Mzigo wa wazazi kulea mabinti na watoto wa binti zao

Ulifanya vyema ingawa mzazi alikua anaona kama unamnyima haki ya kua na wajukuu zake.
Ila kaka hongera 😂..umetimiza neno
 
Mimi hua napenda kuwaambia wanagu kwamba...
Kama ukiona hauna uwezo wa kumlea mwanao basi usizae
 
Hapa ngoja kwanza nikae kimya nina wadogo 2

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Yani mama ako aliteseka kukulea wew na wew unaendaa kukutana na wanaume wa KATAA NDOA unajichanganya mwisho wa siku hata matumizi hatoi. Ubaya unaenda kuongeza na wengine aisee sema kuna wazazi wapole sana ilaa huu ujinga UCHAGANI kidogo sijauona ila mikoa kama mbeya aisee ni balaa ndo maisha yao
 
Yaani baba ndio yeye mwenyewe amkague binti yake mwenye miaka 25,kweli jamani
 
Tumesha fika ukomo dada, ila wananinyoosha....😓
Na hiyo ndiyo Raha ya kua nao Sasa..kichwa 24/7 kinapata moto..wao kwanza before kitu chochote..bado vijitabia vyao vya Raha na karaha..huna budi endelea kupambana kaka katika Hali zao zote..na endelea kumshukuru Mungu kwa ajili yao😊
 
Dah mkuu umenichekesha sana, hakika inaumiza sana na ni janga kubwa sana. Kuna kajamaa kaliwahi kumdunga mimba dada yangu halafu eti kakamkataa mazima hapo ndo nilipojua na sisi wanaume tuna kaukatili. Sio mbaya maisha lazima yaendelee tumekubali yaishe dogo anakuwa.
 
Hii fomula nasikia ipo nchini Botswana,kule kwao wanaume ni wachache kwaiyo wazazi wakule wakikuta jirani yao ni mjamzito waaanza kuwekeana oda,ikatokea nyumba A kazaa wa kiume na nyumba B kazaa wa kike basi palepale familia mbili zinaungana uhusiano katika malezi ya watoto hao
 
Halafu madogo kama hao Mungu anawasaidia sana kuwa na bahati katika maisha,unaweza kuta uyo dogo mbeleni akawa na maisha mazuri ndio hapo utakapoona jamaa anavyojipendekeza kurudisha majeshi
 



Halafu wengine huwa wanaenda kifundishwa uchawi !
Utakuwa mtihani sana kwenye maisha yake Na yao!
Ni maaagano mazito sana!
 
Wachawi wengi hurithishwa uchawi wakiwa na umri mdogo .
Pale ambapo Mtoto akitishwa anatishika!

Wengi hufundishwa uchawi wakiwa wakubwa hukataa katu ingawa kwa kufanya hivyo wengine huuliwa kabisa ma kufa vifo taanishi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…