Mzee Makamba: Watu wazuri huwa hawafi ndio sababu Kinana yupo na Jakaya yupo!

Mzee Makamba: Watu wazuri huwa hawafi ndio sababu Kinana yupo na Jakaya yupo!

Kejeli hizo akumbuke dunia uwanja wa fujo tu tunapita chuki yake isimfanye asahau kua hata yeye siku moja ataiacha dunia
Jamaa anachuki na mu ambaye hayupo kujibishana nae, nimgemuona wa maana kama hizo chuki angezionyesha wakati jamaa yupo hai tungemuona wa maana, kisa cha chuki ni mwanawe kutemwa uwaziri, mzee huyu kasahau kuwa kila nafsi itaonja mauti, hizi kauli za hovyo zilitakiwa zikemewe hapo hapo kikaoni lakini kwa kuwa CCM imebaki jina basi wapambe wamebaki kupiga makofi, kwa hakika CCM ilishaondoka na mwalimu JK Nyerere, na hawa wa kuja ndio wanajifanya ndio wenye CCM, nasubiri kama Mzee Msekwa na Mzee Mangula wataweza kukemea upumbavu huu.
 
Malaika????ndugu mahabba yasikupe upofu ,Malaika kiongozi wao tayari wanayo sasa huyo anaetaka majukumu yasiyo yake atakula kipondo tu
Ninachojua mimi " watu wema hawadumu" angalia JPM ambae alikuwa mkombozi wa Tz hakudumu. Labda Mungu alitaka akaongoze malaika wake.
 
Sasa mtu kama huyu hizo chuki zake kwa Magufuli utasema ni kwa sababu ya nia njema kwa nchi na watanzania? Jana katoka kuongea maneno ya dharau yasio wapendeza watanzania halafu leo anasema watu wazuri hawafi na mfano wa hao watu wazuri ni JK na Kinana kwamba wapo hai hawajafa kwa sababu ni watu wazuri!!!
Mungu hadhihakiwi. Kesho atatuonyesha uzuri wao.
 
Hicho ndio kizazi cha uchawi wazee hawana nasaha zozote njema kwa chama toka wadukuliwe. Umbea wao kama wanawake wamekua watu wa hovyo unamsema marehemu ambaye hawezi kujitetea ajabu hii

Kumsema marehemu ndiyo namna ya kikatili kabisa ya kuwaumiza wafuasi wake.

Ukatili unazidi kupanda chati kwenye siasa za Tanzania.

Jamaa aliyesema “sadism is inevitable when the situation is alarming” alionekana mahiri sana na kushangiliwa na watu hawa hawa ambao leo wanalalamikia kumnanga marehemu bila kujua kwamba hiyo ndiyo sadism yenyewe.
 
Siku zote binadamu anapanga yake na Mungu ameshapanga yake.

Kesho ipo mbali Sana kwetu sisi binadamu,,
Tusiifikirie kesho kutwa kabla hatujaimaliza Leo..

2025 ni mbali Sana.
 
Kagame yuko hai, museveni yuko hai, Nyerere hatunae tena, Karume hayupo, wala uhai sio kitu cha kutolea mfano wowote, watoto wao kua na vyeo wasipofushwe macho mambo hubadilika saa na muda wowote
Kweli kabisa mkuu. Unaweza kuta mwaka huu usiishe mara Mwezi wa Kwanza anakufa, sijui Baba yetu Mauzi atasemaje? Atasema mwanae alikuwa mbaya ndiyo maana kafa?? Nadhani anapaswa aombe msahama mbele ya hadhara ili jamii imsamehe otherwise ulimwengu wa roho hutenda mambo tusiyoyajua. Maana kifo hata uwe nani wote tutakufa tu.
 
..Mzee Makamba ni kama mtu aliyetupa jiwe gizani, sasa kuna watu wenye hatia wanadhani walengwa ni wao.
 
Back
Top Bottom