JET SALLI
JF-Expert Member
- Dec 1, 2014
- 2,392
- 1,578
Kuna watu wengi wamezungumzia hoja ya Mwenge wa Uhuru kwa mitizamo tofauti. CHADEMA katika Ilani yao ya uchaguzi walisema"wakishinda watauweka kwenye Makumusho ya Taifa ili kila anayetaka kuutizama aende huko" Lengo lilikua ni kupunguza matumizi ya fedhayasiyo na tija kwa kukimbiza Mwenge nchi nzima.Wananchi wengine wamenukuliwa wakisema ikiwa Rais Magufuli atazuia Mwenge kukimbizwa nchi nzima atakuwa ameokoa pesa nyingi ambazo zinaweza kutumika kwa shughuli nyingineza maendeleo.Rafiki yangu ambaye ni wakili wa Mahakama Kuu, Egbert Lema anasema dhana ya Mwenge haina tatizo, bali tatizo ni kuukimbiza nchi nzima kwa gharama kubwa.Kwahiyo yeye anashauri ya kuwa Mwenge usifutwe bali mfumo wa kuukimbiza nchi nzima ndio ubadilishwe. Upelekwe Mlima Kilimanjaro ukawekwe pale kileleni ili dhana ya kumulika nje yamipaka yetu iweze kutimia. Ulete matumaini kwa wanyonge, upendo penye chuki na heshima penye dharau.Wapo wanaosema kuwalicha ya athari za kiuchumi, Mwenge pia una athari za kijamii hasa kuzoroteshaafya za watanzania kwani unachangia sana kuongeza maambukizi ya virusi vya UKIMWI. Mara nyingi eneo Mwenge unapolala kunafanyika vitendo vingi viovu vinavyohusishwa na ngono zembe.Anyway; hayo ni maoni ya watu wanavyozungumzia Mwenge wa Uhuru nchini. Lakini je Biblia inasemaje kuhusiana na Mwenge? Katika Kitabu cha Isaya 50:11 neno la Mungu linasema;"Tazama, ninyi nyote muwashao moto, mjifungiao hiyo mienge; endeni ninyi katika mwali wa moto wenu, na katikati ya miengemliyoiwasha. Mtayapata haya kwa mkono wangu; mtalala kwa huzuni."Biblia inasema wanaowasha Mwenge na wale wanaoukimbiza (Waendao na Mwenge ) watalala kwa huzuni. Je ni huzuni ipi hiyo BWANA MUNGU anayoisema? Mimi na wewe hatujui lakini maandiko yanasema WATALALA KWA HUZUNI.Yamekuwepo madai kuwa wale wanaokimbiza Mwenge wamekuwa wakifamuda mfupi baada ya kumaliza kukimbiza Mwenge. Wengine wanasema hufa kwa sababu ya moshi unaotokana na Mwenge huo, lakini wengine wanasema hufa kama tambiko la Mwenge. Mimi na wewe hatujui ukweli ni upi. Pengine wataalamu wa Mwenge wakisoma hapa watatuambia kama kweli moshiwake unaua.Na kama kweli watu wanaokimbiza Mwenge huishia kufa, Je huku ndiko kulala kwa huzuni kunakosemwa ktkBiblia? Mimi sijui ila nachojua ni kuwa Mwenge una hasara kubwakuliko faida. Inapaswa upumzishwe, otherwise waukimbizao Mwenge watalala kwa huzuni.!