Mwigulu Nchemba: Tunawafuatilia wanaopotosha na kuzushia viongozi vifo

Mwigulu Nchemba: Tunawafuatilia wanaopotosha na kuzushia viongozi vifo

Waziri wa katiba na sheria amesema wanawafuatilia wote wanaozushia watu vifo. Na hatua kali zitachukuliwa dhidi yao. Mpaka sasa kuna baadhi wameanza kushughulikiwa.

Mh waziri hata watoto wa vigogo utawachukulia hatua?View attachment 1723074
Huyu Mwigulu ni waziri wa nn tena mpaka anaanza kufuatilia waharifu?
 
Huyu Mwigulu ni waziri wa nn tena mpaka anaanza kufuatilia waharifu?
Wahenga walisema: Kila kabila lina mwerevu wake na mpumbavu wake. Leo tunayaona mubashara. Singida ina Tundu wake na Madilu wake.
 
Kazi hiyo ni ya Waziri Wa Mambo Ya Ndani na TCRA, Jeshi la Polisi wala TCRA hazipo chini ya Wizara yake mpaka atoe amri za kamata kamata na kufanya uchunguzi wa Cyber Crime, yeye kazi ya Wizara yake ni kuandaa proporsal za marekebisho ya sheria na katiba.

Apunguze speed ya kuusaka Urais 2025, kujua kwingi mwisho ataharibu.
Anadhani bado yuko Mambo ya ndani?.
 
Viongozi anamaanisha nini? Amaanisha Mbowe? Anamaanisha John mrema pia? Anamaanisha mbeba maono Tundu Lissu pia? Au anamaanisha wahuni ambao hata wakihojiwa zilipo trillioni 1.7 wanataka kuua watu?
Angeanza na gazeti la TANZANITE, limeripoti kuhusu vifo vya John Mrema na Freeman Aikale Mbowe, tena limetaja hadi sehemu walizo fia, Mbowe kafia Dubai na Mrema kafia S.A. Tusianze kuandikia mate wakati wino upo.
 
Duh,mi imegoma kabisaaaa
Mpk VPN,hata VPN wakati mwingine inagoma!
Km hizi siku 3 imegoma sijui nifanyeje jmn
Mwigulu anza na wale waliomzushia Mrema (Katibu Mwenezi wa CHADEMA) kifo huko South Africa. Viongozi wetu wakizushiwa vifo mnacheka. Wa kwenu akizushiwa mnakuwa mbogo. Watu wa ajabu sana nyie!
 
Kuruhusu baadhi ya watu ambao hawana mbele wala nyuma kuleta taharuki ni failure. Kwa nini msifanye kweli?

Twita na VPN zifungiwe daima. Maana huko wamejaa watu wasiofaa hata kiduchu.

Kama mnaona huruma basi washughulikiwe huko huko walipo. Hamjifunzi jinsi Urusi na China wanavyofanya juu ya watu kama hawa?
 
Back
Top Bottom