Mada yako ikomee hapa hapa.Shutuma ni kali sana mitandaoni dhidi ya Gekul, na hata rais ametengua uteuzi wa Gekul kwenye nafasi ya unaibu waziri.
Kama unaweza kuamini hadi huyo Rais achukue hatua alizochukua..., hii nchi bado tutaluwa tunaamini kwamba ni taifa miongoni mwa mataifa yenye heshima?
Hayo mengine yote uliyo orodhesha hapo ndio kwanza leo nayasikia; lakini pia niliwahi kusikia hadithi za akina Tundu Lissu wakimiminiwa risasi na wenzao, kati yao akiwa Mwenyekiti wake wa chama, ambaye baadae ndiye kawa mstari wa mbele kuokoa maisha yake.
Tumesikia hadithi nyingi za akina Abdul Nondo wakijipoteza na vimada wao. Akina Chongolo, na wengi wengineo.
Huyo Gekul, ni kweli alikamatwa akitaka kutorokea nchi ya jirani, kwa nini atoroke?