Naomba kujuzwa mahali pazuri pa kufikia Zanzibar

Naomba kujuzwa mahali pazuri pa kufikia Zanzibar

Zanzibar kuna hotel inaitwa Baraste lodge kagorofa flani hivi, madem zangu wawili nilifika nao hapo kwa nyakati tofauti pale ni pazuri sana sema kwa siku ni 65,000 kuendelea , chumba kikubwa full ac , friji, viatanda viwili ukienda hatanna watoto fresh, choo bafu humo humo , asubuhi unapata breakfast safi

Sema kwa kipindi hichi ukilia nao 60 hadi 65 unapata chumba cha gorofani safii tu full ac
Uliwezaje kuingia wakati wana kibango kinasema ukiingia na jinsia tofauti lazima uoneshe cheti cha ndoa
 
Kama fedha ipo nenda Paje mpaka Jambiani kuna Zanzibar ya tofauti kama huko Miami wazungu kibao na bei ni ndefu. Nilikuwa huko muda si mrefu
Screenshot_20220130-194618_Instagram.jpg
Screenshot_20220131-083202_Instagram.jpg
 
Bro mbona zenji kawaida sana nilikuwa hapo vacation yamgu mwaka huu...zanzibar beach resort ila nilirakiwa niwe shamba pazur zaid sasa fanya hv ingia google map search gharama za hotel tena kipnd hiki ni cheap sana
 
Sijawahi kuzielewa zile Hoteli za Stone Town ya yale mabei. Wazungu sio wazima kabisa
Hata mi nashangaaga basi wanatuchaji bei kubwa si waboreshe na mazingira, utakuta tutanda twa hostel kagodoro kameishaa tv ipo lakini mbovu, friji ipo lakini pia mbovu ac ikiwashwa inunguruma kama garibovu afu unaambiwa ulipe sh 120,000 per night. Siriaz!
 
Zanzibar hakuna guest house za buku 5 au buku 8 kama bara ?


Inamaana kule wana hawapigi game [emoji3]
 
Ndio madhara ya kukataa watanganyika kuwekeza huko..kisa sio wazenjo..ona sasa hata lodge hakuna..maisha gani haya.

#MaendeleoHayanaChama
Unalosema sio kweli, mbona kuna watu wa huku wana hoteli huko
Sema znz inaonekana nyumba za wageni zinajengwa kulenga watalii wa nje kuliko kulenga wateja wa humuhumu ndani nchini
 
Wadau wa Zanzibar,

Naomba reference ya Guest House au Hoteli nzuri ya kufikia hapo Zanzibar. Ninakaa siku 1 tu ila naongozana na msafara wa watu 5.

Nitashukuru kwa msaada wa jina, sehemu, ikiwezekana namba ya simu ya mhusika.
 
za 40/30 zipo ila inabidi uwe mwenyeji sana au waombe boda wakupeleke kiembe samaki ipo moja, au mtaa wa kariakoo wanapouza vifaa vya umeme used. sehemu nyingi average ni 60-80 hata hiyo ya 50 utaangahika sana za kubahatisha
 
Back
Top Bottom