Naomba kujuzwa mahali pazuri pa kufikia Zanzibar

Shida kuna wengi hawajui lolote kuhusu unguja, wanaropoka tu,gest Safi usinielewe tofauti zinaanzia 30k...Kuna moja inaitwa sayi pia sio mbaya iko fuoni mwisho..ni maarufu tu..iko pemben kidogo ya mji...ukishuka bandarini panda boda ni buku mbili, mwambie unaenda tobo la pili, ukishuka ulizia daladala za fuoni.

Ama angalia kwenye kioo cha mbele zimeandikwa "Fuoni" mwambie konda unaenda "sayi" akifika akushushe...nauli ya daladala ni jero tu.
 
Shukrani sana Kiongozi angalau naanza kupata matumaini
 
Ipo moja tobo la pili sokoni, inaitwa mtendeni Lodge
Hii ya kingese mno,unapanga gesti na wenyeji wanaishi humo humo.

Halafu haiko tobo la pili,iko mtendeni panapouzwa bidhaa za used mwishoni kule...
 
Pole sana ila nimecheka sana navuta picha ulivokuwa unahangaika na majeneza
Acha tu ndugu yangu haya mambo ya utafutaji utakutana na changamoto nyingi ila yapaswa uvumilivu tu.
Tena mbaya zaidi hapo nlikuwa nimechukua mkopo wa 7m bank ilikuwa kipindi kile Corona ndo imechanganya wakawa wanasema watu watakufa sana mwanaume nikajua nikiwekeza pesa nyingi lazima nipige hela mwanaume nikavuta mkopo nikaandaa mzigo mkubwa nikaweka kwenye office yangu hapa Dom then mzigo mwingine nikaugawanya Dar na Zenji nikitaraji kupiga hela msimu wa Corona ila kilichonikuta mpaka leo sintosahau!
 
Biashara ikawa ngumu sio😂😂😂 dah wauza majeneza banaa!
 
Mkuu, Ukifika Zanzibar usilale Stone Town. Panda zile Chai Maharage zao, kisha uende kama Dk 20-30 hivi panaitwa Bububu. Nikilala kwa Elfu 25 hafu kuna vyumba hadi vya 15.

 
Kweli hiyo ni nchi. Nilikuwa na mpango wa kwenda mwezi ujao itabidi nifikirie sehemu nyingine.
 
Kuna mzee mmoja bonge sana!!una mkuta yupo nje muda wote
DAh hiyo mtendeni nimeenda leo asubuhi ni kuchafu sana nimekuta Kuna mzee amekaa mnene mlemavu yupo ananyolewa nywele kwa ndani nikavua viatu ndani Kuna wafaa wenyeji maana Ile ni familia 30,000k ni maajabu nipo zangu Fuoni lodge nimelipa 500 kwa dara dara nipazuli 30,000 at least ahsante kwa mchangiaji na mleta mada pia imenisaidia kwa kiasi kikubwa 🙏
 
Ila we jamaa, nimecheka sana yaani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…