Hiyo budget ya mwenge sio kweli haiwezifika 400bn

Ukiondoa mtazamo wa kupinga kila kitu hebu Fanya zoezi kufuatilia miradi itakayofunguliwa mwenge ukipita mkoan kwako
 
Nashangaa sijawahi kusikia serikali imekosa pesa ya kukimbizia Mwenge. Ila linapoibuka swala kama la kutoa ajira utasikia serikali haina pesa...
Hizi pesa za kukimbizia Mwenge huwa zinatoka kwenye vyanzo vipi ambavyo huwa havikauki? Na kwa nini bunge lisipitishe sheria ya kufuta mbio za Mwenge? Maana kwa karne hii umeshakuwa irrelevant.. Kama ni uhuru tulisha upata zaidi ya miaka hamsini iliyopita and by the way sasa kila nchi iko huru so hakuna haja ya kuendelea na sherehe zisizo na tija...
 
Waulize wafanyakazi wa serikali kinachowakuta kwenye halmashauri zao.
Huwa wanachangishwa kias Fulani, pia kila taasisi hujitegemea kushiriki mbio hizo. Mengine sijui
 
Hela za mwenge kuna wakati walikuwa wanakata mishahara ya baadhi ya watumishi wa umma sijui kama bado wanaendelea kuwakata au ni vipi
 
Walimu ndiyo huwa wanakatwa kwa lazima na kulazimishwa kushona sare
 
Zamani mbio za mwenge wa Uhuru zilikuwa zikikimbizwa maeneo ya mjini na vijijini kuelekea kuzindua miradi mbalimbali kwa miguu kila wanapoingia maeneo hayo,leo lengo lao lipo vile vile ila tofauti ni kuwa mbio hizi siku hizi ni mwendo wa gari mwanzo mwisho. Hata ile fursa wananchi walikuwa wakiipata ya kuukimbiza na kuushika mwenge wao imepotea,labda tatizo nini linalosababisha mabadiliko hayo!?
 
mwenge una uhusiano na nguvu za giza, kwenye ule moshi huwa kuna madawa ya kuwapumbaza wa tanzania sasa wakitumia meli au ndege moshi utapotea bure!
 
mwenge wa uhuru unafaa kuwekwa makumbusho ni upumbafu karne hii bajet ya mwenge ni mabilion kisha unaenda kufungua tundu za choo cha tope huko vijijini ambapo kinakuwa na gharama ya kununua kuku mmoja sokoni !!! what kind of nonesense is this?

instead zile bajeti wangezielekeza kila mkoa, kila mwaka,
mfano mwaka huu itajenga shule kibiti......
mwaka ujao itajenga muundo mbinu somanga....
unaofwatia inamalzia jengo la tra kule chattle.....
kuliko huu unyumbu unaofanywa sasa ,ni ufujaji wa pesa za watanzania,maana hauna faida zaidi ya hasara,ni ukosefu wa akili na maarifa kuendelea tumia mabilion kuhangaika na hiyo tochi...


MY TAKE MATUMIZI YA BAJETI YA MWENGE YABADILISHWE, NA YAELKEKEZWE KWENYE MAMBO MBALIMBALI HASA VIJIJINI IJENGE SHULE MAHOSPITALI MIUNDOMBINU MADAWATI NK.............







hawa watu woote hapa wanalipwa

halafu siku hizi nasikia waalimu wanakatwa pesa kwa lazima kuchangia mwenge woyiii
 
Wananchi walishirikishwa kuushika lakini hivi sasa wanashirikishwa kuchangia,kuushika ni kwa wateule wachache,kuna haja ya mbio hizi kuendelezwa?
 
mwenge una uhusiano na nguvu za giza, kwenye ule moshi huwa kuna madawa ya kuwapumbaza wa tanzania sasa wakitumia meli au ndege moshi utapotea bure!
Mwenge una mapepo makali sanaa
 
Kama swali mlivyoona hapo juu mimi nmeshidwa kujibu naomba mwenye kuweza kujibu ili na mimi nipate faida ya kufahamu mwenge unafaida gani.

Asante
 
Salam,

Nikikwambia nimekuchukia na kukukasirikia Kama ninavyouchukia mwenge.... Jihadhari sana.. Naweza kukudhuru.

Nisiwe mnafiki Lile dude ninalichukia.
 
Wote tunajuwa kwamba binge ndicho chombo cha kuweza kufanya maamzi makubwa hapa nchini, lakini kwa bahati mbaya bunge letu limeshindwa kufanya hivo.

wabunge walipaswa kwa Pauli Moja kupitisha hseria itakayozifuta mbio za mwenge hapa nchini kwani hazina Tija kwa taifa Bali zinaligharimu taifa letu.

kwa kuwa wameshindwa na wameishia kuwa mbumbu natamani magufuli angepitisha amri ya Kuwalazimisha wabunge wawe wanakatwa fedha kutoka kwenye posho za vikao na miashahara yao ya kila mwezi.

nawasilisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…