Mwenge wa Uhuru upo kwa faida ya nani?
Ndugu zanga Nawasalimu katika jina la Bwana..

Leo napanda jukwaani nikiwa na maswali lukuki na matumai humu nitaweza pata majibu

Mh.RAISI JPM toka aingie madarakani amekuwa akibana matumizi na kufuta vitu vingi ambavyo vingetumia pesa za kodi za walala hoi kama SAFARI ZA NJE YA NCHI,SHEREHE ZA UHURU NA MUUNGANO na pesa hizo zilielejezwa katika miradi mingine

watanzania wengi tulikuwa tunasubiria kwa hamu sana Mh.JPM afute MBIO ZA MWENGE WA UHURU na fedha zake zielekezwe angalau kwenye MADAWATI

Nilikuwa namsikiliza mkuu wa mkoa wa Dar siku ana muapisha Mkuu wa wilaya ya kinondoni na pia mkuu huyo wa wilaya siku anahojiwa Clouds fm alikuwa anasema atajitahidi kukutana na watu nakuitisha harambee watu wachangie madawati

Hivi bajeti ya mwenge wa uhuru ingetengeneza madawati mangapi???

NAOMBA KUWAULIZA WAUNGWANA

Hivi siri ya mwenge wa uhuru ni ipi??na faida za mwenge wa uhuru ni ipi??na je Mwenge wa Uhuru usipokimbizwa Nchi itapata Hasara gani??

Maana naona kama huu nwenge umekuwa mfupa mgumu kwa MH.JPM ambae sio muoga na amefanya maamuzi mengi ya kijasiri kwanini kashindwa Mwenge??????????????


BY MKUMBWA JUNIOR
ARUSHA TZ
 
Ndugu zanga Nawasalimu katika jina la Bwana..

leo napanda jukwaani nikiwa na maswali lukuki na matumai humu nitaweza pata majibu

Mh.RAISI JPM toka aingie madarakani amekuwa akibana matumizi na kufuta vitu vingi ambavyo vingetumia pesa za kodi za walala hoi kama SAFARI ZA NJE YA NCHI,SHEREHE ZA UHURU NA MUUNGANO na pesa hizo zilielejezwa katika miradi mingine

watanzania wengi tulikuwa tunasubiria kwa hamu sana Mh.JPM afute MBIO ZA MWENGE WA UHURU na fedha zake zielekezwe angalau kwenye MADAWATI

nilikuwa namsikiliza mkuu wa mkoa wa Dar siku ana muapisha Mkuu wa wilaya ya kinondoni na pia mkuu huyo wa wilaya siku anahojiwa Clouds fm alikuwa anasema atajitahidi kukutana na watu nakuitisha harambee watu wachangie madawati

Hivi bajeti ya mwenge wa uhuru ingetengeneza madawati mangapi???

NAOMBA KUWAULIZA WAUNGWANA

hivi siri ya mwenge wa uhuru ni ipi??na faida za mwenge wa uhuru ni ipi??na je Mwenge wa Uhuru usipokimbizwa Nchi itapata Hasara gani??

maana naona kama huu nwenge umekuwa mfupa mgumu kwa MH.JPM ambae sio muoga na amefanya maamuzi mengi ya kijasiri kwanini kashindwa Mwenge??????????????


BY MKUMBWA JUNIOR
ARUSHA TZ
Imani ya kishirikina nyuma yake
 
Kwa mwenge ateweza kufanya chochote,coz hilo ndilo shart tulilopewa na mwingeleza...kwamba uwe unakimbizwa kila mwaka
 
Hizo gharama zipo wapi? au imesha editiwa tayari?
 
Mr. Alcohol hawezi kusimamisha mbio za mwege hiyo ni ibada ya kanisa katoliki inatoka vatican na serikali ya tanzanaia niyakikatoliki
 
Kila nchi inautamaduni wake jamani mbona tunapinga kila kitu

Uk wanatumia billions kwa asjili tu ya ufalme ambao upo upo tu

all over the world kila nchi inatunu zake
Bila aibu kabisa unasimama mbele ya kadamnasi na kutema pumba zako, harafu mnajinasibu eti mnabana matumizi pesa yote hiyo mnajaza mitumbo tu
 
Samahani naomba nieleweshwe, hizo billion 11.5 za michango ya wananchi, billion 45 za almashauri ni thamani ya miradi iliyofunguliwa na mwenge? au ni gharama za kutembeza mwenge?

Naomba ufafanuzi mwenye kujua vizuri.

Maake kama ni kwaajiri ya kutembeza tu mwenge itakuwa hatari
Huo ni ulaji wa kuzunguka ma mwenge tu hiyo miradi sisi hatuna habari nayo
 
Jamani nauchukia sana mwenge sijui kwanini natamani magufuli aufutilie mbali.. nakumbuka tumechangishwa sana shule ya msingi kuhusu mbio za mwenge.. sijui faida ya mwenge anayejua anijuze pls
 
Huo Nyerere alipewa na mkoloni na masharti makubwa ni kuwa asiache kuukimbiza kila mwaka sasa ww kijana wa Dot.com plus Big results now (Brn) Huwezi elewa kilichopo chini ya kapeti kuhusu mwenge Hata mheshimiwa hatamani uendelee kukimbizwa but hakuna namna, Pengine shilingi ikigeuzwa upande yani upinzani ikipata dola basi ndo kwisha habari ya mwenge
 
Sitaki. Nasema tena sitaki. Kama mmenichoka chamani mseme. Haiwezekani wakuu wangu wa kichama waniombe kuongeza nguvu kwenye mbio za ninachokipinga:Mwenge wa Uhuru.

Mwenge naupinga. Mwenge siupendi. Mwenge umenichemsha na kunichosha. Mwenye sitaki kuuona wala kuusikia. Mwenge umepitwa na wakati. Mwenge unatumalizia fedha kama taifa. Mwenge ni mzigo kwa taifa. Mwenge upumzishwe. Mwenge uwekwe makumbusho. Mwenge una hasara kuliko faida.

Nasema tena,sitakwenda wala kushiriki kwenye mbio za Mwenge. Sasa watanzania wamesusia mbio za Mwenge. Wanalazimishwa tu kuchangia,kusafisha na kushiriki. Si kama mwanzo. Mwenge huu si ule wakati tupo shule. Huu hauna kipaumbele kama ule. Tafadhali,nisihusishwe nao!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Sasa unamlilia nani....wakati nyinyi huko chaman hamtak kusikia habar ya kuuacha mwenge ....
 
Back
Top Bottom