Naibu Waziri mteule wa Madini, Francis Kumba Ndulane ashindwa kusoma kiapo kwa ufasaha, uteuzi wake watenguliwa

Jamaa baada ya uteuzi alifanya bonge la sherehe.... Nimemuonea huruma daah!
 
Nakwambia hivi, kama mwenye IQ kubwa bado yupo mtaani na mwenye IQ ndogo katoka, nani mwenye IQ kubwa hapo?

Kwanini ukubali kuongozwa na uliyemzidi uishie kulalamika tu badala ya kuchukua hatua na kubadilisha mustakabli wako?
Kwa iq yako ndogo na ujinga uliojaa kichwani kwako unajua kutoka kimaisha ni kuwa na iq kubwa. Unaweza kuta mtu mwenye akili na iq kubwa hana smart phone we mjinga unayo. Naomba itungwe sheria wajing kama wewe wasimiliki smart phone.
 
CCM
CCM imejaa majizi, atakuwa aliiba vyeti
 
Walisoma kwa kiingereza?
Kama kusoma kwa kiingereza ndio lazima uweze kuongea kiingereza vizuri basi wabongo wengi wangekuwa wanapiga ung'eng'e huko mitaani maana wamesoma kwa kiingereza na wamefanya vizuri kwenye masomo yao.
 
Ndo dalili za UTAWALA uliofeli..
Haijawahi kutokea hii.
Ukiwa Stressed huwa wanajinyea au kujikojolea achilia mbali kushindwa kusoma mbele ya watu. Hii kisaikolojia inatokea pale mtu anapokuwa na hofu au kuwa overwhelmed juu ya jambo ambalo amelisubiria kwa muda. Wengine siku ya kwanza kukutana na mpenzi wake aliyemtolea nje kwa muda mrefu basi huwa wanashindwa kunaniliu. Asamehewe apige kazi
 
Wabongo nuksi! Wamemvizia siku ya kuanza kazi rasmi kwa kuapishwa ndio wampige kipaipai. Kwanza huyu jamaa ni msomi, na Mungu atamlipia.
 
Ila hatuwezi kujua alichokuwa anapitia huyo waziri unawezakuta alikuwa haoni maandishi au anaona vitu vyengine kabisa,yote yanawezekana uchawi upo.
 
Well, FA yupo vizuri na ana matumizi mazuri sana ya lugha labda ashindwe kwenye utendaji.

Huyo Tale kusoma shida, kujenga hoja ndo kabisa.
FA kwenye kampeni alikuwa anabwabwaja tu labda ata improve kwasababu ya usanii utambeba ila Tale tale ni Mweupe yaani hana anachokijua zaidi ya kuwaibia wasaniii na fitina kwenye sanaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…