Nani anaweza kuwa CDF mpya wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama?

Luteni, Meja, Brigedia (Jenerali).

Hivi anaweza kuteuliwa mtu ambaye sio rank ya Luteni Jenerali direct akawapita walio juu yake?

Mara kibao imefanyika hivyo!
Wkt anatayarishwa kuwa CDF General Mwamunyange alikuwa Brigediar General akapandishwa vyeo mara mbili haraka haraka!
General Robert Mboma alikuwa Meja Jeneral kabla hajawa CDF kwa kuvishwa kwanza cheo cha Luten General kisha General kamili

Nipo tayari kusahihishwa
 
Nadhani Maj. Gen Paul Simuli ni potential kwa high post. Ni mtulivu mpole but bold. Kwa sasa nadhani ana head utumishi ndani ya Jeshi!! Tusubiri mama achamvue mafaili
 
Ndio, anarukishwa kama ilivyofanyika kwa Mbuge kutoka Kanali hadi meja general.
Mbuge Hakuruka cheo kutoka Kanali kuwa Meja Jenerali bali alipandishwa kuwa Brigedia Jenerali kwa kipindi kama mwaka na nusu kabla hajapandishwa tena kuwa Meja Jenerali
 
CDF mpya ni Mkingule !! Period!!
 
Mbuge Hakuruka cheo kutoka Kanali kuwa Meja Jenerali bali alipandishwa kuwa Brigedia Jenerali kwa kipindi kama mwaka na nusu kabla hajapandishwa tena kuwa Meja Jenerali
Mbuge shule hana yule, amejaa fitina tu kuwafitini maboss wake. Huyo kichwani ni bure kabisa hamna kitu vyeo alipandishwa kiva hayo tu, amshukuru sana Paul Makonda aliekuwa anampigia chapuo kwa mwendazake
 
Mbuge shule hana yule, amejaa fitina tu kuwafitini maboss wake. Huyo kichwani ni bure kabisa hamna kitu vyeo alipandishwa kiva hayo tu, amshukuru sana Paul Makonda aliekuwa anampigia chapuo kwa mwendazake
Mimi sijui elimu yake, ila najua kuwa Mbuge alisimamia miradi mbalimbali ya Ujenzi iliyokuwa inafanywa na JKT kwa ufanisi mkubwa sana; ndiyo maana JPM akampandisha cheo na baadaye kumfanya kuwa mkuu wa JKT. Makonda anahusiakje kweli hakuna anayejua, ila rekodi yake inajulikana kuanzia ukuta wa Mererani hadi Ikulu ya Dodoma na kwingineko
 
lieutenant general Meela, huyu alikuwa DARFUR na sasa ni balozi
 
Kuanza kubeti nani anakuwa cdf haiongezi wala haipunguzi mkate wangu wacha niwahi kibarua.
 
..hata mimi naona ni vigumu kumruka CoS wa sasa hivi Lt.Gen.Mkingule.

..vinginevyo itabidi wateuliwe Cdf na Cos wapya.

..iliwahi kufanyika wakati wa Kiaro[cdf] na Kiwelu[cos], na Mboma[cdf] na Sayore[cos].
hizi zote zilikuwa jitihada za kuhakikisha kiwelu hawi cdf, lakini aliacha historia, four star general ambaye hajawahi kuwa cdf
 
Yule luteni Urio aliyeupiga mwingi kwenye ile kesi ya mchongo ya Mbowe na makomandoo angependeza zaidi...
 
Jeshini kuwa cdf siyo kujenga madaraja tu bali ni elimu nzuri, weledi na ujuzi na uzoefu mkubwa wa uongozi wa kijeshi,uzalendo, uaminifu na sifa nyinginezo zilizotukuka seniority na taswira yake jeshini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…