Mzee Makamba: Watu wazuri huwa hawafi ndio sababu Kinana yupo na Jakaya yupo!

Kama amesema haya kweli basi ana matatizo. Hivi anataka kutuambia kuwa wale wote waliokufa walikuwa watu wabaya na walikuwa hawapendwi?
Aidha, anaona kweli fahari kuwa baada ya miaka 60 ya utawala wa chama chake bado wananchi wanahitaji "maji, umeme, huduma bora za afya na elimu"!
Na anaamini kuwa wanapata faraja kwa kuona kuwa baada ya miaka yote hiyo mahitaji yao yapo kwenye ilani ya CCM.
Hapa si anawapigia debe wapinzani akina Chadema?

Amandla...
 
Huyu Mzee anaudhi sana,hv anatonaje sisi wananchi

Sent from my V2026 using JamiiForums mobile app
 
Ni kweli watu wazuri huwa hawafi maana fikra, matendo na mitazamo yao hudumu milele. Na ndio maana pamoja na jitihada zote za kuzima fikra na mitazamo ya watu hao wazuri bado wabaya wanaoishi, wameendelea kufedheheka. Mmojawapo akiwa yeye huyo ambaye pamoja na uzee wake lakini anazidi kuharibu kila kukicha kwa kukosa hekima na busara!


Your browser is not able to display this video.


Heri mwisho ulio mwema!
 
Aseme tu kwamba WEZI na wanaoruhusu WIZI huwa hawafi
 
Umenena mzee. Kitabu cha mithali kinasema Mtu mwema akishika madaraka mioyo ya watu hufarijika lakini asiyehaki akikaa kitini mioyo ya watu huugua.

So hayo ni matokeo ya mioyo kufarijika. Baada ya kuugua kwa Muda mrefu.
 
Mtume Muhamad bado yupo hai? Asimkufuru Mungu huyu mzee. Au mtume alikufa akiwa na Umri gani?
 
Nimeumia sana kwa hii kauli ya huyu mzee.. amekufuru. Nimeuliza swali hilo hilo Je Mtume Muhamad alikuwa na Ubaya gani? Na hao aliowataja wakacheka bila kukemea wanafahamu kweli Dini?
 
Umenena mzee. Kitabu cha mithali kinasema Mtu mwema akishika madaraka mioyo ya watu hufarijika lakini asiyehaki akikaa kitini mioyo ya watu huugua.

So hayo ni matokeo ya mioyo kufarijika. Baada ya kuugua kwa Muda mrefu.
Wazazi wako wote wapo? Wataishi miaka yote? Ndugu zako? Wewe Dini gani kama unayo.... Msikubali mtu aongee upuuzi kama huu.
 
Huyu mzee mbona anazeeka vibaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…