Mwenge wa Uhuru upo kwa faida ya nani?
#FaizaFoxy

Nahisi kuna vitu umevichanganya ambavyo unapaswa ufanye utafiti zaidi. Usichanganye mishumaa ya makanisani na mwenge wa uhuru.

Ila suala kwamba mwenge wa uhuru ni ibada za kishetan naweza kukubaliana nalo kwa upande mwingine kwani huu mwenge huwa unakimbizwa pale tu mungu wa ukoo wa Nyerere ambaye ni nyani mkubwa aitwae "MUHUNDA" anapotokeza katika milima ya wazanaki pale butiama alipozaliwa Mwl. Kwa hiyo mwenge hukimbizwa kama ibada ya kumtukuza huyu Nyani kwani wanaamini alichangia kiasi kikubwa uhuru kupatikana bila vita dhidi ya mkoloni

Kuna wakati hutokeza mara mbili kwa mwaka ndo maana Mwenge siku hizi unaweza kukimbizwa mara mbili kwa mwaka tofauti na zaman ambapo alikuwa anatokeza mara moja.

Kwa sababu hiyo nami naunguna kusema ni ibada ya kishetani ila isuhusishwe na kanisa lolote.
 
Mwenge ni ibada za kishetani hauna mafungamano na ukristo wala uislam ndio maana nasikia mwenge unapolala kuna kuwa na ngono sana.

Unatakiwa kutuletea ushahidi kutoka biblia takatifu na si ushahidi wa kuokoteza. Mwenge ni ibada ya CCM kwa ajili ya kuwapumbaza wananchi wasiwe na ufahamu wanaibiwa rasilimali zao kama dhdhabu, almasi, gasi ........
FaizaFoxy

Hayo niliyoyaandika sikuyafikiria tu kichwani mwangu, na nimekueleza kwenye bandiko langu soma kuhusu "sanctuary lamp". Ni ibada inayofanyika ndani ya makanisa mengi tu, na la Kikatoliki ni moja wapo.

Sasa kama ni ibada ya Kishetani, inabidi wewe ufikirie mara mbili, jee kwanini ifanyike kwenye kanisa? Na pia inabidi uje na maelezo na hoja ya kuijibu post namba moja ya mleta mada. Umeisoma vizuri?

Utueleze, sisi kama wa Tanzania, huu mwenge una maana gani? wa nini, unaashiria nini? kama si ibada ya Kishetani?

Soma hii kutoka kwenye " Catholic Encyclopedia":

In the Old Testament God commanded that a lamp filled with the purest oil of olives should always burn in the Tabernacle of the Testimony without the veil (Exodus 27:20, 21). The Church prescribes that at least one lamp should continually burn before the tabernacle (Rit. Rom. iv, 6), not only as an ornament of the altar, but for the purpose of worship. It is also a mark of honour. It is to remind the faithful of the presence of Christ, and is a profession of their love and affection. Mystically it signifies Christ, for by this material light He is represented who is the "true light which enlighteneth every man" (John 1:9). If the resources of the church permit, it is the rule of the Caerem. Episc. (1, xii. 17) that more than one light should burn before the altar of the Blessed Sacrament, but always in uneven numbers, i.e. three, five, seven, or more. The lamp is usually suspended before the tabernacle by means of a chain or rope, and it should hang sufficiently high and removed from the altar-steps to cause no inconvenience to those who are engaged in the sanctuary. It may also be suspended from, or placed in a bracket at the side of the altar, provided always it be in front of the altar within the sanctuary proper (Cong. Sac. Rit., 2 June, 1883). The altar-lamp may be made of any kind of metal, and of any shape or form. According to the opinion of reputable theologians, it would be a serious neglect, involving grave sin, to leave the altar of the Blessed Sacrament without this light for any protracted length of time, such as a day or several nights (St. Lig., VI, 248). For symbolical reasons olive oil is prescribed for the lamp burning before the altar of the Blessed Sacrament, for it is a symbol of purity, peace, and godliness. Since pure olive oil, without any admixture, causes some inconvenience in the average American climate, oil containing between 60 and 65 per cent of pure olive oil is supposed to be legitimate material. Where olive oil cannot be had, it is allowed, at the discretion of the ordinary, to use other, and as far as possible vegetable, oils (Cong. Sac. Rit., 9 July, 1864). In case of necessity, that is, in very poor churches, or where it is practically impossible to procure olive or vegetable oils, the ordinary, according to the general opinion of theologians, would be justified to authorize the use of petroleum. We are of the opinion, however, that there are but few parishes that can claim this exemption on the plea of poverty. Gas (Ephem. Lit., IX, 176, 1895) and electric lights (Cong. Sac. Rit., 4 June, 1895) are not allowed in its stead. The Caerem. Episc. (ibid.) would have three lights burn continually before the high altar, and one light before the other altars, at least during Mass and Vespers. Before the Blessed Sacrament, wherever kept, a lamp should be constantly burning. Our bishops have the power of granting permission to a priest, under certain circumstances, to keep the Blessed Sacrament in his house. In such cases, by virtue of Faculty, n. 24, Form. I, the priest may keep it without a light, if otherwise it would be exposed to the danger of irreverence or sacrilege. For the same reason we believe It may be kept also in the church without a light during the night.

Chanzo: CATHOLIC ENCYCLOPEDIA: Altar Lamp
 
Acheni mburo nyie..kwani mleta mada alizungumzia taa makanisani au mwenge mnaoita wa uhuru jamani.?! Msituchanganyie habari ....
 
We ni ---- tuu.nakufatiliaga humu always ni radical huendi na kinachomaanishwa. Kwaio na ubwege wako wewe na lichichiemu lako wote ni wakristo sio kwasabab mnabeba mwenge nakuutukuza mkiamini yesu yu hai? TUMIA AKILI USIWE KAMA KONDOO MWENYE WADUDU KICHWANI

Hayo ndiyo inatakiwa tuachane nayo. Tuliingizwa mkenge.

Mimi toka kujuwa maana ya mwenge, sina hamu nao.
 
Jamani mimi mnanikumbusha mbali sana juu ya hili dubwana liitwalo mwenge tafiti zangu zinaonyesha kipindi cha mbio za mwenge ndio kipindi ambacho ufuska unafanyika sana hasa kwenye vituo ambavyo mwenge unalala hapo usiku huo unakua kama ni sherehe flani hivi hususan kule vijijini…nakumbuka kipindi hicho tupo tosa boys iringa pale siku mwenge ukilala hapo shuleni ikifika asubuhi mnafagia condom za kutosha eneo lote kuzunguka shule,wale wazee wa "mitungo" ndio balaa ni full story za madem waliopigwa mitungo!!!
 
Msipotoshe watanzania,Kila nchi ina nembo yake ya heshima na inayotumika kwenye kila Dola kama ishara ya heshima kwa nchi. Kwenye nembo hiyo utaikuta kwenye kofia za majeshi yao na ni ishara ya utambulisho wa taifa husika. Marekani wana ndege eagle, Zimbabwe Jogoo, Uganda nadhani wana ndege kama sikosei ni Korongo na kadhalika. Sasa mnapoushutumu mwenge wa uhuru ni kwamba mnataka dola yetu isiwe na utambulisho wa heshma kabisa! Je zile nembo kwe crown za majeshi nazo ni ibada hivyo ziondolewe? Karatasi nyingi za kiserikali pia zina nembo hiyo hiyo, je mnataka tuwe na taifa lisilo na utambulisho? Hebu acheni upotoshaji, huu ni mwenge wa Uhuru lazima uheshimiwe.

Hatujadharau ila huo mwenge uwekwe makumbusho, kwani hizo nchi nyingine kama america na nchi nyingine bado wanamkimbiza au kumrusha huyo eagle, au mfano nchi ya uganda umesema wana nembo ya jogoo kwa hiyo kila mwaka serikali yao huwa inaadhimisha kuchinja jogoo kama tunavyofanya sisi kukimbiza mwenge? kwanini usiwekwe katika jumba la makumbusho kuokoa gharama zisizo za lazima?
 
Na mwenge wa olimpic je, make nao unazungushwa duniani
 
Hembu tuambieni nyie wenye kujua Kiingereza.
Mwenge kwa Kiingereza unaitwa?
Hapo ndio tuingie kujua ukweli wa hoja za Faiza Fox na matumizi yake sehem hizo.

Ila kama tafsiri itakuwa moja basi hoja zitawahusu wooooooteee
 
Hembu tuambieni nyie wenye kujua Kiingereza.
Mwenge kwa Kiingereza unaitwa?
Hapo ndio tuingie kujua ukweli wa hoja za Faiza Fox na matumizi yake sehem hizo.

Ila kama tafsiri itakuwa moja basi hoja zitawahusu wooooooteee

Torch..
 
Nimepitia michango mingi ya wadau wa jf kuhusu mada hii na kubaini pasi na mashaka kuwa . Mwenge wa uhuru ni nembo (hai) ya taifa la Tanzania// ndio maana huwekewa ulinzi mkali wa FFU na majeshi mengine ya usalama chini ya Amirijeshi Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama. 0 Ibada ya kuutukuza mwenge huu hufanyika kila mwaka kwa kuwasha na kuuzungusha nchi nzima ikiambatana na sherehe za kuchinja ng'ombe, kutoza sadaka ya mafuta ya kuteketezwa na uzinduzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Zipo tuhuma kuwa mwenge huo ni wa Wakirsto wa madhehebu ya kikatoliki lakini si za kweli kwa sababu ibada ya kusifu na kutukuza mwenge hufanyika na kuratibiwa na viongozi wa chama tawala na serikali chini ya ulinzi mkali wa majeshi yaliyopo chini ya Amiri Jeshi mkuu bila kujali kama ni mkirsto ama Muislamu.
 
Kwa kawaida vita ya kiroho haipiganwi kimwili, ukijaribu kupigana kimwili lazima ushindwe, ikiiwa ni Ibada ya kipepo au ni aina gani ya matambiko au vyovyote vile watajijua hao wanao abudu la muhimu kwa watu wote wanaojua kuwa kuna Mungu wa kweli ni kuishi na kufanya yale yanayompendeza Mungu aidha ni muhimu kuiombea nchi/Taifa kwani yapo mambo mengi ambayo yanafanyika ambayo ni chukizo na laana kubwa kwa nchi. Fikiria Damu ya nduguzetu maalbino, mauaji ya vikongwe, ajali zisizo za lazma yote hayo ni chukizo na Dawa pekee pamoja na kukemewa lakini maombi ni silaha na kinga nzuri ili Mungu asijekutushushia ghadhabu yake
 
Kwa kawaida vita ya kiroho haipiganwi kimwili, ukijaribu kupigana kimwili lazima ushindwe, ikiiwa ni Ibada ya kipepo au ni aina gani ya matambiko au vyovyote vile watajijua hao wanao abudu la muhimu kwa watu wote wanaojua kuwa kuna Mungu wa kweli ni kuishi na kufanya yale yanayompendeza Mungu aidha ni muhimu kuiombea nchi/Taifa kwani yapo mambo mengi ambayo yanafanyika ambayo ni chukizo na laana kubwa kwa nchi. Fikiria Damu ya nduguzetu maalbino, mauaji ya vikongwe, ajali zisizo za lazma yote hayo ni chukizo na Dawa pekee pamoja na kukemewa lakini maombi ni silaha na kinga nzuri ili Mungu asijekutushushia ghadhabu yake

Kuiombea kwa moto?
 
Mwenge wa uhuru uliwashwa siku ya uhuru wa Tanganyika Desemba 9 mwaka 1961 katika kilele cha mlima Kilimanjaro ambao ni mrefu zaidi nchini na barani Afrika ili umulike ndani na nje ya mipaka ya nchi yetu na kuleta matumaini pale kwenye kukata tamaa,upendo pale penye chuki na heshima palipo na dharau.

Katika kutimiza azma hiyo,kila mwaka,tangia enzi hizo mwenge wa uhuru umekuwa ukiwashwa na kukimbizwa nchi nzima kwa bara na visiwani

Kwa mwaka huu mwenge wa uhuru uliwashwa tarehe 29 Aprili 2015 mjini Songea mkoani Ruvuma na unatarajiwa kuzimwa mkoani Dodoma.Mwenge huo ukiwa na ujumbe wa "TUMIA HAKI YAKO KIDEMOKRASIA" JIANDIKISHE NA KUPIGA KURA KATIKA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015 unatarajiwa kukimbizwa katika Wilaya/Halmashauri 168 kote bara na visiwani

Hakuna chembe ya shaka kuwa mwenge umekuwa na mafanikio makubwa kwa Watanzania.Yafuatayo ni baadhi tu ya mafanikio yaliyopatikana na yanayooendelea kupatikana kutokana na mbio za mwenge wa uhuru:-

1.Mwenge wa uhuru umekuwa chachu na kiungo muhimu cha kuimarisha umoja na mshikamano thabiti miongoni mwa Watanzania bila kujali itikadi za vyama vya siasa,rangi,kabila wala dini

2.Mwenge umeimarisha uzalendo na kuwafanya Watanzania kuwa wazalendo katika nchi yao

3.Mwenge umekuwa nembo na alama muhimu ya utambulisho wa Mtanzania na Taifa letu

4.Mwenge umekuwa chachu ya kuhamasisha utekelezaji wa mambo muhimu ya kitaifa na miradi ya maendeleo inayotekelezwa kupitia fedha za Serikali,wafadhali na michango/nguvu ya wananchi.

5.Mbio za Mwenge zimetumika kama sehemu muhimu ya kuwaonya,kuwatahadharisha,kuwaelemisha na hata kuwaburudisha wananchi

6.Kupitia mbio za mwenge wananchi wamepata fursa za biashara na hivyo kuongeza kipato na uchumi wa familia

Hiyo ni sehemu tu ya faida,naamini wana JF mnazifahamu zaidi ya hizo,ongezeeni

Tafadhali;naomba upost tu faida na si vinginevyo
 
Mwenge
 

Attachments

  • 1434128257012.jpg
    1434128257012.jpg
    5.9 KB · Views: 276
Ukihudhuria mbio na mikesha ya mwenge ni dhahiri kuwa,mwenge sio suala la kitaifa bali ni mikutano ya kampeni ya CCM.
Watu wanapiga siasa kwenye suala la kitaifa. Nauliza,je ni mikutano ya CCM au kitu gani?
 
Back
Top Bottom