Ndugu tofautisha doctrine imani na revelation mafunuo. Doctrine ya mkristo ni kuliamini jina la Yesu Kristo na kuliitia pale inapobidi kwa kukesha na kuomba.
Revelation ni mafunuo ya muda mfupi. Kwa mfano Yesu alipompaka matooe yule kipofu ilikuwa revelation ya muda mfupi sio imani au doctrine. Imani Ni muda wote wa ukristo ila mafunuo ni kwaajili ya muda huo pekee. Ndio maana humuoni Yesu akimpaka matope kipofu mwingine maana ilikuwa kwa wakati na kwa kusudi maalum.
Sasa manabii wa Leo wanatumia mafunuo na kuyanya imani. Yani watu waache kuliitia jina la Yesu Kristo na kuhangaika na mafuta na maji, ukiuliza wanakwambia mbona Yesu alifanya hivi. Njia moja ya kumjua Nabii wa uongo ni pale anapotumia mafunuo kama msingi wa imani.