Nabii GeoDavie: Biblia sio neno la Mungu bali ni maneno ya wanadamu

Nabii GeoDavie: Biblia sio neno la Mungu bali ni maneno ya wanadamu

Natamani kujibu ila hii mada fikirishi ni ndefu sana.

Ni kweli lengo la kuteketeza maandiko matakatifu yasiwepo lilifanywa ila halikutimia.

Ni kweli kuna aya kwenye maandiko matakatifu ziliongezwa kwa matakwa ya kibinadamu hasa wakati Roman empire ikifikiria namna ya kuunganisha upagani na ukristo.

Ni kweli kuna maneno yaliongezwa ili angalau kuleta tafsiri inayoeleweka kutokana na uhaba wa maneno yaliyofaa kutafsiri kutoka kwenye lugha za kale za Kiebrania, Kiaramu pamoja na kigiriki. Mfano ni Biblia ya kwanza ya Kiswahili ukiisoma sasa hivi huwezi elewa kitu kwa sababu ya lugha mbovu iliyotumika.

Kuna mambo mengi sana yahusuyo Biblia watu waliyapotosha kimakusudi ila angalau sasa kulingana na teknolojia kukua kumefanyika tafiti za kureejesha maandiko matakatifu ya zamani baada vitabu vya kale kuvumbuliwa.
 
Km hashindwi kwanini asimuue shetani ambaye kwa maelezo ya biblia ndiye adui yake mkubwa..!! Nikuulize swali dogo.

Hivi wewe unaweza kuwafungia watoto wako chumba kimoja na simba kisha ukawaacha wajiokoe wenyewe ili kuwapima km wana nguvu?? Ni kweli utakua unawapenda hao watoto wako?
Mfano wa simba na watoto ni mfu,shetani siyo adui mkubwa wa Mungu bali wa binadam..na kwa nini amuue!?
 
Watoto wamepewa nyenzo za kujiokoa na simba kutozitumia nyenzo hizo Mungu analaumika vipi sasa.
 
Mazingira yanabadilisha vipi DNA?

Kwamba wewe ukiwa mwafrika mweusi na mke wako ni mwafrika mweusi vilevile, Mkienda ulaya mtazaa mzungu?

Mkizaana wote weusi kwa wakati wote haiwezekani atokee mzungu from nowhere kwenye ukoo na vinasaba vyenu.

Labda mmoja wenu akazae na mzungu ndio itatokea hivyo.

Unless otherwise, haiwezekani.
Mkuu Hapa Naomba Nikurekebishame DNA inabadilika Mkuu
 
Majini na binadam Wana freewill, tofauti na malaika
Kama malaika hawana freewill, ina maana kwamba hawaamui kwa uhuru wao na maamuzi yao wenyewe, Wana amuliwa na huyo Mungu.

Basi huyo Mungu alidhamiria kabisa shetani aweze kumuasi.

Na kwa maana hiyo, Huyo Mungu atakuwa ni mjinga sana.
 
Upepo upo unasikika ukivuma na kujulikana upo.

Upepo upo unapimika.

In Meteorology, Tunapima upepo kila siku kwa kutumia vifaa kama Anemometer na Windvane.

Hii ni kwa sababu upepo upo na unathibitishika upo.
Unaamini upepo upo kwa athari zake na si kwamba unauona,unaamini umeme upo kwa athari zake kwa taa kuwaka,tv kuwaka lakini huuoni
Mimi naamini Mungu yupo kwa athari zake kwa kutazama mazingira yanayonizunguka na mimi mwenyewe umbile langu.

Mimi kuwa na kinywa chenye meno na mate kwa ajili ya kusaga chakula,kisha kuwa na njia inakipeleka tumboni kwenye mifumo ya umengenyaji Ili nistawi,kisha kujulikana kwamba si chakula chote kitamengenywa,makapi yatabaki na yatatakiwa kutoka,pakawa na njia ya kutoa makapi nje ya mwili tena mwili ukini-alert...hiyo ni athari/dalili ya kuwepo mhandisi aliyehandisi huo mfumo

Kuona si kwa macho tu bali hata kwa akili
 
Huyu ni mjinga mmoja asie na akili timam.
Arusha ana wafuasi kama mchwa, Acha wajinga waliwe😃😃
 
Kama malaika hawana freewill, ina maana kwamba hawaamui kwa uhuru wao na maamuzi yao wenyewe, Wana amuliwa na huyo Mungu.

Basi huyo Mungu alidhamiria kabisa shetani aweze kumuasi.

Na kwa maana hiyo, Huyo Mungu atakuwa ni mjinga sana.
Unapompa mwanao uhuru wa kukutii na kutokukutii si ujinga,bali maamuzi yako tu
 
Mfano wa simba na watoto ni mfu,shetani siyo adui mkubwa wa Mungu bali wa binadam..na kwa nini amuue!?
Biblia inasema “Mungu aliupenda Ulimwengu hata akamtoa mwanae wa pekee ili aje kuukomboa Ulimwengu” Hapo inamaana yeye mwenyewe kashindwa kumdhibiti shetani anatumia sub “Yesu” ambaye naye kazaliwa na binadamu.!! Hivi Yesu naye kule mbinguni alitokea wapi?
 
Unaweza kufikiri na kusadiki chochote.

Unaweza kufikiri na kusadiki hata kitu cha uongo ambacho hakipo.

Ukishindwa kuthibitisha uwepo wa hicho unacho kifikiri na kukisadiki, ni kwamba hakipo.

Na kufikiri kwako ni uongo tu.

Mimi nakwambia specifically Mungu hayupo.
Kutokuwepo maana yake ni nini? Maana hapa ndo tatizo lilipo.
 
Mkuu Hapa Naomba Nikurekebishame DNA inabadilika Mkuu
Sawasawa.

Sasa mazingira ya nje yanabadilisha vipi DNA ya ndani mpaka utofauti unatokea.

Mimi swali langu liko hapa, Je inawezekana vipi mwafrika mweusi azae mtoto mweupe na mwafrika mwenzake mweusi ambapo mtoto huyo atafanana kabisa na mchina mweupe?
 
Wewe uliyesoma, Eleza hapa jinsi mazingira yanavyo badilisha DNA?

Wewe si msomi uliyesoma?

Sasa eleza ni jinsi gani mazingira yanabadilisha DNA.
Kuna sababu nyingi za kutokea nje zinazopelekea kutokea badiliko kwenye DNA hasa zikidumu kwa muda mrefu kwa mtu husika...

1. UV radition kutoka kwenye Jua.
Hizi zinapelekea kutengenezwa kwa kitu kinaitwa Thymine dimers, kikawaida Thymine bases huwa zinafanya pairing na Adenine lakini kwenye uwepo wa UV radition inapelekea Thymine inafanya muunganiko na Thymine kutoka upande mwingine.

Hili linaweza kupelekea Mutation.

2. Chemicals zinazopatikana maeneo husika kama Moshi wa Tumbaku na Kemikali za Viwandani hivi vyote vinapelekea badiliko la DNA

3. Viruses na baadhi ya Biological Agents wanaweza kupelekea kubadilika kwa DNA.

Hizo ni Baadhi ya External Factors, lakini pia kuna Natural Causes.

Sasa kwa huo ujinga wako Nakuomba tena RUDI SHULE
 
Biblia inasema “Mungu aliupenda Ulimwengu hata akamtoa mwanae wa pekee ili aje kuukomboa Ulimwengu” Hapo inamaana yeye mwenyewe kashindwa kumdhibiti shetani anatumia sub “Yesu” ambaye naye kazaliwa na binadamu.!! Hivi Yesu naye kule mbinguni alitokea wapi?
Niliandika awali katika kukujibu kwamba biblia siyo rejea yangu
 
Mungu muweza wa vyote Aliumbaje binadamu wasio na utii?

Mungu muweza wa vyote, Alishindwaje kuumba binadamu watakao mtii siku zote na wakati wote?

Hivi huyo Mungu ana jielewa kweli?
Mungu sio dikteta amekupa freewill uchague mema au mabaya
 
Back
Top Bottom