Naomba kuongea na wadogo zangu wa kike wenye kutafuta ndoa

Ndoa ni stara kwa mwanamke! Hivyo mwanamke anahitaji ndoa kuliko mwanaume

Wanawake wamekuwa wengi ama ni wengi kuliko wanaume... Hivyo ndoa imekuwa kitu adimu hasa ukizingatia kuwa.. Pamoja na uchache huo wa wanaume bado karibia nusu yao si waoaji

Sasa kutokana na hamaniko hilo la kuhitaji ndoa wengi wamejikuta wakiangukia kwenye mikono ya wanaume wasio sahihi
Kuna kauli moja mabinti wenye kutaka ndoa wanaitumia bila kujua madhara yake! Hii kauli ya kusema "hata nikimpata anayepumua tu inatosha!"

Wadogo zangu wa kike hakuna kauli ya kiwaki kama hii... Unaingia kwenye ndoa na sio kwenye mapenzi.. Kauli huumba na Mungu humpa kitu alichokiomba!

Hivi mnajua kwa hakika mwanaume anayepumua tu yukoje!? Si mlemavu wa viungo ama akili.. Bali ni mlemavu wa ufahamu na kujitambua yeye ni nani na anapaswa kufanya nini kwa wakati gani
Unaingia kwenye ndoa ambayo ni mahusiano ya kudumu mpaka talaka itakapowatenganisha! Kifo ni mustakabali

Unapaswa kuwa na mtu anayejitambua, anayejali, anayeweza kubeba majukumu ya baba.. Na anayeweza kuzikabili changamoto kwa weledi kwa hekima na kwa utulivu

Mwanaume anayepumua tu ni yule ambaye utamuacha kitandani uende kazini ukiwa umeshamuandalia mpaka chai, Ataamka kwa kuchelewa, hawezi kutandika hata kitanda. Atakunywa chai na kuacha kila kitu hapo.. Hatafanya chochote mpaka urudi ufanye vyote na bado usiku umpe!

Wengine anaweza kuwa na kazi lakini huoni tofauti yoyote na asiye na kazi majukumu yote unayabeba wewe. Mwanzoni mwa ndoa utaona kama utaweza.. Lakini taratibu mkishazoeana utaanza kuliona tatizo! Na tatizo litazidi kujipambanua kadiri familia itakavyoongezeka. Watoto, Wafanyakazi, Biashara, Ufugaji nk

Utajikuta usipofanya wewe yeye hagusi kitu.. Matumizi ya nyumbani
Mahitaji ya watoto shuleni na nyumbani. Mishahara ya wafanyakazi. Manunuzi ya vitu kama mna biashara. Kuhudumia mifugo kama mnafuga nk

Ikitokea umepata safari ya siku chache tu ndio utaliona tatizo kubwa katika uhalisia wake..utakuta kila kitu kimeparaganyika Hesabu kwenye biashara, Manunuzi hakuna, Loss kama zote. Kama ni mifugo si ajabu kukuta mingine imekufa kwa kukosa huduma na mingine kupotea kwa kukosa ufuatiliaji.

Anaweza kufanya kikubwa ni matumizi ya pesa zako.. Ana we za Ku control mpaka account zako. Anachoweza kingine ni kukuzalisha kila mwaka bila kujali future ya hao watoto. Mwisho wa siku unajikuta unajutia majuto yasiyo na faida.. Unajikuta binti mdogo unazeeka kabla ya umri na kuandamwa na magonjwa yatokanayo na msongo wa mawazo

Nina mengi ya kuandika.. Lakini ya msingi ni haya! Kama ukiisoma hii mada na kuielewa naamini utabadili mtazamo wako kuhusu mwanaume wa kukuoa

Chelewa kuolewa lakini olewa na mtu sahihi.. Si wali nazi wala si mwanaume suruali wala si yule anayepumua tuu
Perfect
 
Tunashukuru Kaka Mshana kwa uzi mzuri sana wenye mafunzo.
 
Ina maana katika mada nzima ndo umeona hili TU? King Kong III umemuona kijana wako alivyo mchokozi?

Inasikitisha sana ,LGBTQ ni laana ,tuipinge kwa nguvu zote ,kwasisi wazazi ni kuomba Mungu asitokee mtoto kufuata mambo ya UPINDE ni aibu kwa FAMILIA nzima.

Kijana wako kwenye content yote ya Mshana Jr ,wali nazi ndiyo imemvutia 😀😀😀
 
cocastic unasemaje kuhusiana na alilolisema kakako@King Kong III eti ni kweli kuwa hiyo ni laana?na ipigwe vita?
 
Unatumia takwimu zipi mkuu kusema wanawake niwengi kuliko wanaume
 
Nimesoma uzi na comments zake zote so far, midume haijaja kupokea ushauri bali imeunga mkono na kuongezea nyama kwenye bandiko la kaka yao, kwahiyo ni kazi kwa washauriwa kuchukua au kupuuza ushauri.

Hata kama wasipozungumza hapa ila tunaamini ujumbe wanaupata, hata kama wanauchungulia uzi huu kwa jicho moja.

Midume oyeee!
Umejielezea sana bhana,
Mkubali tu wanaume mnapenda sana kujua mambo ya kike yaani mpo so obsessed na wanawake
 
cocastic unasemaje kuhusiana na alilolisema kakako@King Kong III eti ni kweli kuwa hiyo ni laana?na ipigwe vita?
Anaweza kuwa sahihi kadri ya mwazo au fikra zake.
Ila ajaribu kufikiri uwanda mpana zaidi, ili kuondoa sintofahamu kwa baadhi ya watu/kundi, ambao hawako ndani ya box alizungumzialo yeye.

Mpe salamu!!
 
Mjukuu labda tu kama huelewi dhima na dhana ya mtu kuitwa mwanaume, mme au baba!
Mungu aliumba mtu mke na mtu mume! Kwenye ndoa na mahusiano anayeingiliwa ni mwanamke na si kinyume chake
Baba shoga hata kama anatimiza majukumu yake kifamilia bado hiyo ni laana na tatizo kubwa...
Natambua wapo wanaoishi hayo maisha kwa siri kubwa lakini si jambo lenye afya kifamilia
Baba shoga unadhani atawakuza wanae katika maadili gani?
Hapo umekosea sana kwanini hua mnadhani Shoga hana maadili lakini mwanaume anayebadili wanawake kila kukicha ana maadili au mwanaume mlevi ana maadili au mwanaume anayekula tigo za wanawake ana maadili au mwanaume jambazi ana maadili au fisadi mla rushwa ana maadili?

Usimjudge shoga kwa uelekeo wake wa kingono wapo mashoga wana hofu ya Mungu vile vile na wengine wachungaji kama ambavyo wapo walevi na wazinzi wenye hofu ya Mungu na wachungaji vile vile
 
Jibu watakalolitoa halina tofauti na nililokupa.

Mume na mwanaume Bora hawezi kuwa na sifa ya ushoga.

Ila sio lazima Kila mtu awe Bora. Hayo mengine nakuachia
😂😂😂😂
Mtibeli, swali limekuzidi uwezo na upeo wako wa kufikiri/kuchanganua mambo.
Poleeeee. 😂😂😂😂
 
Mjukuu kwani hapa ni mjadala wa ndoa za binadamu au wanyama?
Sasa wee mbona unaleta hizo hoja za wanyama, km ulijua tunazungumzia binadamu pekee?

Hivi unajua hata unacho eleza lakini? 😂😂😂😂😂
 
Tafsiri sahihi ya baba ni ile masculinity ,father hood and responsibilities.

-Uanaume
-Ubaba
-Majukumu

Ikiwa shoga anaweza akawa na Masculinity , Fatherhood , and responsibilities anaweza akawa ame -qualify

Ila katika kila sehemu mahitaji ,na tamaduni zipo tofauti .

Mfano mwanamke wa kiswahili ambaye Ana -chase ndoa ili awe secured nikimaanisha apate uhakika wa kula , kulala n.k anaweza sio tu kuolewa na shoga Ila anaweza kuolewa na lesbians .

Ila the real woman ambaye anatambua kuwa marriage is Covenant , she can't married na Gay kwakuwa the real woman hatafuti Sex , and life assurance Ila anatafuta Mambo Kama hayo kuwa na Mwanaume ambaye Ana sifa ya uanaume .
Nilidhani watu huoana kwa mapenzi kumbe huoana ili wapate kusifiwa na jamii zao kua ameolewa na shababi au kaoa kamdada,

Nadhani hiki ndio alichokisema braza Mshana kuwatahadharisha wadada wataka ndoa wasitafute anayepumua au anayejua kusimamia kucha au anayetoa sauti ya base ndani, msome tena
 
Nastick ktk para ya mwisho, kuna vitu ulivitaja pale juu na ukasema akiwa navyo bas ame qualify.

Huku mwishoni unasema Real Woman hatafuti sex & life assurance, anatafuta mambo ya kumfanya awe mwanaume tyuuh. Nafikiri ungeeleza hayo mambo ni yapii ili tujadili sasa kiundani.

Na umeingizia hapo Tamaduni pia, hivi umesoma andiko la Mshana lakini? Ndo maana nikaja na hilo swali, umejitahidi kujibu ila bado hujafikia jibu husika la swali.

Em jaribu kujibu tena, huenda kuna kitu umesahau. 😂😂😂😂😂
Amejichanganya vibaya sana, ndo shida ya kuendeshwa kwa hisia 🤣
 
Okay je hoja nimetoa au sijatoa na Kama nimetoa kipi ambacho kinabidi kifatie.

Mimi nasubiri hoja zako ambazo zitaelezea kuwa shoga anabidi kuoa au ukanushe hoja zangu kwa fact.
Hoja umetoa, kinachobidi kifatie ni wee ueleze au ufafanue kwa undani hizo hoja zako upate kueleweka.

Hoja zangu? Hili nilisha clear kuwa nataka mleta uzi yeye aweke hoja zake tujadili, maana ndo kaweka hili kundi ktk uzi wake

Na siwezi kukanusha hoja zako kwa facts ikiwa hujaeleza au hujadadavua kwa kina. Kwa kifupi ni hujaeleweka.

Narudia lile swali lijibiwe kwa ufasaha, km unaona huliwezi, unaliacha km lilivyo.
 
Amejichanganya vibaya sana, ndo shida ya kuendeshwa kwa hisia 🤣
Unajua leo kuna watu nilkua nawaona akili kubwa na wana upeo mpana, kumbe nilikua najidanganya.

Huyu Dr na Mtibeli, leo wameni suprise haswaa, 😂😂😂😂😂
Nacheka hapa hadi Co poaa. Wanajikanyaga tyuu,

kuna mtu aliwahi nambia, "ukitaka kuijua akili au uelewa wa mbongo hasa mwanaume, mpe Mada ya Ushoga afu mjadili, hata awe na PhD, hutoona tofauti yake na std 7"
Nimeamini leo hii hapa ktk huu uzi.
😂😂😂😂😂
 
Hapo umekosea sana kwanini hua mnadhani Shoga hana maadili lakini mwanaume anayebadili wanawake kila kukicha ana maadili au mwanaume mlevi ana maadili au mwanaume anayekula tigo za wanawake ana maadili au mwanaume jambazi ana maadili au fisadi mla rushwa ana maadili?

Usimjudge shoga kwa uelekeo wake wa kingono wapo mashoga wana hofu ya Mungu vile vile na wengine wachungaji kama ambavyo wapo walevi na wazinzi wenye hofu ya Mungu na wachungaji vile vile
Shoga mwenye hofu ya Mungu 😂 dah ya Leo kali
 
Ndoa ni stara kwa mwanamke! Hivyo mwanamke anahitaji ndoa kuliko mwanaume

Wanawake wamekuwa wengi ama ni wengi kuliko wanaume... Hivyo ndoa imekuwa kitu adimu hasa ukizingatia kuwa.. Pamoja na uchache huo wa wanaume bado karibia nusu yao si waoaji

Sasa kutokana na hamaniko hilo la kuhitaji ndoa wengi wamejikuta wakiangukia kwenye mikono ya wanaume wasio sahihi
Kuna kauli moja mabinti wenye kutaka ndoa wanaitumia bila kujua madhara yake! Hii kauli ya kusema "hata nikimpata anayepumua tu inatosha!"

Wadogo zangu wa kike hakuna kauli ya kiwaki kama hii... Unaingia kwenye ndoa na sio kwenye mapenzi.. Kauli huumba na Mungu humpa kitu alichokiomba!

Hivi mnajua kwa hakika mwanaume anayepumua tu yukoje!? Si mlemavu wa viungo ama akili.. Bali ni mlemavu wa ufahamu na kujitambua yeye ni nani na anapaswa kufanya nini kwa wakati gani
Unaingia kwenye ndoa ambayo ni mahusiano ya kudumu mpaka talaka itakapowatenganisha! Kifo ni mustakabali

Unapaswa kuwa na mtu anayejitambua, anayejali, anayeweza kubeba majukumu ya baba.. Na anayeweza kuzikabili changamoto kwa weledi kwa hekima na kwa utulivu

Mwanaume anayepumua tu ni yule ambaye utamuacha kitandani uende kazini ukiwa umeshamuandalia mpaka chai, Ataamka kwa kuchelewa, hawezi kutandika hata kitanda. Atakunywa chai na kuacha kila kitu hapo.. Hatafanya chochote mpaka urudi ufanye vyote na bado usiku umpe!

Wengine anaweza kuwa na kazi lakini huoni tofauti yoyote na asiye na kazi majukumu yote unayabeba wewe. Mwanzoni mwa ndoa utaona kama utaweza.. Lakini taratibu mkishazoeana utaanza kuliona tatizo! Na tatizo litazidi kujipambanua kadiri familia itakavyoongezeka. Watoto, Wafanyakazi, Biashara, Ufugaji nk

Utajikuta usipofanya wewe yeye hagusi kitu.. Matumizi ya nyumbani
Mahitaji ya watoto shuleni na nyumbani. Mishahara ya wafanyakazi. Manunuzi ya vitu kama mna biashara. Kuhudumia mifugo kama mnafuga nk

Ikitokea umepata safari ya siku chache tu ndio utaliona tatizo kubwa katika uhalisia wake..utakuta kila kitu kimeparaganyika Hesabu kwenye biashara, Manunuzi hakuna, Loss kama zote. Kama ni mifugo si ajabu kukuta mingine imekufa kwa kukosa huduma na mingine kupotea kwa kukosa ufuatiliaji.

Anaweza kufanya kikubwa ni matumizi ya pesa zako.. Ana we za Ku control mpaka account zako. Anachoweza kingine ni kukuzalisha kila mwaka bila kujali future ya hao watoto. Mwisho wa siku unajikuta unajutia majuto yasiyo na faida.. Unajikuta binti mdogo unazeeka kabla ya umri na kuandamwa na magonjwa yatokanayo na msongo wa mawazo

Nina mengi ya kuandika.. Lakini ya msingi ni haya! Kama ukiisoma hii mada na kuielewa naamini utabadili mtazamo wako kuhusu mwanaume wa kukuoa

Chelewa kuolewa lakini olewa na mtu sahihi.. Si wali nazi wala si mwanaume suruali wala si yule anayepumua tuu
Umenena mambo ya msingi sana, mwenye sikio na asikie maneno haya ya msingi. Ubarikiwe sana
 
Back
Top Bottom