Mwenge wa Uhuru upo kwa faida ya nani?
Kuna watu wengi wamezungumzia hoja ya Mwenge wa Uhuru kwa mitizamo tofauti. CHADEMA katika Ilani yao ya uchaguzi walisema"wakishinda watauweka kwenye Makumusho ya Taifa ili kila anayetaka kuutizama aende huko" Lengo lilikua ni kupunguza matumizi ya fedhayasiyo na tija kwa kukimbiza Mwenge nchi nzima.Wananchi wengine wamenukuliwa wakisema ikiwa Rais Magufuli atazuia Mwenge kukimbizwa nchi nzima atakuwa ameokoa pesa nyingi ambazo zinaweza kutumika kwa shughuli nyingineza maendeleo.Rafiki yangu ambaye ni wakili wa Mahakama Kuu, Egbert Lema anasema dhana ya Mwenge haina tatizo, bali tatizo ni kuukimbiza nchi nzima kwa gharama kubwa.Kwahiyo yeye anashauri ya kuwa Mwenge usifutwe bali mfumo wa kuukimbiza nchi nzima ndio ubadilishwe. Upelekwe Mlima Kilimanjaro ukawekwe pale kileleni ili dhana ya kumulika nje yamipaka yetu iweze kutimia. Ulete matumaini kwa wanyonge, upendo penye chuki na heshima penye dharau.Wapo wanaosema kuwalicha ya athari za kiuchumi, Mwenge pia una athari za kijamii hasa kuzoroteshaafya za watanzania kwani unachangia sana kuongeza maambukizi ya virusi vya UKIMWI. Mara nyingi eneo Mwenge unapolala kunafanyika vitendo vingi viovu vinavyohusishwa na ngono zembe.Anyway; hayo ni maoni ya watu wanavyozungumzia Mwenge wa Uhuru nchini. Lakini je Biblia inasemaje kuhusiana na Mwenge? Katika Kitabu cha Isaya 50:11 neno la Mungu linasema;"Tazama, ninyi nyote muwashao moto, mjifungiao hiyo mienge; endeni ninyi katika mwali wa moto wenu, na katikati ya miengemliyoiwasha. Mtayapata haya kwa mkono wangu; mtalala kwa huzuni."Biblia inasema wanaowasha Mwenge na wale wanaoukimbiza (Waendao na Mwenge ) watalala kwa huzuni. Je ni huzuni ipi hiyo BWANA MUNGU anayoisema? Mimi na wewe hatujui lakini maandiko yanasema WATALALA KWA HUZUNI.Yamekuwepo madai kuwa wale wanaokimbiza Mwenge wamekuwa wakifamuda mfupi baada ya kumaliza kukimbiza Mwenge. Wengine wanasema hufa kwa sababu ya moshi unaotokana na Mwenge huo, lakini wengine wanasema hufa kama tambiko la Mwenge. Mimi na wewe hatujui ukweli ni upi. Pengine wataalamu wa Mwenge wakisoma hapa watatuambia kama kweli moshiwake unaua.Na kama kweli watu wanaokimbiza Mwenge huishia kufa, Je huku ndiko kulala kwa huzuni kunakosemwa ktkBiblia? Mimi sijui ila nachojua ni kuwa Mwenge una hasara kubwakuliko faida. Inapaswa upumzishwe, otherwise waukimbizao Mwenge watalala kwa huzuni.!
 
Siku za hivi karibuni kumezuka mtazamo mpya juu ya mwenge, wapo wanaotamani Rais aufute kwa kuwa unatugharimu pesa nyingi sana pia sababu nyingine ni za kiimani zaidi. Pamoja na hayo tumeona mwenge unatumika kuchochea pia kuzindua miradi mingi ya maendeleo nchini pia ni historia kwa vizazi vijavyo. Kwa mtazamo wangu nadhani kabla ya kuufuta ni vyema kwanza kupima faida na hasara za mwenge ndipo tuamue nini cha kufanya au kumshauri Rais
 
Attachments

  • FB_IMG_1448520382922.jpg
    FB_IMG_1448520382922.jpg
    17.2 KB · Views: 432
Siku za hivi karibuni kumezuka mtazamo mpya juu ya mwenge, wapo wanaotamani Rais aufute kwa kuwa unatugharimu pesa nyingi sana pia sababu nyingine ni za kiimani zaidi. Pamoja na hayo tumeona mwenge unatumika kuchochea pia kuzindua miradi mingi ya maendeleo nchini pia ni historia kwa vizazi vijavyo. Kwa mtazamo wangu nadhani kabla ya kuufuta ni vyema kwanza kupima faida na hasara za mwenge ndipo tuamue nini cha kufanya au kumshauri Rais

Miradi inaweza kuzinduliwa bila hata ya mwenge wa uhuru.
Hata hivyo mikesha ya mwenge ni sehemu prone sana ya maambukizi ya magonjwa ya zinaa. Mwenge usitishwe, na pesa zake tununulie vyandarua tujukinge na malaria
 
Ni kweli kwa hili nakuunga mkono
 
pamoja na hayo huo mwenge kuukimbiza ni ghali sana bora usiwepo tu
 
Futa hiyo mizimu ya watawala wa zamani walitaka waTanzania tusifikiri kabisa.
 
Miradi inaweza kuzinduliwa bila hata ya mwenge wa uhuru.
Hata hivyo mikesha ya mwenge ni sehemu prone sana ya maambukizi ya magonjwa ya zinaa. Mwenge usitishwe, na pesa zake tununulie vyandarua tujukinge na malaria

Mkuu umesema kweli...maana shughuli znazofanywa na mwenge mbna ata mkuu wa wilaya anazfanya..kam kuzndua vyumba vya madarasa..mkuu wa wilaya husika anafnya kabsa
 
Unaoitwa mwenge wa uhuru umekua adui yetu mkubwa. Garama za uendeshaji wa mbio za mwenge ni mchwa namba moja kwa kodi zetu. Mikesha ya mwenge inatawaliwa na ULEVI na NGONO:- Uenezaji mkubwa wa VVU.
 
Amani iwe juu yenu wana jamvi.

Katika hali ninayoiona ya Mh. RAIS wetu kukabiliana na mdudu mbaya (GHARAMA ZA SHEREHE ZISIZO ZA MSINGI) na kuelekeza fedha hizo katika matumizi ya lazima. Nami naomba nimshauri juu ya gharama inayotumika kwa kukimbiza mwenge mikoani nalo aliangalie na alichukulie hatua.
 
Uchunguzi umebaini kwamba hakuna mradi wowote uliozinduliwa na mbio za mwenge ukadumu zaidi ya miezi 6 .
 
Leo kwa mara nyingine mbio za mwenge zimeanza tena Tanzania, na safari hii mwenge umewashwa huko Dole Zanzibar kuendeleza ile adhma ya taifa letu changa kuwa "sisi tumekwisha kuwasha mwenge na kuuweka Kilimanjaro". Mwenge huu ulipowashwa mara ya kwanza na kuwekwa kwenye kilele cha Kilimanjaro na Nyirenda, ulikuwa uwe ishara ya matumaini, upendo, na umoja wa Taifa letu.

Matukio ya hivi karibuni hasa baada ya muasisi wa mwenge huo kufa, kuna kila dalili kuwa tunachokimbiza sasa hivi ni kivuli tu cha mwenge ule kwani miale ile ya mwanzo ya mwenge wetu wa uhuru imeanza kuzimika na inaonekana ikififia kila mwaka mpya ujapo. Mwenge huu sasa umekuwa ni alama ya watu wachache kujiangazia wao na familia zao huku sisi wengine tukiendelea kubakia gizani. Hakuna kitu kinachoonesha kufifia kwa mwenge huo kama suala la mikataba ya nishati, madini, ununuzi wa rada, ndege ya rais, n.k Zaidi ya yote kwa wanafunzi waliokwama Ukraine, mwenge huu kwao tayari umezimika ( a little strech there, but why not try..??)

Je kuna matumaini ya kurejesha nuru yake tena? Je kuna haja ya kuuwasha tena ili uendelee "kuwamulika" wabadhirifu, wazembe maofisini, wala rushwa magendo n.k ? Au tuamue kuuzima tu, ili kila mtu ajiwashie mshumaa wake yeye mwenye na wale wenye uwezo wawashe vibatari, chemli, na taa za umeme! ?

huu mwenge kweli tunasababu ya kuendelea kuukimbiza?

Yaani kwa magufuli na uhakika huo msalagambo wa mwenge ndio kwaheri mwaalim. Hatuhitaji kuabudu miungu mingine, kwani uhuru ni mwenge au kazi!
 
Hope wote mmeamka salama kwa kudra za Mwenyezi Mungu,

Naomba nitoe wazo kuhusu huu mwenge wa uhuru unaomaliza mabilioni ya hela huku watoto na wamama wajawazito na wengine wengi wakiteseka.

Naonelea kama mwenge wa uhuru unaonekana bado unamulika maadui, wauweke pale Dodoma maana ni center ili kila mmoja yaani kila mkoa uende pale ku- uwasha maana tumechoka na huu ujinga unaozidi kudidimiza taifa letu.

Naomba mawazo yenu jamani ili tulipeleke bungeni.
 
Nadhani ukiwekwa makumbusho itapendeza zaidi,

Huku Mikoani watu wakimbize mishumaa tu inatosha
 
Hope wote mmeamka salama kwa kudra za Mwenyezi Mungu,

Naomba nitoe wazo kuhusu huu mwenge wa uhuru unaomaliza mabilioni ya hela huku watoto na wamama wajawazito na wengine wengi wakiteseka.

Naonelea kama mwenge wa uhuru unaonekana bado unamulika maadui, wauweke pale Dodoma maana ni center ili kila mmoja yaani kila mkoa uende pale ku- uwasha maana tumechoka na huu ujinga unaozidi kudidimiza taifa letu.

Naomba mawazo yenu jamani ili tulipeleke bungeni.

Mwenge ufutwe tuuu kwani unapoteza pesa za watz, unasababisha ukimwi,

Pesa zipelekwe kukarabat shule kongwe za serekali.
 
Nashauri usifutwe huwa unawasaidia watu wenye ukame ndiyo maana asubuhi wafanya usafi huokota ndom nyingi
 
Back
Top Bottom