Mwigulu Nchemba: Serikali imekusanya bilioni 48 kutoka kwenye Tozo za miamala ya simu kwa wiki nne

Mwigulu Nchemba: Serikali imekusanya bilioni 48 kutoka kwenye Tozo za miamala ya simu kwa wiki nne

Naipongeza Serikali kwa hilo

" Sincerely licha ya malalamiko kuwa mengi kumekua na descending curve kwenye graph ya mapato(Tozo) agaist muda. "
 
Hivi TRA iliacha kukusanya kodi?
Kama inakusanya zinafanya kazi gani, maana maendeleo yote tunachangia.
Au TRA inakusanya kodi ili kulipa mamilioni viongozi wezi?
 
US $2.9bn kule Stiegler's Gorge

US $2.9bn kule Stiegler's Gorge Rufiji Tanzania ni Mzigo mwingine aliotwikwa mwananchi kwa staili ya miradi ya kimkakati iliyoanzishwa kwa wakati mmoja na miradi mingine mikubwa

14 August 2021

Construction of Julius Nyerere Hydropower Station 45% complete​

Construction of the Julius Nyerere Hydropower Station; the largest in the East African Community (EAC) has reached 45%. The US $2.9bn project is expected to add 2,115MW into the national grid.

The US $2.9bn hydropower station project is being constructed across the Rufiji River in eastern Tanzania. The station is expected to produce 5,920GWh of power annually. The power generated will be evacuated via a new 400kV high voltage power line to a substation where the power will be integrated into the national electricity grid. The government of Ethiopia is advising the Tanzanian government on the implementation of this project.

Source : Construction of Julius Nyerere Hydropower Station 45% complete
 
Hivi na yeye kipindi hiki angeambiwa akatwe tozo kama hizi za sasa hivi, angekubali kweli?

View attachment 1899463

MAONI YANGU:

Andika barua ya kujiuzulu, hufai kuwa Waziri Wa Fedha kwasababu ni muongo kweli kweli.
Hivi kipindi hicho,nani alikua Waziri wa fedha!? Maana alikua na huruma sana, Mtu Kama huyo umtoze Kodi kweli!?
 
Mh Madelu kaongea akiwa composed sana leo na kujishusha, ile ya kutuambia tuhamie Burudi ni pepo kisirani lilimkumba tu kwa bahati mbaya ya wezekana alisahau kuomba asubuhi siku ile shetani akambeep/deep. Huyu ameonesha kukomaa kiuongozi kwa sasa na atamsaidia Mh Rais SSH sana kama hatavurugwa na wapambe nuksi.

Alikaribisha mawazo. Atuambie atafanya nini kwenye mafuta ya petrol yashuke bei ikiwa tunaambiwa nchi jirani bei ni ahueni comperatively na zinapitishia shehena ya mafuta hayo kwenye bandari zetu? Hii neema ya bandari Mungu aliyotupa kwa nini wanashindwa kuitumia vilivyo? Wanakwama wapi?

Kasema wamekusanya 48B kwenye tozo kwa hardly 4 weeks. Na uwiaono ni shs 10: shs 400 au 1:40 kwa serikali: Makampuni ya simu. Kwa maana nyingine kipindi hicho hicho makampuni ya simu yamekusanya mabillioni mengi tu kulinganisha na serikali huu si uwizi wa wazi tunafanyiwa na hizi kampuni za simu? Serikali inafanya nini juu ya hili?

Mgao wa afya umependelewa kuliko elimu sijui kwa nini? Wakati yanahitajika madarasa 10000 kabla ya Januari. Hii trend itaendelea kila wanapopanda kidato. Hawaja fikiria Walimu, chaki, matundu ya vyoo na madawati nk

Wasijifariji na kauli za postive -negative baada ya muda tozo zitapungunguza kasi ya kukua kwa uchumi kutokana na kuongeza muda wa kufanya transections. Watu wanaendelea kujipanga katika kupata njia mbadala, week 4 hazitoshi kufikia hitimisho. Mh Mwiguli kaonesha anaweza kuwa Daniel wa awamu ya sita kumsaidia Mh Rais wa JMT SSH.
 
Kuna mawaziri wawili ambazo kwa kweli wananitia hasira sana huyu na Ummy
 
Bagambilana : miradi yote 5 ya meli itagharimu Sh bilioni 438.8.

Tunamuenzi JPM miradi ya meli​



RAIS Samia Suluhu Hassan amesema mikataba mitano iliyosainiwa jana Mwanza ya ujenzi na ukarabati wa meli ni kazi nzuri ya kumuenzi Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano, John Magufuli ambaye ni mwanzilishi wa miradi hiyo.

Aliyasema hayo jijini Mwanza baada ya kuzindua chelezo, meli ya New Victoria ‘Hapa Kazi Tu’ na meli ya New Butiama ‘Hapa Kazi Tu’ pamoja na kushuhudia utiaji saini wa mikataba mitano ya ujenzi wa meli mpya nne na ukarabati wa meli ya zamani.

Rais Samia alisema anajisikia faraja kushuhudia kukamilika kwa ukarabati huo wa meli, kusainiwa kwa mikataba na kukamilika kwa ujenzi wa chelezo.

“Kama ingekuwa haijakamilika roho zetu zisingejisikia vizuri kwa sababu mwanzilishi wa miradi hii ameitwa na Mungu na ameitika, kama anatusikia bila shaka anafarijika,” alisema Rais Samia.

Alisema ni dhamira ya serikali kuifanya Mwanza kuwa kituo kikubwa cha biashara kwa kuwa Mwanza iko kwenye ukanda wa mikoa wazalishaji wakubwa wa mazao wa chakula na biashara na mazao ya uvuvi, hivyo serikali itaendelea kuimarisha miundombinu ya usafiri na usafirishaji na miundombinu laini ya kuboresha mawasiliano ya kimtandao.

Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli, Philemon Bagambilana alisema ukarabati wa meli hizo ulianza Januari 2019 kwa gharama ya Sh bilioni 27.6 na zilianza kufanya kazi tangu Agosti mwaka jana.

Alisema meli ya New Victoria ina uwezo wa kubeba abiria 1,200 na tani 200 za mizigo wakati New Butiama ina uwezo wa kubeba abiria 200 na tani 100 za mizigo.

“Meli ya New Victoria inafanya safari zake mara tatu kwa wiki kati ya Mwanza na Bukoba kupitia Bandari ya Kemondo, na meli ya New Butiama inafanya safari zake kila siku kati ya Mwanza na Nansio Ukerewe,” alisema Bagambilana.

Aliongeza, “Ujenzi wa chelezo nao ulianza Januari 2019 kwa gharama ya shilingi bilioni 36.4, ni chelezo kikubwa kupita vyote katika Ziwa Victoria.”

Alisema meli ya New Victoria ilitengenezwa mwaka 1960 na meli ya New Butiama ni ya mwaka 1980.

Kuhusu mikataba mitano iliyosainiwa, alisema mkataba wa kwanza ulihusu ujenzi wa meli mpya katika Bahari ya Hindi kwa kulenga soko la Comoro na mkataba wa pili unahusu ujenzi wa meli mpya ya mizigo katika Ziwa Victoria itakayokuwa na uwezo wa kubeba tani 3,000 za mizigo kwa kulenga ujio wa Reli ya Kisasa (SGR).

Mingine ni ya ujenzi wa meli mpya ya mizigo katika Ziwa Tanganyika; wa nne ni ujenzi wa meli mpya ya abiria na mizigo katika Ziwa Tanganyika itakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria 600 na tani 400 za mizigo, na mkataba wa tano ulihusu ukarabati wa meli ya Mv Umoja yenye uwezo wa kubeba abiria 1,200 na pia ina reli ndani yake.

Bagambilana alisema miradi yote hiyo itagharimu Sh bilioni 438.8.

Source : MSCL
 
Nadhani hapo wanataka kuwaangushia zigo makampuni ya simu yapunguze ada lakini tozo ziendelee kuwepo.
 
👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏✔✔✔✔✔✔✔✔✔👏👏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏



I believe sasa kila mwezi serikali itaweza fikia 2 trilioni au zaidi kidogo, hongereni sana Mh. Rais Mama Samia, na Waziri wa Fedha, Dr. Mwigulu Nchemba na Watanzania wote. Tulipe tozo jamani, mtaona maendeleo
 
YÜTEK Shipbuilding 180 million dollars contract

The Turkish shipbuilding industry signed 4 new shipbuilding contracts to the Tanzania Ministry of Transport within the framework of its African expansion.

YÜTEK Shipbuilding Industry Company signed a new ship contract for the Tanzania Ministry of Transport to build 2 general cargo, 1 passenger and 1 wagon ferry ship. It was learned that the cost of the project was 180 million dollars.

Read more : YÜTEK signed 4 new shipbuilding contracts to Tanzania Ministry of Transport
 
Wakuu,

Waziri wa Fedha, Dr Mwigulu Nchemba anazungumza na waandishi wa habari muda huu kuhusu miradi ya Serikali pamoja na Tozo za miamala ya simu pamoja na mafuta. Kuwa nami kukujuza yanayojiri
Zikitumika vzr,zinaweza kuleta matokeo mazuri,ufanyike utaratibu hata mikopo ya Elimu ya juu ikusanywe namna hii,
 
Pesa zinakuzanywa na kupelekwa kwenye matumizi bila ya utaratibu maalumu, si ndo kutakuwa na upigaji wa kiwango cha lami?
Huu utaratibu wa kufanya projects na matumizi bila ya kupitia bunge aliuanzisha mwendazake , na naona imekuwa ni kanuni kwa sasa .
Haya tumekusanya billion 48 , sawa , zimeenda kujenga zahanati na nk, sawa pia , ni nani anaratibu zahanati ipi ijengwe wapi na kwa gharama zipi?
 
Hivi madini yetu yanatufaidisha vipi muheshimiwa waziri...

Napata wakati mgumu sana kuona tunakomaa na tozo sijui za miamala, kodi za nyumba kupitia LUKU...

Madini madini madini....hii nchi ni tajiri kwenye hili lakini mbona hakuna uwiano wa madini yaliyopo kulinganisha na tunavyofaidika???
 
Piga kazi jembe, mengine yatajisema yenyewe hapo baadae! kubwa kuwe na ukweli tu katika hizi takwimu (zisitolewe kisiasa kwani haina maana yoyote) na zifanyiwe kazi husika inayosemwa (kuwe na usimamizi usio na huruma kwa wafujaji)........tuone hayo mabarabara na mazahanati yenye huduma na mambo mengine mengi ya kimaendeleo.

Bado tuko nyuma sana kimaendeleo kama nchi na huu ni mwanzo tu na ni lazima uwe mgumu (matusi, kuchukiwa, kejeli, kukatishana tamaa, kuzodolewa n.k) lakini kukiwa na matokeo chanya baadae, hao wanaokejeli sasa ndiyo watakaosifia kazi kubwa inayofanyika hapo baadae.

Hisia haziishi kuniambia kuwa hii nchi ikipata viongozi wabunifu, wajanja kiuchumi na 'makatili' dhidi ya wahujumu uchumi, wavivu, wenye kulalama lalama au mapingapinga tu siku zote badala ya kufanya kazi n.k; itakimbiliwa kama inavyokimbiliwa south africa kwa madiba.........au itakuwa nchi ya watu wenye furaha sana. maliasili tele, ardhi kubwa, water bodies za kutosha, amani na urafiki wa watanzania unaochagizwa na lugha yetu kuu ya kiswahili vipo pale kufanya hayo yote yawezekane. ni sisi tu kuamua.

Hatika nchi ambayo bado watoto wanakaa chini madarasani, wilaya kibao bado hazijaunganishwa kwa lami, usafiri wa ardhini haujaboresheka vya kutosha, ajira ni shida n.k, lazima ukatili utumike katika kuanza......mama endelea kuanza kama hivyo

Tafsiri yangu ya kiongozi mkuu wakati mwingine ni kuthubutu kufanya jambo kubwa ambalo kama ukikosea (ingawa sio lengo) basi ukosee sana na ukipatia basi upatie haswaaa. hili likisimamiwa vema, serikali itakuwa na pesa na miradi mingi itaenda vizuri na sote tutafaidika kama taifa. hapo utakuwa umepatia sana mama na hilo ndilo waungwana tunaloomba. matusi yetu, kejeli, zetu na kila aina ya chokochoko vitakoma matokeo yakionekana.
 
Wakuu,

Waziri wa Fedha, Dr Mwigulu Nchemba anazungumza na waandishi wa habari muda huu kuhusu miradi ya Serikali pamoja na Tozo za miamala ya simu pamoja na mafuta. Kuwa nami kukujuza yanayojiri

==========
Umenikaba koo nilipe na umezikomba kwa lazima toka mifukoni kwangu sasa unajitapa! Mungu anakuona.
 
Back
Top Bottom