Kitu pekee alichojaliwa ni ujasiri wa ajabu kupindukia. Kupoteza binadamu wenzako au hata kuwabambikia kesi watu wasio na hatia, siyo kila mtu anaweza.
Unawapoteza binadamu wenzako, familia zao zinalia na kuomboleza, halafu wewe unaona kawaida kabisa, na moyoni una amani, watu wa namna hiyo ni wachache sana Duniani, na hata wakiwepo, jamii zinazojali utu na uhai wa binadamu, haziwezi kukubali wapenye kwenye uongozi.
Na nina hakika wengi wenye akili walipata funzo. Mzee yupo sahihi kwenye jambo moja, siyo rahisi mtu wa namna ile kupenya kwenye uongozi.