Mwigulu Nchemba: Dr. Slaa na Mbowe wakamatwe kwa ugaidi!

Leo nimekosa kuona Bunge kwa hiyo munasema wwamemchokonoa nae akachokonoleka,yaani amejianika kuwa ni master wa hiyo staged video
Anasema anayo na anaweza kutoa ushahidi popote sasa mbona polisi walisema waliitoa JF
Imekuwaje aseme yeye aliipeleka polisi na alipewa na kiongozi mwanadamizi wa chadema, je amelieleza bunge kama huyo kiongozi mwandamizi wa chadema alikuwa ni sehemu ya kutengeneza hiyo video
Dr Slaa na Mbowe wakamatwe kwa sababu ni magaidi aah mwigulu tayari kaliweka swala lenyewe kisias kwisheny mwigulu kwa mantiki hiyo umejishushia credit za kisiasa kwa kasi ya ajabu
Kijana inawezekana unakaswende ya ubongo mara nyingi watu wa aina hiyo huwa wanajichanganya wenyewe umetoa crews zote kwamba wewe ni muhusika namba one, hakika MACCM menzio yenye uelewa watajitenga nawe unaharibu sifa ya chama, mwenzio NAPE alivyopewa ukatibu mkuu alikuwa akiwatukana akina Lowasa Rostam na chenge wakamwambia magamba yamenasa akapotea njia hajui hata aseme nini sasa hivi na wewe punde tuu utakuwa huna nyimbo manake karata yako ya mwisho kuituhumu chadema imeshaisha
 
kwa mambo ya kipuuzi kama haya kujadiliwa bungeni kamwe tanzania hatuta piga hatua....tuna matatizo mengi ya kujadili
 
Kaonyesha ukomavu au ujinga kwa kuruhusu makosa yarudiwe. Hivi kama Lissu akivunja sheria kwa kuingia Bungeni uchi na Spika naye kesho ataingia uchi ili aonekane mkomavu, ni ujinga na wanaom-support ni wajinga.
 
Hii nchi inavyoonekana haina baba wala mama! How come spika anamezea uvunjifu wa kanuni za bunge kisa tu mbunge anayevunja kanuni ni wa chama chake?

The day is coming haya yote yatabaki historia.

mbowe jana vip
 
Ni kweli wakamatwe maana lwakatare hakufanya mwenyewe alitumwa nani aliyemtuma kama si viongozi wake kamata hao tupia keko haraka sana
 
Hivi huyu mwigulu ni mzima kweli kama anataka wenye digrii wakafundishe form 1.2. si aanza yeye kwende yeye kama mfano.
 
Mwigullu Nchemba ANAJIAMINI SANA Kuhusu haya mambo atakuwa na uhakika na kile anachokisema.

zile sms za matusi na matisho ziliishia wap? anadhani watanzania ni madodoki? anazidisha chuki kwa wananchi tu,badala wahangaike na kutimiza ahadi wanabaki kuhangaika na chadema.Jamani mchawi wa ccm ni nyiye wenyewe, hata mtoto wa shule hahitaji kufafanuliwa then cha ajabu ccm kuna wasomi wengiiiiiiiii lakini kumbe ulevi wa madaraka nooma!!!
 
anayehojiwa polisi ni mhalifu. mashahidi wanahojiwa mahakamani. subiri kesi ianze kusikilizwa ndipo ulaumu kama nchemba hatahojiwa
Afadhali sasa mmeanza ku-pre empty kuhojiwa kwake awali mlikuwa mnasema ahojiwe kwa lipi.
 
kwa mambo ya kipuuzi kama haya kujadiliwa bungeni kamwe tanzania hatuta piga hatua....tuna matatizo mengi ya kujadili

kama kiongozi wa upinzani bungen analeta hoja za ajabu kama hizi jana ulitegemea tukae kimya
 
 
Hivi huyu mwigulu ni mzima kweli kama anataka wenye digrii wakafundishe form 1.2. si aanza yeye kwende yeye kama mfano.

we form 1&2 ulifundishwa na form six div0 kama mbowe ndio maana hauna akili hadi hapa jf
 
gaidi huwa hafichwi nikumlipua tu

Ni sawa gaidi kulipuliwa, lakini je imethibitika kwamba hao ni magaidi? na itakuwaje ikithibitika kwamba hao si magaidi maana kesi iko mahakamani.

Nilidhani Mwigulu anajua nini maana ya utawala bora kumbe mbumbumbu wa kiwango cha juu kabisa. unawezaje kuwa mbadala wa mahakama?
 
Afadhali sasa mmeanza ku-pre empty kuhojiwa kwake awali mlikuwa mnasema ahojiwe kwa lipi.

ni kukubali kuwa alipewa cd na kiongoz wa chadema ambaye amekubali kushiliki kupanga mauaji very simple
 
Aliyevunja kanuni ni spika kwa kumruhusu Mbowe kuongelea na Pia wabunge wa ccm hawajui kanuni kwani Kama Mbowe alivunja kanuni kwanini ccm wasiombe mwongozo wa spika? Nakumbuka Mbowe aliishauri serikali kupitia mihimili yake Kama mahakama na bunge kushughulikia swala Hilo ili wanaohusika wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria Huku akitaja viongozi waandamizi wa serikali ya ccm bila kumtaja kwa Jina mwigulu. Sasa mwigulu kawataja Mbowe na Slaa direct. Ifahamike kuwa mawasiliano ya Slaa Mbowe na lwakatare ni lazima maana wanafanya kazi Pamoja sasa JIULIZE mwigulu nae ilikuwaje wawe na mawasiliano na mpinzani wake? Kama Hujui kusoma na picha pia Hujui kuangalia?
 
Hawajifunzi kwa yaliyotokea nchi jirani tu ya Kenya? kama hawajifunzi basi watakuwa hawana mbinu,wananchi ndiyo waamuzi siyo Pilisi wala Mahakama wala chama chochote ingekuwa hivyo basi Uhuru Kenyata asieenda mjengoni.

urais wa kenya unategemea hasa wewe unatoka kabila gani.Ukae ukijua tz siyo kenya na mfano wako hauna mashiko
 
Hivi kuna umuhimu wowote wa baba mwenye nyumba kumwogopa mwanaye? kama CHADEMA ni chama cha magaidi watupu mbona hamjawasilisha The Hague mashtaka yenu? Mwigulu Nchemba unataka kunithibitishia udhaifu wenu katika kuiongoza nchi? Kama kweli Mbowe na CHADEMA ni magaidi basi kusiwe na muda wa kupoteza kubishana bungeni, WAPELEKENI MAHAKAMA KUBWA ZA KIMATAIFA ZIWAHUKUMU au hamjui maana ya CHAMA CHA KIGAIDI (Al-Qaeda). Msitake kukuza mambo ili kuficha upuuzi wenu, TUNA MATATIZO KIBAO

1. Mpaka sasa maelfu ya watoto waliomaliza form four mwaka jana hawajui hatima yao
2. Tunaoishi maghorofani tumepoteza imani ya kuiona kesho
3. Mbeya , Geita na karibu maeneo yote ya nchi bado wanaulizana nani achinje
4. Mwanza tuna mgao wa umeme usio rasmi
5. Wanafunzi wanaozidi 45% hawajaiona hata senti ya mikopo yao, unajua wanaishije?
6. Naomba nijifanye nimesahau hili la nauli kupanda
Na matatizo mengine lukuki ya nchi yetu, hayana hata dalili ya kutatuliwa
Halafu badala ya kutuambia ni lini mtatyatatua mmekaa kujadili CHADEMA na Ugaidi

NDIVYO ILANI YA UCHAGUZI 2010 ILIVYOTANABAISHA? KWAMBA KUPAMBANA NA UGAIDI WA CHADEMA KUFA NA KUPONA?

Ombi langu kwa Mwigulu Nchemba na crew yako ya ccm, Hebu tafuteni kamusi ya kiswahili fasaha kisha tazameni maana halisi ya neno UGAIDI (
Terrorism) kisha fananisheni na hiko mnachodhani ni ugaidi.
Halafu rudini kutatua kero za wananchi,

Au Endelea Na Unachokifanya Ndipo tujue "Mchawi Humkamata Mchawi Mwenzie"

NAWASILISHA
cc: Mwigulu Nchemba
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…