Kwa alichokifanya Israel si kwamba ameshambulia utawala wa Iran. Alichokifanya ni kuishambulia Iran. Hilo inabidi ulielewe.
Unachokifikiria wachambuzi wa historia wanasema ndilo kosa lilimgharimu USA wakati wa vita ya Korea kaskazini na Korea kusini. USA ilidhani raia wa China hawatoingia vitani nao kwa kuwa utawala wa China wa Mao unaonekana ukiwadidimiza raia wake.
Kumbe kwa wachina ni tofauti. Matatizo ya ndani ya nchi yao watayamaliza wenyewe ila ukivamia nchi yao wataungana na kupambana na wewe kwanza.
Hili ndilo wengi humu tunashindwa kulielewa: Wengi wanasema utawala wa Ayatollah utang'olewa. Lakini hawajui kuvamia ubalozi wa nchi nyengine kuna maanisha nini! Kwa ufupi Israel imefanya makosa makubwa sana. Kwa hii hali ni kuangalia busara ya Iran itaamua vipi! Na kwa kutaka kufahamu ni kosa kubwa angalia anachopitia Israel kwa sasa. Mara afunge balozi, nchi yote kaiweka kwenye hatari ya kivita n.k