Naibu Waziri mteule wa Madini, Francis Kumba Ndulane ashindwa kusoma kiapo kwa ufasaha, uteuzi wake watenguliwa

Wewe mbona umeandika haibu badala ya aibu
 
Hamnaga rehearsal ya kuapishwa? Fimbo mashuleni zinafanya tuwe watu wazima tusiojiamini. Muda wote unakuwa muogamuoga tu.
Asante sana. Hii athari ya fimbo hata ukiimba namna gani watanzania hawatakuelewa hata kidogo. Fimbo zinaathiri sana watu ukubwani ni vile watu hawajui tu. Siyo kutojiamini tu ila kuna athari nyingine nyingi tu.
 
Huyo atakuwa alipatwa na WENGE au Alipagawa au Aliashikwa na KITETE kikamuondolea confidence!! Swala la kutoona ni uongo mtupu! Maana maneno ni yale yale hata usiposoma utayakariri "MImi Francis NGUMALU naapa kwamba nitakuwa mtiifu kwa jamhuri ya muungano wa tanzania na sitotoa siri za baraza la mawaziri ehee mwwnyezi mungu nisaidie" hapo inahitaji kusoma kweli???
 
Aliwezaje kuomba kura jimboni kwake yule
Watanzania elimu yetu ni mbovu sana. Mtanzania ujanja wake uko kwenye kupiga gumzo mitaani na kubishana mambo ya low level. Mtu kama Kibajaji akisimama jukwaani huko vijijini anaweza kubwatuka maneno mengi tu ila kuongea kwenye watu wanaojielewa hawezi.
 
Tusiwe wakali sana kwa watoto tusiwatishe bali tuwaelekeze nao watajiamini
Sasa ndo mtu ameshakuwamkubwa kama waziri hivyo na hajiamini..atajifunzaje kujiamini?
 
Alishinda uchaguzi au Ni wale waliobebwa kuanzia kwa wajumbe Hadi ballot.
 
Kafutwa Kazi Tayari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…