Mwenge wa Uhuru upo kwa faida ya nani?
Mzee wa Ufipa katika ubora wake. Yeye kila kitu kinachofanywa na Serikali na chama tawala anakipinga. Huyu jamaa ataugua vidonda vya tumbo soon maana siku hizi anaandika kwa jazba na mihemko
 
Mkuu wewe ndiyo unashituka leo, sisi wengine tuliachana na mwenge siku nyingi sana
 
Mzee wa Ufipa katika ubora wake. Yeye kila kitu kinachofanywa na Serikali na chama tawala anakipinga. Huyu jamaa ataugua vidonda vya tumbo soon maana siku hizi anaandika kwa jazba na mihemko
Uzuri,mengi ninayoyakosoa yanafanyiwa kazi. Nyinyi mnaounga mkono kila kitu hamkisaidii chama. Ukitaka kujua level yangu,muulize Mzee Sitta kwenye uspika.

Mzee Tupatupa
 
Uzuri,mengi ninayoyakosoa yanafanyiwa kazi. Nyinyi mnaounga mkono kila kitu hamkisaidii chama. Ukitaka kujua level yangu,muulize Mzee Sitta kwenye uspika.

Mzee Tupatupa
Mzee Sitta alishachoka. Usijitafutie umaarufu. Niambie japo jambo moja tu umepigania ndani ya CCM na linafanya kazi.
 
Sitaki. Nasema tena sitaki. Kama mmenichoka chamani mseme. Haiwezekani wakuu wangu wa kichama waniombe kuongeza nguvu kwenye mbio za ninachokipinga:Mwenge wa Uhuru.

Mwenge naupinga. Mwenge siupendi. Mwenge umenichemsha na kunichosha. Mwenye sitaki kuuona wala kuusikia. Mwenge umepitwa na wakati. Mwenge unatumalizia fedha kama taifa. Mwenge ni mzigo kwa taifa. Mwenge upumzishwe. Mwenge uwekwe makumbusho. Mwenge una hasara kuliko faida.

Nasema tena,sitakwenda wala kushiriki kwenye mbio za Mwenge. Sasa watanzania wamesusia mbio za Mwenge. Wanalazimishwa tu kuchangia,kusafisha na kushiriki. Si kama mwanzo. Mwenge huu si ule wakati tupo shule. Huu hauna kipaumbele kama ule. Tafadhali,nisihusishwe nao!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Mzee VUTA-NKUVUTE duh umenikuna majuzi nimetishiwa na Mwenyekiti wa Kijiji nisipochangia Mwenge nimejiondoa mwenyewe kwenye kijiji chake nasema Kijiji chake si chetu hapana chake nikamwangalia kuanzia utosini hadi miguu iliyojaa sagamba nikampasha hadi hakapashika kwamba mchango wa Mwenge sitoi hata ndururu lau kama ni mchango wa madarasa,ujenzi wa barabara,ujenzi wa msikiti au kanisa nitatoa kwa moyo mweupeee.

Mbio za Mwenge ni ibada nikishiriki kwa mujibu wa Imani yangu maana yake niko nje ya kundi maana yake nimesaliti Imani yangu maana yake nimejiingiza katika Imani nyingine ambayo yaweza kupunguza uwezo wangu wa kufikiri na kuamua mambo.
 
Umeandika vizuri utinzi wa shahiri lako ila umesahau kuweka vina na korasi. Lahasha ungevutia zaidi.
 
Weka jina lako halisi hapa tukujue,,, vinginevyo na wewe walewale tu
 
Leo niko hapa Uhuru Printers. Kuna kazi tunafanya. Uje nikuelimishe.

Mzee Tupatupa
Sina sababu ya kuelimishwa na Mtu ambaye anahitaji kuelimishwa. Subirini Magufułi achukue chama tuone kama hao mawakala wenu wataendelea kupumua
 
mwenge unatumia mabilioni ya pesa kuja kufungua mradi wa milioni ishirini amabao ungeweza kufungulia na mwenyekiti wa kijiji au mzee waheshima kijijini,wanabana matumizi kwa kuzuia bunge live kuwa watu wafanye kazi lakini kunawatu mwaka mzima wanazurula nchi nzima wakicheza disco na kuhamasisha anasa,tathimini ya haraka kila mwenge unapopita unazalisha,maambukizi mapya ya ukimwi,huvunja mahusioano,mimba zisizo tarajiwa zinazo zaa watoto wanaoishi kwenye mazingira magu,huu wote ni mzigo wa serikali na kila mwaka serikali yenyewe inaamua kujitengenezea mizigo ya kuibeba wakati huo inabana matumizi..!! Ukweli usio na chembe ya unafiki tunahitaji serikali mpya,yenye watu wapya na mawazo mapya kiujumla serikali yenye mawazo na maono chanya tuache kuishi na kuongoza kwa historia niwakati wakutungeneza historia nyingine baada ya historia takatifu ilio tukaka ya kina mwalimu Nyerere,unsung hero Kambona,mzee Karume na wengine wengi walioshiriki katika harakati za uhuru,mapinduzi ya Zanzibar na mapinduzi ya ASP na TANU
 
Sina sababu ya kuelimishwa na Mtu ambaye anahitaji kuelimishwa. Subirini Magufułi achukue chama tuone kama hao mawakala wenu wataendelea kupumua
Binti,acha woga. Uje basi hata Lumumba

Mzee Tupatupa
 
Sitaki. Nasema tena sitaki. Kama mmenichoka chamani mseme. Haiwezekani wakuu wangu wa kichama waniombe kuongeza nguvu kwenye mbio za ninachokipinga:Mwenge wa Uhuru.

Mwenge naupinga. Mwenge siupendi.

Mkuu,
Ni jazba? Hoja yako ni ya msingi, hasa unapouliza "je Mwenge bado ni kipaumbele kwa taifa"?
Kwa hiyo kuna vipaumbele vya kitaifa ambavyo hatutaacha kuvisimamia. Lakini kama ni kipaumbele kwa Chama ni vema kikashauriwa kuangalia mambo yenye kukiongezea umaarufu chama kama vile kasi mpya, ari mpya na nguvu mpya ya Rais Dr JPM kwenye kurekebisha mambo nchini.

Majuzi hapa Dar, kulikuwa na kazi ya kupeleka askari Polisi kusimamia uthamini wa mali za mrrathi ya watoto walioachwa yatima. Kumbe siku hiyo mwenge ulikuwa unafanya ziara katika wilaya hiyo. Mkuu wa Polisi Wilaya OCD akaenda na askari wake bila kujipanga ila kazi muhimu ikaonekana ni hiyo ya mwenge na watoto hao hadi sasa wanasubiri 'utaratibu"

Yazungumzeni hayo huko chamani ndiko yatasaidia.
 
Mwenge wetu bwana basi tu! yaani ni bora mkuu wa mkoa afanye makosa katika kumpokea Rais kuliko akicheza na mwenge!!!
 
Back
Top Bottom