Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Leo kwa mara nyingine mbio za mwenge zimeanza tena Tanzania, na safari hii mwenge umewashwa huko Dole Zanzibar kuendeleza ile adhma ya taifa letu changa kuwa "sisi tumekwisha kuwasha mwenge na kuuweka Kilimanjaro". Mwenge huu ulipowashwa mara ya kwanza na kuwekwa kwenye kilele cha Kilimanjaro na Nyirenda, ulikuwa uwe ishara ya matumaini, upendo, na umoja wa Taifa letu.
Matukio ya hivi karibuni hasa baada ya muasisi wa mwenge huo kufa, kuna kila dalili kuwa tunachokimbiza sasa hivi ni kivuli tu cha mwenge ule kwani miale ile ya mwanzo ya mwenge wetu wa uhuru imeanza kuzimika na inaonekana ikififia kila mwaka mpya ujapo. Mwenge huu sasa umekuwa ni alama ya watu wachache kujiangazia wao na familia zao huku sisi wengine tukiendelea kubakia gizani. Hakuna kitu kinachoonesha kufifia kwa mwenge huo kama suala la mikataba ya nishati, madini, ununuzi wa rada, ndege ya rais, n.k Zaidi ya yote kwa wanafunzi waliokwama Ukraine, mwenge huu kwao tayari umezimika ( a little strech there, but why not try..??)
Je kuna matumaini ya kurejesha nuru yake tena? Je kuna haja ya kuuwasha tena ili uendelee "kuwamulika" wabadhirifu, wazembe maofisini, wala rushwa magendo n.k ? Au tuamue kuuzima tu, ili kila mtu ajiwashie mshumaa wake yeye mwenye na wale wenye uwezo wawashe vibatari, chemli, na taa za umeme! ?
huu mwenge kweli tunasababu ya kuendelea kuukimbiza?
ila mwenge ni moja ya national symbols huwezi kuufuta kirahisi kama watu wanavyodhani ina hadhi sawa na katiba offcource zote ni national system swala la kuufuta ni gumu sana labla atafute namna nyingine ya kuukimbia huo mwenge with low cost
mwenge wa uhuru karibu mwamashimba, uwachome walanguzi wote, uwachome mafisadi wote, uwamulikie wazalendo wote
Leo kwa mara nyingine mbio za mwenge zimeanza tena Tanzania, na safari hii mwenge umewashwa huko Dole Zanzibar kuendeleza ile adhma ya taifa letu changa kuwa "sisi tumekwisha kuwasha mwenge na kuuweka Kilimanjaro". Mwenge huu ulipowashwa mara ya kwanza na kuwekwa kwenye kilele cha Kilimanjaro na Nyirenda, ulikuwa uwe ishara ya matumaini, upendo, na umoja wa Taifa letu.
Nimevutiwa sana na hatua ya rais wa Jamhuri ya Muungaano ya Tanzania John Pombe Magufuli kufuta sherehe za uhuru wa Tanganyika na badala yake siku hiyo itumike kusafisha mazingira. Pamoja na pongezi hizo kwa Magufuli lakini kilio kikubwa cha wananchi kipo kwenye hili la mbio za mwenge wa uhuru. Kwa muda mrefu wapinzani na wananchi wa kada tofauti wamekuwa wakipinga gharama kubwa za fedha,muda na nguvu kazi inayotumika kugharamia shughuli za mbio za mwenge wa uhuru kuanzia unapowashwa mpaka unapozimwa. Kwa hiyo kama kazi iliyopo mbele yetu ni kupunguza matumizi yasiyo ya lazima serikalini basi futa kabisa haya masuala ya Mwenge wa uhuru. Nakutakia majukumu mema katika kutumbua majipu na kubwa na naomba umalize mkwamo wa kisiasa Zanzibar na kuturudishia mchakato wa katiba mpya tukianzia pale walipoishia tume ya mabadiliko ya katiba chini ya Jaji Warioba.
Pamoja katika ujenzi wa Tanzania mpya.