio na maendeleo ya taifa, maswala yote yanayozungumziwa kwenye mwenge, yangelikuwa yanatekelezwa kwa ufanisi bora kufuatia vipaumbele na mipango sahihi ya kitaalamu.
MWENGE UFUTWE MILELE, KWA SABABU NI UHARIBIFU KWA TAIFA.