Alimwambia bosi wake Rais Mkapa, kuna mambo makubwa tunaweza kufanya bila kubembeleza wazungu. Barabara ya kwanza kujengwa Tanzania kwa hela ya ndani lilikuwa wazo lake.
Ameishi na amekufa na imani hiyo. Hotuba ya ziara yake ya mwisho akizindua stendi ya D'Salaam akatamka, "tuliwaomba barabara ya njia mbili wakaturingia, tunajenga wenyewe ya njia 8." Uwanja ukarindima, wananchi wakaamsha vichwa juu, vifua mbele.
Hata Nyerere hakuwahi kuwatamkia wazungu "msituringie."
He was a visionary and had brass balls.