Naibu Waziri Mkuu majukumu yake Kikatiba ni yapi? Wafahamu waliowahi kuwa Manaibu Waziri Wakuu nchini

Naibu Waziri Mkuu majukumu yake Kikatiba ni yapi? Wafahamu waliowahi kuwa Manaibu Waziri Wakuu nchini


Nanukuu sehemu ya uzi wa ndungu Petro E. Mselewa, uliopo hapo juu...

"Kikatiba, Mhe. Rais yuko sahihi. Ibara ya 36, Ibara Ndogo ya 1 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inampa Rais, pamoja na mambo mengine, kuanzisha na kufuta nafasi za madaraka ya namna mbalimbali katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Inasomeka:

36.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katika Katiba hii na ya sheria nyingine yoyote, Rais atakuwa na mamlaka ya kuanzisha na kufuta nafasi za madaraka ya namna mbalimbali katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano." .. Mwisho wa kunukuu
Nadhani hujaelewa
 
Nianze kwa kusema Ulale Pema Peponi Shujaa Magufuli

Sitashangaa kijana wako Dr Dotto Biteko akawa mgombea Urais wa JMT kwa tiketi ya Chama chetu CCM

Hakika Uzalendo wako ni Urithi Wetu

Mungu ni mwema Wakati Wote!
 
Nadhani hujaelewa
Nilichoelewa ni kwamba umesema katiba imevunjwa na rais. Sasa nimekuwekea kifungu kilichotajwa na bwana Petro E. Mselewa cha kwenye katiba kukuonyesha kuwa rais hajavunja katiba, bali ametumia madaraka yake kwa mujibu wa katiba ya JMT. Kama maelezo hayo bado yanakuambia sijaelewa, naomba unieleweshe ulimaanisha nini.
 
Nianze kwa kusema Ulale Pema Peponi Shujaa Magufuli

Sitashangaa kijana wako Dr Dotto Biteko akawa mgombea Urais wa JMT kwa tiketi ya Chama chetu CCM

Hakika Uzalendo wako ni Urithi Wetu

Mungu ni mwema Wakati Wote!

Nani atakubali kuongoza na mrundi?
 
Ni msaidizi bamba moja wa Waziri Mkuu.

Majaliwa anasaidiwa kikazi. Inaonesha afya yake si nzuri.
Una anzaje kuzungumzia afya ya mtu mwingine wewe ni msemaji wa familia ya waziri mkuu au dactari wake...

Tufafanulie...

Asylum alycum
 
Nawasalimu Waungwana wa JF,

Mwanzo mwanzoni nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa uhai na afya anazotujalia hata kuendelea kupashana habari za hapa na pale kupitia mtandao wetu huu pendwa wa JamiiForums.

Hivi punde, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko kwenye Baraza la Mawaziri kwa kuteua Mawaziri wapya; kuwahamisha wengine; kuteua Manaibu Mawaziri na kuwahamisha wengine na kuwateua Makatibu Wakuu, Manaibu Makatibu Wakuu na kuwahamisha wengine.

Kingine na kikubwa zaidi ni uteuzi alioufanya Mhe. Rais Samia kumteua Dkt. Doto Biteko kuwa Naibu waziri Mkuu na Waziri wa Nishati. Hili ni kubwa kwakuwa limeanzisha mjadala kwa wadau, wakiwemo watumiaji wa JF, kudai kuwa uteuzi huo (wa Naibu Waziri Mkuu) umekiuka Katiba.

Kikatiba, Mhe. Rais yuko sahihi. Ibara ya 36, Ibara Ndogo ya 1 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inampa Rais, pamoja na mambo mengine, kuanzisha na kufuta nafasi za madaraka ya namna mbalimbali katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Inasomeka:

36.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katika Katiba hii na ya sheria nyingine yoyote, Rais atakuwa na mamlaka ya kuanzisha na kufuta nafasi za madaraka ya namna mbalimbali katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

(2) Rais atakuwa na madaraka ya kuteua watu wa kushika nafasi za madaraka ya viongozi wanaowajibika kuweka sera za idara na taasisi za Serikali, na watendaji wakuu wanaowajibika kusimamia utekelezaji wa sera za idara na taasisi hizo katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, nafasi ambazo zimetajwa katika Katiba hii au katika sheria mbalimbali zilizotungwa na Bunge kwamba zitajazwa kwa uteuziunaofanywa na Rais.

(3) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (2), masharti mengineyo yaliyomo katika Katiba hii na ya sheria yoyoteinayohusika, mamlaka ya kuwateua watu wengine wotewasiokuwa viongozi wala watendaji wakuu, kushika nafasi za madaraka katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, na pia mamalaka ya kuwapandisha vyeo watu hao, kuwaondoa katika madaraka, kuwafukuza kazi na mamlaka ya kudhibitinidhamu ya watu waliokabidhiwa madaraka, yatakuwa mikononi mwa Tume za Utumishi na mamlaka mengineyo yaliyotajwa na kupewa madaraka kuhusu nafasi za madaraka kwa mujibu wa Katiba hii au kwa mujibu wa sheria yoyote inayohusika.

(4) Masharti ya ibara ndogo ya (2) na ya (3) hayatahesabiwa kuwa yanamzuia Rais kuchukua hatua za kudhibiti nidhamu ya watumishi na utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Ni wazi kuwa kabla ya leo ( achilia mbali wakati wa uongozi wa Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi), hakukuwa na nafasi ya Naibu Waziri Mkuu. Leo, akitumia mamalka yake kikatiba, Mhe. Rais ameanzisha nafasi hiyo ya Naibu Waziri Mkuu. Ili nafasi hiyo ifanye kazi, akamteua Dkt. Biteko kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati.

Kwa mamlaka hayo hayo, leo hii hii, Mhe. Rais amefuta iliyokuwa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na kuanzisha Wizara mbili: Wizara ya Ujenzi na Wizara ya Uchukuzi. Na uteuzi wa Mawaziri; Manaibu Mawaziri na Makatibu Wakuu ukafanyika. Yote haya yamefanyika kikatiba.

Kimsingi, Katiba yetu ya sasa inaruhusu kuanzishwa na/au kufutwa kwa nafasi yoyote ile ya kimadaraka. Wengi wetu tunajua, kwa kutumia Katiba hii hii, Rais Mstaafu Mwinyi aliwahi kumteua Hayati Augustine Lyatonga Mrema kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Ilitumika Katiba hii hii na Ibara hii hii iliyorekebishwa mwaka 1984 na mwaka 2000.

Pengine huelewi “bila kuathiri” ina maana gani
 
Watanzania hawajaridhika na Mkataba. Hii teua tengua sio Suluhisho.....

"serikali Ina namna mbili tu..
1. Kiheshimu hofu na maoni ya wananchi kwamba hawajaridhika na suala hili, au
2. Kuwapuuza wananchi na kuendeleza na suala hili.

Lakini wapime madhara ya kila uamuzi watakaoifanya"

Mapinduzi yapo mlangoni mwako.
Nani wa kufanya mapinduzi Tanzania?
Tisi wengi wao ni uvccm
 
Mwalimu mwingine kaongezewa kuongeza nguvu
Ni hivyo tu yaan
 
Jamani hili Taifa letu tunaendaje? Vyeo vinakuwa vingi Sana. Ina maana ofisi ya Waziri Mkuu imekuwa kubwa sana mpaka utendaji unakuwa Mdogo na kuamua kuiongeza nguvu kumpa msaidizi vipi? Vipi wizara zilizo chini yake?

Ningependa kujua majukumu ya Naibu Waziri Mkuu yatakuwa yapi kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri na Muungano wa Tanzania.

---
Lyatonga hakuandaliwa kuwa Raisi, aliwekwa hapo kisiasa, yaani kupooza nchi maana yeye ndio alikuwa anaaaminika.
 
Nani wa kufanya mapinduzi Tanzania?
Tisi wengi wao ni uvccm
Haya unayoyaona na kusikia ndio Mapinduzi yenyewe. Kuanzia sakata la DPW na maijadala inayoendelea|Kesi za Wazalendo Mahakamani|Jeshi kudai mitumba | na hii shuffle ya Cabinet....itoshe, yanayojiri huko Sudan-Mali-Burkina Faso-Gabon-Niger..
Kumbuka hata huko hakuna aliyetegemea mianguko hiyo?
 
Haya unayoyaona na kusikia ndio Mapinduzi yenyewe. Kuanzia sakata la DPW na maijadala inayoendelea|Kesi za Wazalendo Mahakamani|Jeshi kudai mitumba | na hii shuffle ya Cabinet....itoshe, yanayojiri huko Sudan-Mali-Burkina Faso-Gabon-Niger..
Kumbuka hata huko hakuna aliyetegemea mianguko hiyo?
Maybe, yawe tu yenye maslahi na taifa yasiwe yenye maslahi na kikundi cha wachache
 
Naona Hiyo Wizara ya Madini inatakiwa iwe chini ya Uangalizi wa Karibu wa Waziri Mkuu maana kulikuwa kuna Mambo mengi saaana
Ni Naibu Waziri Mkuu na pia Waziri wa Nishati. Huko Madini kahamishwa...
 
Back
Top Bottom