Nimekuwa niki fatilia sana swala la mkanda uliokua nao kuhusu njama za mauaji.
Nina maswali machache kwako;
1) Mara nyingi umekuwa ukisema ushahidi unao wakutosha kuhusu njama za mauaji, swali ni kwamba kama kweli wewe nimzalendo na mpigania haki, Kwanini usimfichue uyo kiongozi wa CDM Alie kupa mkanda, wote kwapamoja msaidie mahakama kupata data zakutosha? Maana bado kilakitu kinachoonekana kwenye video vinaonekana ni njama zakuiuwa CDM?
2) Nili nukuu maneno yako ukiwa bungeni uliposema pia uko tayari kutoa ushaidi mbingini, Kwa uchungu mkubwa, Mimi nikujuavyo maneno yako mengi huwa ni Tata sana, Mara nyingine hutoa matusi mazito. Kwanini usirahisishe kuwataja waliokupa video ili upate dhawabu kwa Mwenyenzi Mungu? Maana maneno matupu hayavunji mfupa.
3) Wewe na Kijana mtuhumiwa wa Ugaidi (LUDOVICK) Mna mahusiano gani? Maana taarifa zilizopo inasemekana wewe Ndio mfadhili wake, umekuwa ukimtumia fedha napia kuwasiliana nae Mara kwa Mara, ushahidi upo. Wewe usafi wako ni ipo? Uta tudhibitishiaje kuwa wewe ni msafi?
4) Kama mahakama ikigundua kwamba, Ile video ilikuwa yaku tengeneza, kama wasemavyo wataalam wa IT na wasomi.. Huoni utakuwa matatani? Na je ukotayari kuwajibika pale inapo takikana haki kufwata mkondo?
Yapo mengi sana yanayo kuhusu na pia kama ukitaka ushahidi kuhusu wewe kuhusika sema, tutajitaidi ku attach sauti na baadhi ya text message..za tangu mwaka Jana..
Tunaitaji majibu yako ya busara maana tunaitaji, kuweka Hili swala vizuri bila kuegemea upande wowote..
Tunasubiri majibu yako.