Mimi ni CHADEMA lakini kwa suala hili chama kinazingua sana, kuna haja gani ya kuhangaika na mtu aliyetangulia kwa Mungu?
Huoni haja Kwa sababu wewe ni mjinga usiyejua hata maana ya "historia"
This is not about
John P. Magufuli as a person.
John P Magufuli anajadiliwa na ataendelea kujadiliwa si Kwa sababu nyingine yoyote bali kama mtu aliyewahi kuwa Rais wa nchi hii kwa kuangazia alama (
footprints) za uongozi wake alizoacha kwa kuangazia pande zote yaani ule wa
UBAYA au
UZURI wake..
Na hivi historia itaachaje kumrekodi na kumulika kwa kurunzi kali mtu kama huyu aliyewahi kuwa kiongozi mkuu wa nchi ( Rais) kwa kuangazia alama (footprints) za uongozi wake alizoacha?
Afikiriye kuwa hili linaawezekana, basi huyo ni mpumbavu na mjinga asiyeelewa na anayestahili kupuuzwa kabisa...!
Tatizo kubwa la mtu wenu huyu yaani
hayati John P. Magufuli ni kuwa, ameacha alama ya ubaya mwingi kiasi cha kufunika mazuri kidogo aliyofanya...
Sasa nyie watetezi wa
legacy yake kila mkijitutumua kutetea mazuri yake, mnajikuta
graph imelalia upande wa wale wanaomwandika kwa ubaya...
Na mkiona hivi ndo hapo mnapoamua kuweka mpira kwapani na kuanza kuropoka hovyo kama hivi unavyofanya wewe.!!
Kwa hiyo,
HAIWEZEKANI John P Magufuli kuacha kusemwa iwe ni kwa njia ya maandishi, majukwaa ya kisiasa au mijadala mbalimbali ya midomo...
Wewe kama una zuri la kusema juu yake, liseme na wala hakuna wa kufanya lolote. Vivyo hivyo wanaosema mabaya yake, acha waseme na kama unapinga, yapinge
kwa ku - replace na mazuri uone kama utaweza..!!