Naomba kujuzwa mahali pazuri pa kufikia Zanzibar

Naomba kujuzwa mahali pazuri pa kufikia Zanzibar

Wakuu nifikie wapi au nikakeshe forodhani
Kuwa makini huko hakunaga gesti za bei chee kama hizo ulizozizoea hapo ubungo za buku teni teni
Kule Zenji ukienda uwe na hela ya kulala hotels na bei zinaanzia elfu 60 na kuendelea, hizo za elfu 40 sidhani labda huko pembeni sana halafu upate wenyeji ila pia uwe makini kama umetoka bara ukifika kuna wale waarabu weusi(wapemba) wale jamaa wengi wao hujifanya wakarimu sana kwa wageni kiasi kwamba unaweza kujikuta mpaka sehemu ya kulala ushalipiwa na mpaka shida zako zote za huko nyuma zitatatuliwa[emoji23][emoji23][emoji23]pwani kuna mamende kuwa makini sana.
 
za 40/30 zipo ila inabidi uwe mwenyeji sana au waombe boda wakupeleke kiembe samaki ipo moja, au mtaa wa kariakoo wanapouza vifaa vya umeme used. sehemu nyingi average ni 60-80 hata hiyo ya 50 utaangahika sana za kubahatisha
Yaan ndio kusema vyumba hakuna au kukomoana mbon bongo huku 30/35 unalala chumba kikali, hio 40/50/60/70/80 ni bed & breakfast au ?
 
Wakuu nifikie wapi au nikakeshe forodhani
Kuna sehem inaitwa kwa mama Janet ni maarufu sana kwa kitimoto...Wana room Safi za "kawaida" ni 25000 ila kulala ni kuanzia saa tatu...
Na kwa mama frank (soko la bar) kuna sehem room ni Safi sana bei ni 25000,nimesahau jina ila napo ni Kati ya 25000/30000,hapa napapenda ni pasafi.
 
za 40/30 zipo ila inabidi uwe mwenyeji sana au waombe boda wakupeleke kiembe samaki ipo moja, au mtaa wa kariakoo wanapouza vifaa vya umeme used. sehemu nyingi average ni 60-80 hata hiyo ya 50 utaangahika sana za kubahatisha
Sasa naelewa Kwann nimeangushiwa hii safari,walijua sitabaki na chochote...
 
Nakumbuka mara ya mwisho nilienda huko miaka ya hivi karibuni kupeleka biashara yangu ya majeneza mambo yakawa magumu kule wengi ni waislamu hawaziki kwa majeneza niliishi kwa taabu sana mpaka nikaamua kusafirisha mzigo uliobaki nikarudi nao kwenye branch yangu ya Dar
Kwa siku nilizokaa huko nisingekuwa jeuri lingenikuta jambo[emoji848]
 
ndo tunaishi hivyo labda kam ana mabegi mengi ila kam yupo kisport tu mbona anaishi
 
Yaan ndio kusema vyumba hakuna au kukomoana mbon bongo huku 30/35 unalala chumba kikali, hio 40/50/60/70/80 ni bed & breakfast au ?
Mkuu breakfast kuanzia 70, zingine zote unpagishwa mswaki. Ilivyokuapo merryland pale malindi ndo ilikua around 40 na unapiga na breakfast fresh, ila yule owner nadhani alipata some issue akaifunga. Zenji is very expensive kule wavuvu kibao ila bei ya samaki moto
 
Back
Top Bottom