Na hii ndio maana halisi ya ule msemo wa kusema Mungu ni roho

umejuaje? hakuna hio kitu bhan
 
sorry mtu wa dini ivi roho kazi yake niipi kwa mtu na binadam.?
 
Ukitaka kuwa chizi tafuta kumjua Mungu kimwili...

Ndicho nilichoona hapa.

NB: Wanaoongozwa na Roho wa Mungu hao ndio wana wa Mungu
 
Roho ipo na ni uhai ndio maana tupo hai, ikiondoka kwenye mwili, ndio mtu anakufa,
Roho = Uhai
Roho ipo
Uhai ni nini?

Virusi vina uhai au havina uhai?

Virusi vina roho au havina roho?
 
Uhai ni chanzo cha maisha
Kila kiumbe kina Roho, Nafasi na Mwili katika ulimwengu wa kishikika (Physical),
Body - Power
Soul - Intercessor/ Coordinator/ Conductor
Spirit - Energy, source
 
Sasa mbona umejibu theluthi moja tu?
Virus sio viumbe hai -
Viruses are not made out of cells, they can't keep themselves in a stable state, they don't grow, and they can't make their own energy. Even though they definitely replicate and adapt to their environment, viruses are more like androids than real living organisms.
 
Haya, bacteria nao je? Wana roho?
 
Haya, bacteria nao je? Wana roho?
Bacteria ni viumbe hai kwa sababu Wana seli (Cell) ambayo ndio imebeba nishati ya uhai ambao chanzo chake ni Roho tofauti na Virusi wasiokua na Seli (Cell) hawana hiyo nishati ya uhai mpaka wawe ndani ya kitu chenye hiyo nishati uhai
 
Roho unaithibitishaje kibaiolojia? Unaithibitishaje kimaabara?
 
Roho unaithibitishaje kibaiolojia? Unaithibitishaje kimaabara?
Roho ndio chanzo cha nishati iliyopo kwenye seli (Cell), na ndio uhai, kibaiolojia Roho ni nishati ( Energy) inayotegemeza uhai na kwenye viumbe imehifadhiwa kwenye seli (cell), seli zikiwa Kamilifu zinatoa nishati hiyo ya kutosha na zikiwa dhaifu nishati hiyo hupungua na kiisha na kisababisha hitilafu mpaka mwisho wa uhai kwa kiumbe kutokana na kukosa nishati
Roho unaithibitishaje kibaiolojia? Unaithibitishaje kimaabara?
Nishati iliyopo kwenye seli ndio imetoka kwenye Roho sawa na maji kutoka kwenye chemchemu
Roho= Chemuchemu
Nishati= Maji
 
Kwa hivyo unaiita nishati roho?

Mtu akifa, nishati haitoki mwilini mwake. Lakini mnasema mtu akifa, roho inatoka.

Hapo kuna contradiction inayoonesha roho si nishati.
 
Kwa hivyo unaiita nishati roho?

Mtu akifa, nishati haitoki mwilini mwake. Lakini mnasema mtu akifa, roho inatoka.

Hapo kuna contradiction inayoonesha roho si nishati.
Mtu akifa maana yake mwili umekua disconnected na chanzo cha nishati yake yaani Roho, yaani mwili umefeli kupokea nishati kutoka kwenye Roho, ndio mtu anakufa, wanaposema kukata Roho Yani nishati itokayo rohoni (uhai) imekwisha ndio maana maisha ya mwili yanakomea hapo,
Roho ni Chanzo Cha Nishati Ya Uhai, Bila hiyo nishati ya uhai mwili haufanyi kazi.
 
Unajichanganya. Roho ni nishati au chanzo cha nishati?

Kibaiolojia chanzo cha nishati ya mwili ni jua. Tunakula vyakula vilivyopata nishati ya jua na kutumia nishati hiyo.

Hiyo roho haijawahi kuwa proved kuwa ipo kwenye maabara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…