Mzee Mohamed: Tuna kazi kubwa sana kumuandaa kijana atakayefanana na Magufuli

Mzee Mohamed: Tuna kazi kubwa sana kumuandaa kijana atakayefanana na Magufuli

MZEE Mohammed Juma, Mkazi wa Unguja Zanzibar amesema kama Taifa tuna kazi kubwa sana kumuandaa kijana atakayefanana na Hayati Dk. John Pombe Magufuli na alikubali lolote limfike lakini Tanzania isonge mbele

“Tuna kazi kubwa sana ya kumuandaa kijana atakayefanana na Magufuli, tuna kazi kubwa sana , yule mzee aliingia pale hakuwa na tamaa yoyoye aliingia pale kwa niaba ya kuijenga Tanzania na alikubali lolote limfike lakini Tanzania isonge mbele” Mzee Mohamed Juma Mkazi wa Unguja, Zanzibar Tanzania.

Pumbavu
 
Hilo ni kweli tupu. Jana nilipita sehemu panapoendelea ujenzi sgr nikaona kazi inavyotembea na nikajisemea kweli Magufuli alikuwa kichaa. Kichaa mwenye maamzi magumu aliyekuja wakati mwafaka kabisa. Ndani ya miaka yake mitano aliweza ibadili tz kwa miundombinu pamoja na mambo mengine mazuri kedekede.

Nb. Kichaa si tu mwehu bali pia mtu mwenye maamzi magumu na mzee wa kazi kazi

Mbona SGR imebuniwa 2005. Yeye Ni mtekelezaji sio mwasisi
 
MZEE Mohammed Juma, Mkazi wa Unguja Zanzibar amesema kama Taifa tuna kazi kubwa sana kumuandaa kijana atakayefanana na Hayati Dk. John Pombe Magufuli na alikubali lolote limfike lakini Tanzania isonge mbele

“Tuna kazi kubwa sana ya kumuandaa kijana atakayefanana na Magufuli, tuna kazi kubwa sana , yule mzee aliingia pale hakuwa na tamaa yoyoye aliingia pale kwa niaba ya kuijenga Tanzania na alikubali lolote limfike lakini Tanzania isonge mbele” Mzee Mohamed Juma Mkazi wa Unguja, Zanzibar Tanzania.

Weeh mzee weeh!!
Hamna haja ya kumuanda! Wako wengi tu SEMA shida kubwa ni hii ukoo wa Panya CCM unaotafuna na kupukuza! Nafasi zinapewa walewale tu watu wamestaafu wanarudishwa kazini!

Isitoshe wako vijana mahiti upande wa pili mfano halisi ni mkoswakoswa wa risasi akiwepo huyu unayempa sifa! Inawezekana kabisa kuwapatia wenye uchunguzi na nchi hii.
 
shika adabu yako Mzee Mohamed hakusema ameongea kwa niaba ya watanzania wewe ndio umesema hayo maneno yeye ameongea hisia zake, Watu wazuri hawafi inawauma baada ya kampeni yenu ya SUKUMA Gang kugonga mwamba sasa mnaanza kutapatapa kuona wazanzibari wako na JPM
Ahaa wako na Jpm wapi ahera au mbinguni
 
Hakuna ndoa yoyote batili Kati ya CCM na dola isipokuwa kupitia sanduku la kura. Mimi siku zote nipo tofauti na CHADEMA na vyama vingine vya upinzani kwenye Jambo hilo. Mitaani na vijijini huko watu wengine hawavijui wala hawavifahamu vyama vingine vya upinzani leo mzee Dovutwa sijui yule mzee wa ubwabwa anakuja na yeye anadai kaibiwa kura.

Wacha nikukumbushe tena mtaa ninaoishi Mimi wanachama wa CHADEMA hawazidi hata 80 wakati wanachama wa CCM wapo zaidi ya 5000 bila kuhesabu watoto na wakinamama. Upinzani hauna watu mitaani na huku mitandaoni wanapojivunia napo sio pa kuamini.
Hiyo ni dodoma tu mikoa ya wajinga na masikini ccm imetamalaki na ndio ngome yao,ndio maana ccm haitaki kupunguza umasikini
 
Huyo mzee ni nani katika nchi hii,mnaokota wauza kahawa mnawarekodi wanaongea kwa niaba ya watanzania
Kwahiyo wewe ni nani katika hii nchi hadi upingane na mzee Mohamed.

Kwani kuuza kahawa sio kazi inayompatia riziki?

Mmeanza dharau zenu wauza nchi.
 
Alimwambia bosi wake Rais Mkapa, kuna mambo makubwa tunaweza kufanya bila kubembeleza wazungu. Barabara ya kwanza kujengwa Tanzania kwa hela ya ndani lilikuwa wazo lake.

Ameishi na amekufa na imani hiyo. Hotuba ya ziara yake ya mwisho akizindua stendi ya D'Salaam akatamka, "tuliwaomba barabara ya njia mbili wakaturingia, tunajenga wenyewe ya njia 8." Uwanja ukarindima, wananchi wakaamsha vichwa juu, vifua mbele.

Hata Nyerere hakuwahi kuwatamkia wazungu "msituringie."

He was a visionary with big brass balls.
 
He was a visionary and had brass balls.
Yuko wapi sasa,kumtukana mzungu adharani ni sawa na kulala na kahaba bila kinga utakufa
 
Ni miongoni mwa waasisi wa Afro Shiraz Party Zanzibar acha kucharau watu na amezungunza kupitia Channel Ten kituo kinachomilikiwa na Chama cha Mapinduzi
Ana umri gani hata akawa muasisi wa ASP? Au amerithi uasisi kwa baba yake?
 
Kama mlijua anakubalika hivi why mkapora uchaguzi hivi unajua Jimbo nalotokea hatukufanya uchaguzi wa ubunge Wala kata sababu CCM walipiga bila kupingwa ila eti kura za Urais turnout ilikua 90%!!!! Imagine

Hizi hoja zenu zingekua na ukweli kama mngeruhusu demokrasia Ili angeshinda kihalali wote tungeziba mdomo ila Kwa rafu zile nani atapinga kuwa alikua sio popular kama mnavyomkuza humu.
Mawazo Yako waliomchaguwa MAGU na wabunge ni wengi mno angalia mazishi Yako na wanavyo mkumbuka niushaidi tosha aliwagalagaza vibaya
 
Eti hakuna rais Kama magufuli, mnalazimisha watu uongo. Kila Rais alifanya yake akaondoka. Haya ya kulinganisha Marais mmeanza nyie msiojua nchi imetokea wapi mpaka hapa ilipofikia. Kama Marais waliopita wangeweka misingi mibaya hata huyo magufuli asingefanya lolote.

Ila Ni kweli hakuna Rais aliyewahi kufia madarakani zaidi ya magufuli hapa Tanzania Bara.
Sasa chuki zimetoka wapi? Nchi imetoka wapi kwani we hujui!!
 
Back
Top Bottom