Naombeni ushauri kuhusu kubadili dhehebu ili kufunga ndoa

Hapana mm sijamtaka yeye abadili ninachotaka Mimi kila mtu abaki na Imani yake
 
Asante
 
Wow...hii ni nzuri sana
 
Wow...hii ni nzuri
 
Hapana kipenzi usiseme hivyo jamani, still naangalia maoni yenu then nimshirikishe Mungu zaidi ili niamue maamuzi mazuri ambayo nitakuwa na amani siku zote za maisha yangu
 
Ni changamoto
 
ulikosea kuzipanga mkuu nimerekebisha😀
1.AKILI
2.UPENDO
3.IMANI
 
ukijifunza misingi ya BIBLIA vizuri nakuhakikishia lazima utafuata misingi ya SABATO.....
kua na madhehebu tofauti kwenye dini moja huo sio mpango wa Mungu halafu SABATO sio dhehebu
 
Hakuna ndoa inakaa vizuri kwa mama kusali A na baba kusali B. Amua kama kweli unataka kuishi maisha safi ya ndoa, mfuate mume wako, hakuna mwanaume anajielewa akafuata dini/dhehebu la mkewe.
 
Ushauri

1. Wengine tunaishi bila hizo Ndoa na tunaishi kwa furaha.
Ndoa kwa muktadha wa sasa ni kuruhusu kutawaliwa na external forces kama Mila, dini, na serikali.
Funga ndoa baadaye sana kwa maslahi ya mkeo au mumeo kupata haki zake pale siku usipokuwepo.. ishini walau miaka 20 huko ndio mfunge Ndoa.

2. Angalieni mazuri yaliyopo katika dini hizo mbili. Usabato na ukatoliki ndio yawe muongozo wa kulea watoto wenu.
Kila dini inamazuri na mabaya yake.
Jiangalieni ninyi wenyewé, kuona nani yupo vizuri kwenye sekta fulani ndio apewe kuifanyia kazi kuwalea hao watoto. Mfano, kama Mke unajua zaidi biblia basi mumeo ndio akuachie kazi ya kuwafundisha watoto lakini naye akijifunza. Yaani shirikianeni.

3. Msiruhusu external forces ikiwemo wazazi, jamii, dini kuongoza Familia yenu.

4. Tumieni kitabu mtakachoona kinawafaa kama ni Biblia kiwe ndio mwongozo wenu.
Hapo hakuna cha usabato wala Ukatoliki wala ulutheri. Hayo madhehebu hayapo kwenye hivyo vitabu ila yalianzishwa na Wanaume na wanawake kama mlivyo ninyi. Hivyo ohata ninyi mnaweza kuanzisha dhehebu lenu.

Mimi sikumshauri mwenza wangu abadili dini na wala sikutaka ajue dhehebu langu na hata sisemi najivunia yeye kunifuata kwani dhehebu kwangu has nothing to do kwenye mapenzi na kuongoza familia yangu. Muongozo upo kwenye Biblia.
Biblia haina Ukatoliki wala usabato. Biblia ni kitabu kikuu cha kuongoza wanadamu. Muhammad alitumia vitabu vya biblia kuunda dini yake ya uislamu.
Nanyi mnaweza kutumia biblia na quran kuunda dhehebu lenu.

5. Mnapotatua matatizo yenu makubwa na madogo kama hili la kutofautiana mtazamo kuhusu nani abadili dini. Msipende kushirikisha Watu. Wala msipende kufanya reference Kwa kuangalia mlipotoka bali angalieni maslahi yenu ninyi wawili na wapi mnataka kwenda.

6. Mtu akifafanua biblia au Quran asiweke mawazo yake mwenyewe bali aache biblia yenyewe ijisemee yenyewe.

7. Ndoa inajengwa na watu wawili tuu walioamua kupendana, kuwa kitu kimoja, na kuanzisha maisha yake.
 
Kama yeye ndiyo kageuka makubaliano bado all cards rests on you.....

Mkumbushe kuhusu makubaliano yenu, kama ataendelea kukaza shingo basi chukua maamuzi unayoona yanafaa kwako..

Japokuwa, dini kwa mwanamke sio kitu kikubwa sana, as long as huyo jamaa unaona anafaa kuwa baba wa wanao na mumeo, basi mfuate kwa kila kitu including dini..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…