Na hii ndio maana halisi ya ule msemo wa kusema Mungu ni roho

Ok,sijaweza prove kama kuna roho(kwa maana nimekwambia kwamba ni religious terminolgy)

Lakini nimekwambia kitu gani kuhusu religion?(nimesema kwenye religion hakuna sehemu ya kuprove kitu kwa maana tayari kila kitu ni ukweli kwa mtazamo wa dini)

Something to be subjective kwa mara ya kwanza unatoa chance for opinions(kwamba kila mtu anaweza kuwa na mtazamo wake)

Ndio katika "Buddhism" wanasema hakuna roho(huu ni mtazamo wao) hii haiwezi kuwa true katika Islam au christianity.

Siwezi kuonyesha kama kuna roho au hakuna kwasababu roho is religious terminology(kwa maana katika dini hakuna sehemu believer anaulizwa prove existence of something).

Kama roho is real or not real(sio jambo la believer,scientists can prove , but guess what spirit is beyond science)

Labda kuweka mambo sawa.Topic ambayo inaweza kuwa na debate ni ile tu inayoruhusu watu kupinga topic pale inapokuwa generalized(kwa mfano, niseme wanaume wote ni hovyo.Hapa natoa room for debate but what if wewe useme mimi(mwanaume) ni hovyo(hapa hakuna debate kwa maana ushatoa hitimisho)).
 
Mpaka sasa, kwa kipimo cha uthibitisho kuangalia nini ni kweli na nini ni imani tu isiyo na uthibitisho kuwa ni kweli, uwepo wa roho ni jambo la imani tu, si ukweli, si fact, na hujaweza kuthibitisha roho ipo kama ukweli, kama fact, kama kitu kilichothibitishwa.

Unakubali au unakataa?
 
Kama mtu wa dini nakubali kuna roho.Kwanini nimefikia hitimisho hili? Ni kwa sababu nimetumia msingi wa imani ambao ni muongozo kwa wenye kuamini(dini).

Kama wewe sio mwenye kuamini hauna sababu ya kuniuliza ni prove kwamba kuna roho(kwa maana nimetoa hitimisho na sababu ya kwanini nimefikia hitimisho hili)

Wewe ambaye ni mwanazuoni unatakiwa uje na kauli yako ambayo inaonyesha hakuna roho na sababu za kufikia hitimisho hilo sio kuniuliza mimi tena(Hii ni sawa na mtu wa CHADEMA akwambie kwamba Mbowe ni mwenyekiti wetu.Then,kwa sababu wewe ni CCM useme hapana afu uwaulize watu wa CHADEMA kwamba prove to me kuwa Mbowe ni mwenyekiti wenu(sio mtu wa siasa nimekupa kama mfano tu))
 
Kwenye dini amini chochote unachotaka, huko hakuhitaji fact.

Sijakuuliza dini wala imani, nimekuuliza fact, ukweli.

Roho ipo?
 
Kwenye dini amini chochote unachotaka, huko hakuhitaji fact.

Sijakuuliza dini wala imani, nimekuuliza fact, ukweli.

Roho ipo?
Nimetoa majibu ya kila kitu(sijui jibu gani unataka hapa?)

Roho ipo ndio(na sababu nimekupa kwamba wanatheolojia wamekubaliana hivyo kutokana na ufunuo katika vitabu vya biblia(dini)).
 
Nimetoa majibu ya kila kitu(sijui jibu gani unataka hapa?)

Roho hipo ndio(na sababu nimekupa kwamba wanatheolojia wamekubaliana hivyo kutokana na ufunuo katika vitabu vya biblia(dini)).
Kitu haiwi kipo kwa sababu wanatheolojia wamekubaliana hivyo.

Kwanza wanatheolojia hata hawajakubaliana hivyo. Wanatheolojia wa ki Buddhist hawakubali roho ipo.

This is a fallacy, argument from authority.

Thibitisha Mungu yupo.
 
Angalau wewe umekuja na hoja fikirishi ambayo inazidi kusiriba imani yangu ya kusema Mungu ni roho iliyo na mwili.
Imani yako ni batili kwasababu unachokiamini hakipo kwenye uhalisia.
 
Yesu alivyofufuka alikuwa na mwili wa namna gani?tafakari hilo kisha utajijibu maswali yote uliyoyauliza hapo juu.
Yesu kufufuka ni stori tu ambazo watu walitunga kupitisha agenda zao.

Hakuna kitu kama hicho kuwahi kutokea nje ya hadithi tu.
 
Kitu haiwi kipo kwa sababu wanatheolojia wamekubaliana hivyo.

Kwanza wanatheolojia hata hawajakubaliana hivyo. Wanatheolojia wa ki Buddhist hawakubali roho ipo.

This is a fallacy, argument from authority.

Thibitisha Mungu yupo.
Umeuliza kuhusu fact si ndio? Nimekupa tafsiri ya fact ni nini(moja ya tafsiri ni kwamba, fact is something agreed by group of experts and play a role in how they perceive something)

Sasa unapokataa msimamo wa wanatheolojia unataka msimamo wako ndio uonekane sahihi sio?(msimamo wako utakuwa sahihi lakini mimi sitautumia kama reference sehemu yoyote ile)

God does exist(nshakwambia sio kazi yangu kuprove bali mimi nakumbushwa kuamini na nikakupa wewe nafasi ya kuprove wrong kwa kutumia discipline yoyote unayopenda)
 
Nimekwambia hata wanatheolojia hawajakubaliana kuhusu uwepo wa roho.

Wanatheolojia wa ki Buddhist hawakubali kuwa roho ipo.

Tatizo wewe ulimwengu wako unaishia kwenye dini yako tu.

Nimekwambia pia kusema kitu ni fact kwa sababu experts wamekubaliana ni logical fallacy, argument from authority. Google that.

Anayesema roho ipo ndiye mwenye mzigo wa kuthibitisha ipo.

Anayesema Mungu yupo ndiye mwenye mzigo wa kuthibitisha yupo.

Thibitisha roho ipo.

Thibitisha Mungu yupo.
 
Tatizo sio mimi, tatizo ni wewe tu ambaye unadhani kila kitu kitafuata misingi ya kisayansi ku-draw conclusion.

Buddhism scholars kukataa kuwepo kwa roho haifanyi kwamba existence ya roho iko nullified(hapana).Kwao hii ndio perception yao na ndio ukweli wao lakini kundi jingine(hapa naongelea christians,Islamic scholars,Jews,just to make list shorter) wamekubaliana kuna roho na sababu wametoa kwamba kuna ufunuo katika vitabu vyao.

Kama ambavyo wanasayansi wanapishana katika mada tofauti tofauti ndio hivyo katika theology au discipline nyingine.

Nimekupata nafasi, onyesha ni kivipi hakuna roho umeshindwa sasa unataka mimi nifanye nini wakati nishakupa hitimisho kwamba roho ipo na sababu za hitimisho hili nikakupa
 
Umesema wanatheolojia wamekubaliana roho ipo, lakini tumeona hata wanatheolojia hawajakubaliana.

Wewe unayesema roho ipo ndiye mwenye mzigo wa kuthibitisha ipo. Usinipe mzigo huo mimi.

Thibitisha roho ipo.
 
Umesema wanatheolojia wamekubaliana roho ipo, lakini tumeona hata wanatheolojia hawajakubaliana.

Wewe unayesema roho ipo ndiye mwenye mzigo wa kuthibitisha ipo. Usinipe mzigo huo mimi.

Thibitisha roho ipo.
Mimi nimekupa hitimisho(I have nothing to prove here.Siwezi toa hitimisho nikakupa na steps nilizopitia kudraw conclusion then ukaniuliza tena ni prove)

Mwanasayansi anapofanya observation,aka create hypothesis,akafanya data gathering and analysis ya data,mwisho wa siku aka draw conclusion then kesho ukamuuliza prove to me(wewe unakuwa kichaa.Mwenye akili atarudi field aje na model ya kupinga findings zake then aifanye public tayari kwa critism)
 
Hujathibitisha roho ipo, hujathibitisha Mungu yupo.

Unahubiri imani yako tu.

Thibitisha Mungu yupo. Thibitisha roho ipo.
 
Hujathibitisha roho ipo, hujathibitisha Mungu yupo.

Unahubiri imani yako tu.

Thibitisha Mungu yupo. Thibitisha roho ipo.
Ndio nahubiri imani kwa sababu ndio msingi wa dini(wewe hapa ulitaka nifanye experiment kuonyesha kwamba Mungu yupo sio?(siwezi))

Mungu yupo na roho pia ipo(Huu ndio msimamo wa dini na miongozo ya dini.Hakuna mtu kakukataza kusema tofauti lakini make sure unakuwa na model ambayo inapinga ukweli huu na ufanye presentation publicly huku ukisubiri critism.Sio tu kuja kuniuliza prove wakati nimesema religion haina nafasi hiyo ya kuprove(kwa maana msingi wake ni imani)
 
Hujathibitisha Mungu yupo, hujathibitisha roho ipo, unalazimisha imani yako iwe ukweli wakati hujathibitisha Mungu yupo wala roho ipo.
 
hizi story zauongo bhan 😔
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…