Naishi na Mwanamke Nisiemfahamu, Nahitaji Namna Nzuri ya Kumuacha

Naishi na Mwanamke Nisiemfahamu, Nahitaji Namna Nzuri ya Kumuacha

Nikwambie bro wala usimfukuze huyo mke umeletewa na Mungu kwa njia ya ajabu.! Wewe cha kufanya muulize kwao muishi kwa amani, halafu acha kumix datting app na social media. Nna uhakika huyo mdada mmekutana Fb 🤣🤣🤣

Halafu na wewe umempenda ndiomana ukampiga na shopping ya viwalo. Ww ni mtu mwema sana na mpole.!! Pls usimfukuze mama wa watoto wako.
 
Dadekii mtakuja paramia majini kelebuu..

Mwambie umepata safari ya kikazi hivyo kesho unasafiri na utafunga nyumba yako hadi mwezi ujao.
Bon voyage..!
Atamsubiri kwani anakaa huko huko mpk kifo chake?? 🤣
 
Mpaka nguo umenunua kupika anakupikia na hana makuu mpole mstaarabu Sasa ubasubiri Nini?

Kipengele kitakachokusumbua maisha Yako n Dating app
Huyo wake aoe, amuache akutane na vivuruge km hajamkumbuka
 
Uhuru huoatikana kwa njia mbili
1. Active approach
2. Passive approach
Chagua kati ya hizo ila nakushaur chagua active approach hainaga mawaaa
 
Ila walimwengu mna ujasiri hasa. Sasa mtu humjui undani wake unamuweka ndani kwako. Ghafla akikata moto utapeleka wapi maiti. Ukute hata jina lake halisi hulijui.
Watu wanatembea na magonjwa yao, mara ukute ni kichaa usiku mmoja anaanza kukucharaza mboko ndani humo.

Siku zote mwanamke unaekutana nae juu kwa juu hata siku moja usimpeleke nyumbani kwako. Mbona lodge zipo nyingi.

Hii kauli narudia kila siku, mtaani kugumu. Watu wapo tayari kukaa hata na zimwi ilimradi tu awe na hifadhi ya uhakika.

Sasa ukute hizo nguo ulizomkuta nazo ndio pekee anazomiliki, halafu ghafla unampeleka shopping, ndugu yangu hata wewe ungekuwa huyo demu ungetaka kuondoka tena?

Huyo ni mkeo tayari, mwambie akuonyeshe kwao tu maisha yaendelee.
Akili za watu wa sku hizi zinatia mashaka
 
Nasubiri jibu na mie, [emoji23][emoji23][emoji23]
Kuna mdau kanijibu kuwa ni special Apps,tena kaitaja Badoo.

Hii App nimeisikia sana,tena pia nimesikia na mengine zaidi,kuwa ni app ambayo watu wengi wanaojiuza huutumia.

Sasa kwa context hiyo Sina uhakika kama ni sahihi kumpata mwenza wa maisha huko. Tena mkikaa pamoja na kuanza kufikiria mlipokutana kuwa ni huko,Kila mmoja anaweza kumhisi mwenzie vibaya kuuwa anarudi rudi huko kutafuta mwenza mpya.
 
Back
Top Bottom