Mwenge wa Uhuru upo kwa faida ya nani?
Mwenge upo mkoa wa mwanza na Leo unaingia wilaya ya Ilemela
Hakuna huduma ya daladala kuanzia eneo la National kuelekea buswelu na maeneo ya jirani
Taabu yote hii ni kwa sababu ya mwenge
Wanafunzi na watu wengine wakiwemo wanaCCM wamejazana barabarani kusubiri mwenge
Wanafunzi hawasomi Leo kisa mwenge huu ni upuuzi kuvunja ratiba za maana kisa kusubiri moto tu
Nimepita karibu na shule flani wamejaa kina mama,migambo,police na wanafunzi ambao ndo mtaji wa CCM wanasubiri mwenge
Mwanajeshi anawaamrisha mgambo kwa matusi wakae vizuri wote katika gari nkaamini kweli kazi ya jeshi ni utumwa
Tangu nazaliwa hadi sasa sijui faida ya huu mwenge kwenye nchi hii anejua aniambie
Au ndo unatumika kupumbaza watu??
 
Poleni sana, siku mwenge ukipelekwa museum na ccm nao wataufuata huko

Psalm 133:1[emoji768] "Behold, how good and how pleasant it is for brethren to dwell together in unity."
 
Kwa muda mrefu wapinzani wamekuwa wakishauri mbio za mwenge zizitishwe kwani kwa sasa hazina ulazima sana na pia itasaidia kuokoa fedha zinazotengwa kwa ajili ya kugharamia shughuli za kukimbiza mwenge nchi nzima.

Wapinzani na wadau wengine badala yake walishauri mwenge huo uwekwe katika Jumba la Makumbusho kwa ajili ya kumbukumbu ya vizazi vijavyo.

Hata hivyo,ushauri huu siku zote umekuwa ukigonga mwamba na mbio hizi zimeendelea mpaka sasa.

Lakini pamoja na yote haya naomba niwe wa kwanza kutoa angalizo kuwa mbio hizi zinaweza kufutwa /kusitishwa wakati wowote ule iwapo madai ya kuporomoka kwa uchumi ni yana ukweli japo watawala wamekuwa wakipinga hoja hizi.


Hata leo mheshimiwa anaweza kabisa(natabiri) kuzifuta mbio hizi na kutangaza leo ndio siku ya mwisho ya kuadhimisha kilele cha mbio za mwenge.Kama sio leo basi inaweza kuwa siku nyingine.

Siku wakifikia uamuzi huo watakuja na sababu zao lakini kamwe hawawezi kutaja sababu zilizowahi kutolewa na wapinzani au kama kweli hali ya uchumi ndio itakuwa chanzo.

Tunaweza kuambiwa tu sasa ni wakati wa kufanya kazi au ikatolewa /zikatolewa sababu nyingine zozote zile.

Time will tell.
 
Kinachokera ni mambo yao wayaanzishe na Mwenge unabajeti yake lakini wafanyakazi ambao hatuna maana kwa serikali hii ndio tunaobanwa eti tutoe pesa za Mwenge kama wamekata increment, kupandisha madaraja na mambo mengine basi msisumbue wafanyakazi na wafanyabiashara
 
- "Mimi nawashangaa sana watu wanaotaka Mwenge ufutwe, sijui wanatoka sayari gani?

- Mimi siwezi kukubali Mwenge ufutwe, najua na Dkt. Shein hawezi kukubali mwenge ufutwe katika kipindi chake. Naomba muwazomee na muwasute hao wanaosema Mwenge ufutwe.

- Kufuta Mwenge wa Uhuru ni sawa na kufuta historia na alama za nchi yetu.

- Katika kipindi cha uongozi wangu na uongozi wa Dkt. Shein Mwenge utaendelea kuwepo na utaendelea kukimbizwa nchini Kote." Kauli ya Rais Magufuli.

Note:

Yeah hayo ni mawazo yake hakuna anaepinga mawazo ya mtu mwingine.Hata hao wanaosema mwenge haufai ni mawazo yao sioni sababu ya kutokwa na povu.Kila mtanzania anayomawazo pia tujiulize toka mwenge umeanza kukimbizwa umeliingizia taifa bei gani? Kama hakuna je'faida ya mwenge ipo wapi? Nadhani wazo la kuanzisha mwenge lilifanikiwa hapo nyuma lakini kwa dunia ya leo gharama za maisha zimezidi kuongezeka zaidi na uwendeshaji wa mwenge umekua na gharama kubwa sana.Niishauri Serikali kama mtanzania mwenge uwepo kama kawa ila uwashwe kwa siku moja kila mwezi papohapo ulipo kuliko kukimbizwa nchi nzima, pesa yake ya bajeti ya mwenge walipiwe matibabu maskini wenzetu waliopo mahospitalini kwani mwenge umekua chumaulete kwa taifa badala ya faida leo mashuleni vyoo, maabara pamoja na ofisi za walimu ni shida lakini bajeti ya mwenge ipo.
 
Ndio njia rahisi sana ya kusambaza maradhi nchi nzima kwa kasi ya radi.

Kumbukumbu zangu zinaonyesha kwamba hakuna mradi wowote uliozinduliwa na mbio za mwenge uliodumu hata kwa miezi 6 tu .
 
Unasaidia kujua kiwango cha kipya cha maambukizi ya UKIMWI

Mwisho wa Kunukulu.
 
Nilijuacho, anayekupinga wewe mpinge kwa hoja... KUZOMEA NI ALAMA YA KUISHIWA HOJA...
 
Wandugu yule mchungaji mwenye makeke ahoji mwenge una faida gani kama watu kuona basi wautembeze kutoka posta mpaka ubungo halafu wa mikoani wauangalie kwenye TV, huyu jamaa nashindwa kumwelewa kabisa wandugu ?


images
 
YouTube please ,ktk mahubiri yake
Gwajima Amjibu Magufuli Kuhusu Mwenge wa Uhuru
 
Kwa akili tu za kawaida mwenge una faida gani kwa wananchi wenyewe?! Zaidi ya kukaririshwa maneno ya hovyo!!
 
Back
Top Bottom