Mwenge wa Uhuru upo kwa faida ya nani?
Kama kazuia sherehe za maadhimisho ya Uhuru, kwenye mwenge ndo sina wasiwasi kabisaaaaaaaaa!!
Waliokuwa wanapiga dili kupitia mbio za mwenge wajiandae tu kisaikolojia hakuna namna
 
Hiki ndio kilio chetu kwa sasa kwa Rais wetu JPM.Afutilie mbali hizi mbio za mwenge kwani 'mapaka shume' wanakwangua pesa nyingi kupitia 'mradi' huu.Mbio za mwenge hazina mantiki kwa sasa na wala hakuna impacts inayoeleweka.
 
Wacha auache uendelee akizuia mabo..y..a yatasema hazina haina pesa..
 
Eti huyu Mzee Mwanakijiji mbona namfananisha na yule aliyeanikwa na Gwajima???
 
Enzi hizo Mwanakijiji alikua hajatembelewa na hela za escrow... Sasa hivi humwambii kitu
 
Kusema kweli mwenge umepitwa na wakati na haumsaidii chochote mwananchi wa kawaida.Na kama sisi wananchi hatuutaki, una save interest ya nani?Obviously ni status quo.

Upo ushahidi wa kutosha kwamba zoezi zima la kukimbiza mwenge lina misingi ya ushirikina.Baada ya kutafuta maana halisi ya symbol ya mwenge,there is ample evidence kwamba zoezi la kukimbiza mwenge lina agenda ya kupumbaza watu.No wonder watanzania ni watu wasiojielewa kabisa.
Leo kwa mara nyingine mbio za mwenge zimeanza tena Tanzania, na safari hii mwenge umewashwa huko Dole Zanzibar kuendeleza ile adhma ya taifa letu changa kuwa "sisi tumekwisha kuwasha mwenge na kuuweka Kilimanjaro". Mwenge huu ulipowashwa mara ya kwanza na kuwekwa kwenye kilele cha Kilimanjaro na Nyirenda, ulikuwa uwe ishara ya matumaini, upendo, na umoja wa Taifa letu.

Matukio ya hivi karibuni hasa baada ya muasisi wa mwenge huo kufa, kuna kila dalili kuwa tunachokimbiza sasa hivi ni kivuli tu cha mwenge ule kwani miale ile ya mwanzo ya mwenge wetu wa uhuru imeanza kuzimika na inaonekana ikififia kila mwaka mpya ujapo. Mwenge huu sasa umekuwa ni alama ya watu wachache kujiangazia wao na familia zao huku sisi wengine tukiendelea kubakia gizani. Hakuna kitu kinachoonesha kufifia kwa mwenge huo kama suala la mikataba ya nishati, madini, ununuzi wa rada, ndege ya rais, n.k Zaidi ya yote kwa wanafunzi waliokwama Ukraine, mwenge huu kwao tayari umezimika ( a little strech there, but why not try..??)

Je kuna matumaini ya kurejesha nuru yake tena? Je kuna haja ya kuuwasha tena ili uendelee "kuwamulika" wabadhirifu, wazembe maofisini, wala rushwa magendo n.k ? Au tuamue kuuzima tu, ili kila mtu ajiwashie mshumaa wake yeye mwenye na wale wenye uwezo wawashe vibatari, chemli, na taa za umeme! ?

huu mwenge kweli tunasababu ya kuendelea kuukimbiza?
 
Jaman atawezaje kuutoa mwenge kwenye route ya nchi nzima kama jina lake kwenye M Kuna mwenge katikati ndo mwanga wake ule wacha uendelee kumulika kazi zake
 
Jamani mwenge sio jambo la kuingiza kipato. Ni kweli kuna gharama ambazo naamini mara nyingi zinaonekana kubwa kwani ujanjaujanja umekuwepo sana miongoni mwetu. Sipingi kudhibiti gharama lakini kama symbol ya utaifa wetu, umoja wetu na uzalendo wetu sioni umuhimu wa kuziondoa mbio hizi. Mwenge hufika hata viongozi wetu wasipotazamia kufika, kwangu ni muhimu mno.
Kuna mengi hayana faida kwa nchi hasa za kiuchumi. Bendera ya taifa, picha za viongozi kwenye maofisi ya umma nk. Tunapowapigia viongozi wanapotutembelea mizinga 21 haina maana kiuchumi ila kiprotokali ni jambo la muhimu mnoo.
Naamini kabisa unapozungumzia Xmas, Idd, nk huwezi kuona umunimu wake kiuchumi ila watu kwa nn wanasherehekea? Kuwaweka watu pamoja. Kuleta bond kwenye familia, kuwaunganisha watu wawe kitu kimoja.
Sidhani kama kila kisichokuwa na uingiizaji wa kipato kinapaswa kifutwe, tutafakari kwa pamoja.
 
mwenyekiti bado ni muhimu kwa nchii ili ukiendelea kujenga udugu na umoja watu, ila taratibu za uratibu wake zitizamwe upya
 
Namwomba Rais Magufuli futilia mbali mwenge wa Uhuru ambazo ni garama zisizo na msingi. Wakuu wa mikoa na mawaziri wafanye kazi ya kufungua miradi ambayo mwenge unafungua kwa garama nafuu.
 
ila mwenge ni moja ya national symbols huwezi kuufuta kirahisi kama watu wanavyodhani ina hadhi sawa na katiba offcource zote ni national system swala la kuufuta ni gumu sana labla atafute namna nyingine ya kuukimbia huo mwenge with low cost

km sherehe za uhuru zinapotezewa hiyo tochi itazimwa tu hakuna nmna nyingine wizi mtupu upuuz uharibifu wa kodi na uenezaj wa ukimwi
 
mwenge wa uhuru karibu mwamashimba, uwachome walanguzi wote, uwachome mafisadi wote, uwamulikie wazalendo wote

instead unawamulikia wezi na wafujaji wa kodi.....

Weka pale makumbusho......

angalia faida zake na hasara zake kwa karne hii...km hasara ni kubwa kuliko faida
wa kaz gani tupa huko....
 
Zanzibar hatujatumia ushirikina kuabudu mungu moto Abeid Aman Karume hakukubali upuuzi huo anajuwa ni ushirikina kuabudu Mungu Moto
 
Leo kwa mara nyingine mbio za mwenge zimeanza tena Tanzania, na safari hii mwenge umewashwa huko Dole Zanzibar kuendeleza ile adhma ya taifa letu changa kuwa "sisi tumekwisha kuwasha mwenge na kuuweka Kilimanjaro". Mwenge huu ulipowashwa mara ya kwanza na kuwekwa kwenye kilele cha Kilimanjaro na Nyirenda, ulikuwa uwe ishara ya matumaini, upendo, na umoja wa Taifa letu.

mbio hizi kusema kweli zingesimamishwa baada ya miaka 18 tu ya uhuru. sasa Tanzania limtu lina miaka 54 bado linasherehekea kuwa huru kutoka kwa wazazi. huu utakuwa mradi wa mtu.
 
Nimevutiwa sana na hatua ya rais wa Jamhuri ya Muungaano ya Tanzania John Pombe Magufuli kufuta sherehe za uhuru wa Tanganyika na badala yake siku hiyo itumike kusafisha mazingira. Pamoja na pongezi hizo kwa Magufuli lakini kilio kikubwa cha wananchi kipo kwenye hili la mbio za mwenge wa uhuru. Kwa muda mrefu wapinzani na wananchi wa kada tofauti wamekuwa wakipinga gharama kubwa za fedha,muda na nguvu kazi inayotumika kugharamia shughuli za mbio za mwenge wa uhuru kuanzia unapowashwa mpaka unapozimwa. Kwa hiyo kama kazi iliyopo mbele yetu ni kupunguza matumizi yasiyo ya lazima serikalini basi futa kabisa haya masuala ya Mwenge wa uhuru. Nakutakia majukumu mema katika kutumbua majipu na kubwa na naomba umalize mkwamo wa kisiasa Zanzibar na kuturudishia mchakato wa katiba mpya tukianzia pale walipoishia tume ya mabadiliko ya katiba chini ya Jaji Warioba.
Pamoja katika ujenzi wa Tanzania mpya.
 
Waveja sana, Hapa Kazi Tu!!!
 
Naunga mkono hoja.

Mwenge hauna faida yoyote zaidi ya madhara kwa taifa.

Matumizi makubwa ya fedha za serikali bila tija.

Matumizi mabaya ya muda na rasirimali watu badala ya kutumika kwa uzalishaji.

Utoaji wa mianya ya wazi kwa wizi, rushwa na ufisadi ukizingatia hakuna auditing inafanyikaga juu ya miamala ya mwenge.

Uhamishaji na uenezi wa kazi wa maradhi ya kuambukiza kama ukimwi,na hivyo kupelekea vifo, matumizi makubwa ya fedha za kigeni kwa kuimport madawa, uzorotaji wa uzalishaji, upunguzaji wa nguvu kazi, uchumi tegemezi katika kaya za waathirika, na madhara yote ambayo huambatana na maradi kwa familia hadi taifa.

Hakuna mshikamano wa kitaifa unafanywa na mwenge kwa kuwa taifa haliwezi kushikamanishwa kwa igizo la siku moja kwa mwaka. Jambo la mshikamano wa kitaifa litafanikishwa kwa mikakati kama iliyokuwepo zamani ya kuwachanganya watu wanaotoka maeneo tofauti tofauti katika sehemu za kazi, mashuleni, kutopeleka viongozi sehemu walizozaliwa ambako kunaimarisha ukbabila na mgawanyiko wa kjamii, kuondoa ubaguzi katika huduma zote katika sekta ya uma, kutawanya mifumo ya maendeleo badala ya kuirundika sehemu moja, kuboresha huduma za jamii katika maeneo ya vijijini na kuimarisha usalama wa mipaka ya nchi yetu pamoja na ustawi wa binadamu ndani ya nchi, n.k n.k.

Mwenye haufanikishi lolote zaidi ya sanaa za kufungua miradi na kutamka kaulimbiu ambazo huisha siku mwenge ukitoka bila kufanikkisha lolote. Matangazo na vipaumbele vinaweza kusikika na kutekelezeka ziadi vikiratibiwa kitaalamu na kusimamiwa utekelezaji wake katika ngazi zote husika kitu ambacho hakiwezi kufanyika kwa makelele na makeke ya mwenge.

Kila eneo mwenge unakopita kuna serikali kuu na local government ambazo kama zingelikuwa ni kwa ajili ya mafanikio na maendeleo ya taifa, maswala yote yanayozungumziwa kwenye mwenge, yangelikuwa yanatekelezwa kwa ufanisi bora kufuatia vipaumbele na mipango sahihi ya kitaalamu.

MWENGE UFUTWE MILELE, KWA SABABU NI UHARIBIFU KWA TAIFA.
 
Back
Top Bottom