Mwenge wa Uhuru upo kwa faida ya nani?
bhangi haijwahi kumuacha mtu salama...ila nimependa concept yake hahahahhahahahah
 
Naunga mkono mbio za mwenge kwakuwa miradi mbalimbali ya maendeleo inazinduliwa na kuhamasisha shughuli mbalimbali za kijamii.
Kinachonikera na kunisikitisha ni Tabia za kwenye mkesha wa mwenge, Ulevi , umalaya, ubakaji, wizi na tabia zote mbaya zinazoendana na hizo. Sasa nauliza hatuwezi kukimbiza huu mwenge bila kuweka mkesha. Hapa namaana ikifika usiku unazimwa halafu asubuhi unawashwa kazi inaendelea au hauzimwi lakini unawekwa sehemu mpaka asubuhi.

Naomba Viongozi walifikirie hili ili kuepusha mikasa hii inayojitokeza siku ya mkesha wa mwenge.
 
Kwani ulishalazimishwa kukesha?
 
IJUE HISTORIA YA KUANZISHWA KWA MWENGE:
Mnamo miaka ya zamani hizo kabla na baada kidogo ya ukoloni watu waliamini sana katika Mazindiko, Uchawi na Kafara tofauti kidogo na miaka ya hivi leo(miaka ya utandawazi) ambapo watu huyapooza mambo hayo kwa kukemea mila potofu na pengine ni ukiukwawaji wa haki za binadamu. Naam basi tuitizame miaka ya 1900 ambapo walizaliwa watu mashuhuri na baadaye waliitwa "wataalamu" walioweza kusaidiana na viongozi wa nchi yetu kwenye mambo mbalimbali ya kitaifa na waliaminika sana kwenye tawala za ki-chief na jamii kwa ujumla.
Miongoni mwao alikuwepo mtaalamu aliye julikana kwa jina la Forojo Ganze, huyu alizaliwa mwaka 1902 na alikuwa na jopo la wafuasi wake/wazee wenzake wa nyakati hizo ambao walikwenda sambamba na Mwl.Nyerere katika kutoa mchango wao wa kitaalamu kwenye maswala nyeti ya kitaifa.
Forojo Ganze, alikuwa ni mchawi maarufu na ni mmoja kati ya wazee waliotumwa kufanya zindiko la nchi baada ya uhuru kule bagamoyo, walipewa kazi ya kuhakikisha rais aliye madarakani (Mwl.Nyerere) hapingwi na mtu yeyote. Zindiko hilo lilifanyika bagamoyo katika moja ya mashimo yanayopatikana wilayani hapo, na zoezi hilo lilienda sambamba na kumuuliza shetani na malaika zake "ni jambo gani lifanyike ili Tanzania iendelee?".
Basi kiongozi wa msafara Forojo Ganze ndiye mtu pekee aliyeingia kwenye hilo shimo mithili ya pango kwaajili ya kuuliza , alikaa huko kwa muda wa siku 10 huku akiwa amewaacha wazee wenzake nje wakimgoja atakuja na jibu gani ili wakampatie rais na wazee wengine wa Dar es salaam, kilichoshangaza siku ya kumi na moja alitoka akiwa hoi hajiwezi alikuwa kama mtu aliyepigwa na alikuwa anaongea lugha isiyofahamika, wenzake wakiwa wanaongozwa na Yahaya Hussien walimbeba hadi ikulu Dar es salaam na walipomfikisha mbele ya mwalimu Nyerere alitamka maneno haya "Baba, sisi tunataka kuwasha mwenge na kuuweka juu ya mlima kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini mahala pasipo na tumaini, faraja palipo na huzuni, upendo penye chuki na heshima palipo na dharau ".
Alitamka maneno hayo yanayohusu mwenge kwa kiswahili kisha akanyoosha juu mkono wake wa kulia ambao tayari ulikuwa umeandikwa namba hii 115, kisha akakata roho.
Baada ya mazishi mwalimu aliyafanyia kazi maneno ya Forojo Ganze akaanzisha mwenge wa uhuru bila kujua ulikuwa na maana gani, baada ya hapo alimuagiza Yahya Hussein atafasiri maana ya ile namba 115, kama kawaida ya Shekhe Yahaya alitafasiri akamwambia kuwa namba hiyo inamaanisha "Utakufa ukiwa na umri wa miaka 77 na taifa la Tanzania kwa kipindi hicho litakuwa na umri wa miaka 38 ".
Hii inamanisha ukichukua 77 umri wa mwalimu jumlisha 38 umri wa taifa utapata 115, na hii ndivyo ilivyokuwa, mwaka 1999 mwalimu alikufa akiwa na miaka 77 na taifa lilikuwa na miaka 38 ya uhuru (77+38=115) pia utamaduni wa rais kuongea na wazee wa Dar es salaam unaendelea hadi sasa na wamekuwa na maamuzi ya kitaifa na husikilizwa sana wanachokisema.
Jiulize, mbona haijawahi kutokea rais akaongea na wazee wa Bukoba ama wa Arusha jambo la kitaifa?
Jibu, Zindiko la bagamoyo linafanya kazi.
Safu iliyoagizwa kufanya zindiko ilikuwa ya watu watano(5) ambao ni.
1: Forojo Ganze mwenyewe,
2: Mzee Ramadhan, aliye zaliwa mwaka 1920,
3: Ally Tarazo, aliye zaliwa mwaka 1929,
4: Komwe wa Komwe, aliye zaliwa mwaka 1918 na
5: Shekhe Yahya Hussein, aliye zaliwa mwaka 1925.
 
Isaya 50:11
Mwenge ni uduwanzi tu
Lakini nyinyi mnaowasha moto, na kujifanyia silaha za mienge, tembeeni kwa mwanga wa moto huo, miali ya moto mliowasha nyinyi wenyewe. Mtakachopata kutoka kwa Mwenyezi-Mungu ni hiki: Nyinyi mtalala chini na mateso makali.
 
Naunga mkono mbio za mwenge kwakuwa miradi mbalimbali ya maendeleo inazinduliwa na kuhamasisha shughuli mbalimbali za kijamii.
Kinachonikera na kunisikitisha ni Tabia za kwenye mkesha wa mwenge, Ulevi , umalaya, ubakaji, wizi na tabia zote mbaya zinazoendana na hizo. Sasa nauliza hatuwezi kukimbiza huu mwenge bila kuweka mkesha. Hapa namaana ikifika usiku unazimwa halafu asubuhi unawashwa kazi inaendelea au hauzimwi lakini unawekwa sehemu mpaka asubuhi.

Naomba Viongozi walifikirie hili ili kuepusha mikasa hii inayojitokeza siku ya mkesha wa mwenge.
Mkuu kama ulivyoeleza, mimi iliwahi kunitokea miaka fulani nikiwa kwenye kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya fulani.

Mnalazimishwa kukesha huku miziki ikipigwa, pombe kunywewa na zinaa kutembea mtindo mmoja mpaka asubuhi!

Mtu usiyetumia kilevi ni karaha kubwa kukesha ukipigiwa kelele na walevi bila kuwa na hisia ya furaha.

Mwenge wenyewe unawekwa kwenye stand maalumu na kuzungukwa na walinzi walioshikamana mpaka kunakucha.

Hutoa moshi mzito wa diesel, hatari kwa afya za watu hasa wanaokesha wameuzunguka, lakini hawajali wala kutafakari hayo.
Kwa kweli hakuna umuhimu wowote wa mkesha wa mwenge
 
Afadhali unisaidie kueleza maana kuna watu hawaelewi.
 
Back
Top Bottom