Mwenge wa Uhuru upo kwa faida ya nani?
Kila nchi inautamaduni wake jamani mbona tunapinga kila kitu

Uk wanatumia billions kwa asjili tu ya ufalme ambao upo upo tu

all over the world kila nchi inatunu zake

Ningekubaliana na wewe kabisa iwapo tungekuwa tumewaweka watoto wetu wote wa shule za msingi juu ya viti na kuandikia kwenye madawati wawapo darasani - tena baada ya miaka hamsini ya uhuru.
Haya maoni yako ndio ninayaita (kwingineko) WORLDVIEW YA MSOGA (bado tunaedekeza fikira za kiujimaujima, yaani karne ya 17). Etu "kila nchi ina tunu zake"!! Yaani kuwakalisha watoto wa shule sakafuni na kupoteza mabilioni ya pesa kukimbiza alama tu ndiyo TUNU YA TANGANYIKA? (nilitaka kusema tusi hapa, basi)
 
moi wagonjwa wanalala chini,alaf ndio hospitali ya taifa.
 
Kila nchi inautamaduni wake jamani mbona tunapinga kila kitu

Uk wanatumia billions kwa asjili tu ya ufalme ambao upo upo tu

all over the world kila nchi inatunu zake[/QUOTE]SA




sasa huo utamaduni kwa uingereza au ndio top leader wao?au hujui kuwa Uingereza ni nchi ya kifalme,usiwe unatetea -----,bil 11 unajua ni kiwanda kinachoweza ajir watu kadhaa,sasa imagine hizo ni kila mwaka
 
hii nchi ya ajabu sana gharama zote za kazi gani sasa, unatumia mabilioni kuzindua miradi ya mamilioni halafu tunalalamika nchi haina fedha! hii ni sawa na kuuza ng'ombe kwa kesi ya kuku.
Khaa wewe vipi?? Nani kakwambia mwenge ni biashara?? Hii ni siasa haulinganishi mapato na matumizi
 
Unawachangisha masikini mabilioni halafu huku nyuma unapiga Bilioni 200 toka BOT kwa ajili ya manufaa ya wachache. Huu ni wenda wazimu mtupu.
 
Huku bado vijijini wanatembea umbali mrefu kuzifuata huduma za afya na wajawazito kujifungulia chini na upungufu wa madawa na vifaa vya huduma za kiafya,mashuleni vifaa ni hafifu au hamna kabisa,madarasa na walimu ni wachache hapohapo wanafunzi wanakaa chini...laiti kama hizo fedha zingesaidia elimu,afya,miundo mbinu basi angalau hata tungejivunia huo mwenge lakini hamna jipya ni UFISADI MTUPU.
 
Licha ya kutafuna pesa zetu kwa mgongo wa huu mwenge hivi serikali haifahamu kuwa hizi mbio za mwenge huchangia kwa asiliamia kubwa maambukizi ya UKIMWI????Vijijini ndio balaa yaani mwenge ukilala hapo kijijini basi inakuwa kama sodoma na gomora!!!Nachukia sana hizi mbio za mwenge na nadhani ni wakati muafaka watanzania tuanze kupiga kelele mbio za mwenge zikome, na hizo pesa zitumike kuboresha huduma za jamii. MIA

Viongozi wa dini walitakiwa kuwaonya vijana na waumini wao kwenye hili.Unalosema ni kweli kabisa,Mwenge unahamasisha ngono sana kwenye maeneo unamopita na hasa unapolala.Serikali ingeacha hii kitu kwa sasa,haina maana.Kama UPENDO,AMANI,UHURU nk vinaletwa wananchi/watanzania wakipewa haki zao za msingi,Afya,elimu nk.
 
Mwenge wa CCM kuwamulikia mafisadi mali zaidi ili wazikombe!!
 
Kila nchi inautamaduni wake jamani mbona tunapinga kila kitu

Uk wanatumia billions kwa asjili tu ya ufalme ambao upo upo tu

all over the world kila nchi inatunu zake
SA




sasa huo utamaduni kwa uingereza au ndio top leader wao?au hujui kuwa Uingereza ni nchi ya kifalme,usiwe unatetea -----,bil 11 unajua ni kiwanda kinachoweza ajir watu kadhaa,sasa imagine hizo ni kila mwaka[/QUOTE]

Tunazungumzia faida na hasara hauwezi kuwa na tunu zinazokufanya uwe masikini.
 
Baada ya kusoma haya yaliyosemwa na Naibu waziri wa habari Juma Nkamia leo May 27 2014 bungeni, unalolote la kuchangia?

Mtazamo wako kwa ujumla uweke hapa.

Mimi ni mfanyakazi wa NGO moja hapa nchini na ni member wa management katika shirika hilo na moja ya suala ambalo limekuwa linatusumbua sana katika maamuzi kila mwaka ni hili suala la kuchangia mwenge, kila mwaka huwa tunapokea barua kutoka kwa either Mkuu wa Mkoa au Mkuu wa Wilaya ikituomba tuchangie na nikiri kuwa mimi nimekuwa napinga sana suala hili lakini kila mwaka tunachangia kwani CEO wetu huwa anasema suala hili ni nyeti sana na tusipochangiwa shirika linaweza kuwa matatani na kwa kuwa katika hii management kuna wazungu wanaogopa sana na kuamua tuchangie, nimeshangaa sana na nitaendelea kushangaa sana kuona gharama hizi kubwa za ufunguzi na kilele tu ni kubwa kiasi hiki wakati kila siku tunaona madarasa ya walalahoi hayana madawati, kwa mfano juzi kwenye taarifa ya habari ya kipindi kimoja hapa Tanzania tuliona jinsi shule moja ya msingi mkoani Shinyanga wilaya kishapu ikiwa na madawati yanayotosha madarasa mawili tu kati ya saba. Naomba tuendelee kupinga hili suala la mwenge kwa moyo nguvu zote ili lisiwepo, wanaosema mwenge unaleta umoja, maendeleo, uzalendo na kadhalika ni wanafiki wa kutupwa, mwenge unaleta njaa, ukimwi, manyanyaso, umaskini na ubwanyenye. Hatuhitaji mwenge kufungua miradi ya wananchi, hatuhitaji mwenge kufungua guest house za watu binafsi.......hatuhitaji mwenge kuendelea.
 
Kila nchi inautamaduni wake jamani mbona tunapinga kila kitu

Uk wanatumia billions kwa asjili tu ya ufalme ambao upo upo tu

all over the world kila nchi inatunu zake

Stupid argument..............
 
Kila nchi inautamaduni wake jamani mbona tunapinga kila kitu

Uk wanatumia billions kwa asjili tu ya ufalme ambao upo upo tu

all over the world kila nchi inatunu zake

pia UK wanautamaduni wa ushoga , naomba nikutafutie bwana ili udumishe vizuri mila za UK
 
Unawachangisha masikini mabilioni halafu huku nyuma unapiga Bilioni 200 toka BOT kwa ajili ya manufaa ya wachache. Huu ni wenda wazimu mtupu.

Hiyo ndiyo CCM inayotetewa kwa nguvu zote humu na Juliana Shonza aliyefukuzwa chadema kama mbwa
 
Last edited by a moderator:
Samahani naomba nieleweshwe, hizo billion 11.5 za michango ya wananchi, billion 45 za almashauri ni thamani ya miradi iliyofunguliwa na mwenge? au ni gharama za kutembeza mwenge?

Naomba ufafanuzi mwenye kujua vizuri.

Maake kama ni kwaajiri ya kutembeza tu mwenge itakuwa hatari
 

Attachments

  • koroboi.jpg
    koroboi.jpg
    37.7 KB · Views: 86
Back
Top Bottom