Karibu watu wote wenye kuona Mbali tulifahamu kwamba Mwigulu Nchemba ni lazima atayasema haya anayoyasema , maana ndiyo Move ilivyopangwa , kujua tu kwamba angeropoka uongo hata kabla hajaropoka , Ni ushindi mkubwa ! Siku za Mwigulu kwenye Siasa zinahesabika .
Kwa hili mimi napingana kabisa na wewe ki msingi spika hana makosa kwani hata jana kwenye hotuba ya Mbowe kama ulifuatilia vizuri alizungumza maneno makali sana na kwa suala hili alimlenga Mwigulu moja kwa moja na Mwigulu alikuwepo alitulia tuli sasa tatizo nini Mwigulu kujibu hoja leo. Mimi nadhani paia Mwigulu kasaidia kasema yupo tayari kutoa ushahidi popote tatizo ni nini? Kama CHADEMA kitaendeshwa kwa kila kitu kuona kuwa kinaonewa ni ngumu sana kukijenga chama na kwa utaratibu huu nina wasiwasi mkubwa kama wakipewa madaraka ya nchi watakuwa ma dictator kwani siku zote dictator hapendi kukosolewa
Sio Mwigulu tu hata Spika naye ni tatizo
Spika Anna Makinda, ameruhusu Kiongozi wa Upinzani Bungeni kushambuliwa, kuhusu matokeo yake akiwa Shuleni, akaruhusu CHADEMA waitwe wauaji, akakataza waliotaka Mwigulu afute kauli Bungeni, akashangilia pamoja na Wabunge wengine wa CCM waliokubaliana na maneno hayo].
MAKINDA JAMANI!:nono: MUNGU AMSAMEHE NAJUA ANAMLINDA BOSI,ILA AJUE WATANZANIA WANAUMIA KWA AFANYAYO. MKUU NIMEKUNUKUU KWAN UMEONGEA POINT.
Akichangia bungeni muda huu Mwigulu Nchemba amesema yupo tayari kutoa ushahidi popote pale iwe polisi, mahakamani bungeni hata mbinguni kuthibitisha video ya Lwakatare jinsi alivyoipata, na kwamba kiongozi wa CHADEMA aliyempa pia yupo tayari kuthibitisha mahali popote. Amewataka viongozi wa chadema wasitafute mchawi kwa kusingizia vyombo vya dola hasa polisi na usalama wa taifa kwamba vinahusika.
Amesema ni vyema viongozi wa chadema popote pale walipo waende kwenye nyumba za ibada zilizopo karibu nao wakatubu na kuungama kujisafisha na matendo maovu ya kigaidi na mauaji wanayoyafanya. amewashangaa kutaka madaraka huku wanawaua wananchi wanaotaka kuwaongoza...awaambia shame on you, look at you chadema!!!!!
Amesema ile ya chadema iliyowasilishwa na mbowe ilikuwa ni malalamiko ya kambi ya upinzani na sio hotuba ya kambi ya upinzani kwa kuwa haina mapendekezo wala solution ya matatizo pamoja na kwamba ina urefu wa kurasa 70.
Amelitaka jeshi la polisi limkamate Mbowe kwa sababu ndiye anayewasiliana sana na LWAKATARE kwa kuwa ni mkurugenzi wao wa ulinzi na usalama, kufuatia maelezo ya mbowe jana kwamba anayewasiliana na gaidi naye ni gaidi pia hivyo akamatwe..
omba ajira clouds patakufaa! una lafudhi kama ya kina kibonde!
Sijui wamekumbwa na upofu gani kushindwa kuona kuwa mwisho wao ni 2015.mwingula yukokwenye hatamu kwa hiyo anayo haki ya kuyasema hayo lakini akumbuke kila enzi inaomwisho cjui wakati huo atakuwa mwingula yupi
Wanao ruhusu kuchezea rasilimali za taifa pamoja na mkeo ndo wapo makini?
Hivi huyu jamaa anajua mziki wa engineers au keshalewa madaraka, lets wait and see 2015 is coming.....!!!Huyu mwehu huyu ...eti Ma engineer wakafundishe shule za kata...alaf walipwe acccordingly...wakati hao tu walimu wameshindwa kuwalipa...
Ati Viongozi wa CHADEMA ndio Magaidi na wauaji ...na yupo tayri kutoa ushahidi na pia aliyerecord video ile yupo na yupo tayari kusema chochote..
Ati "You look Messless,shameless...look at you "
Kiongozi huyu ni mfano wa kuigwa kwani anajiamini, hapendi dhulma na pia namuomba mungu aonyeshe na kuwadhalilisha waovu wote wanaochonganisha serikali na wananchi,
viongozi gani hawaamini jeshi la polisi, mahakama bunge n.k?