Mzigo wa wazazi kulea mabinti na watoto wa binti zao

Sisi WANAUME utatulaumu bure mwisho wa siku anayebaki na msala ni binti
 
Wakishaacha watoto nyumba huwa wanakuja mjini kuwataftia chochote kitu.ukienda mbele ukirudi nyuma hawa masingo mama hulea sana familia zao
Si sawa usemalo. Nina mpwa wangu alizaa nje ya ndoa na tena mtoto ana sickle cell, lakini amemuacha nyumbani kwao, dada yangu na mumewe ndiyo wanalea. Wanapeleka hospitali kutwa. Yeye yupo mjini anahangaika kutafuta vibarua ambavyo nina uhakika ni dada yangu anamjazilizia ili apitishe mwezi.

Tatizo kuu ni binti kujidai kuwa anazaa na kwao wana uwezo wa kumtunza mwanae. Ukiwa na msimamo kama wangu hamleti. Maana akiibeba nahakikisha anaitoa kavu, unless anaichukua mimba itumzwe na aliyempa, au baba ya aliyempa au ndugu wa aliyempa; si kwangu!
 
Sisi tuliozalisha tunawatunza mpaka wanajitegemea sasa. Ni uhanithi kutupa damu yako mwanaume.
 
Mambo mengine haya ni ya kuomba Mungu atupishilie mbali.

Mazingira yanaweza kuwa tofauti hadi ukashangaa.

Waliona mbali sana waliotambua kutokuwatukana mamba kabla ya kuvuka mto.
Ni kweli mkuu ila inauma sana tena sana..
Pia ukali unahitajika hapa
 
kuna wale wazazi wa kike wanaosaidiana na mabinti zao kutoa mimba ili mtoto aonekane kijana, kwa kweli sitapenda kuona wanangu wanazalishwa wakiwa nyumbani lakini ikitokea hivo kwa kweli atakwenda leba na huyo kijana nitawaozesha wakalee mtoto wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…