Nape Nnauye: Tuachane na hii habari ya "Sisi Wanyonge", kauli hiyo inatulemaza

Nape Nnauye: Tuachane na hii habari ya "Sisi Wanyonge", kauli hiyo inatulemaza

Hii ni sehemu ya nukuu ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akizungumzia marekebisho ya Kanuni ya Maudhui ya Mitandao ya Mwaka 2020, leo Machi 14, 2022. Msome kisha uniambie tuitafakari hii kauli ya WANYONGE.

Watanzania wameanza kuwa wanaongea barabarani wakiongea na simu haloo haloo kama wanapigishana kelele na mtu, hata msikilizani, hakuna smooth connection na mazungumzo.

“Niwaombeni tuwape muda TCRA wakati wakitafuta ufumbuzi, wakati huo tupate huduma lakini zilizo bora, ni jambo linazungumzika.

“Tuondoe hii habari ya sisi wanyonge, sisi wanyonge, inatulemaza, nataka niwaombe, tuondoke katika baadhi ya mambo, ukiambiwa tulipo na tunakotaka kwenda inahitaji muujiza wa ajabu sana…”
Hili jina la Wanyonge binafsi silipendi kweli yani
 
“Tuondoe hii habari ya sisi wanyonge, sisi wanyonge, inatulemaza, nataka niwaombe, tuondoke katika baadhi ya mambo, ukiambiwa tulipo na tunakotaka kwenda inahitaji muujiza wa ajabu sana…”
Inge sound meaningful angesema angalau siku 370+ kabla ya leo
 
Mkuu umesahau kua mwendazake amejivika cheo cha izilaili.

Waislam wanasema ukiona mtu anafanya kitu kibaya hatua ya kwanza mkataze kwa mdomo,kama huwezi hatua ya pili tumia nguvu zako,kama humuwezi tena hatua ya 3 na mwisho chukia lile tukio na mchukie na anaetenda.

Kipindi cha mwendazake watu wengi walibaki kwenye kuchukia maana hawakua na ubavu tena.ukithubutu kwa hatua yoyote unaweza kunyofolewa roho.

Hivyo mkuu usimulaumu mtu kwa kutoongea kitu kwa wakati ule.
Hii ipo kiimani zaidi au ni scholarly opinion ya kidunia?
 
Inaweza kuondoka endapo kutakuwa na usawa kati ya wenye nacho na wasio nacho. Kama kuna matabaka, neno 'wanyonge' haliwezi kuondoka. Kama kuna tofauti ya maskini na tajiri, wanyonge watakuwepo tu.
Zab 41:1 Heri amkumbukaye mnyonge; Bwana atamwokoa siku ya taabu.

Mnyonge ni mtu anayetamani kutendewa haki pasipo masharti, lakini hana uwezo. Leo hii kwenye mitandao wanakata salio kablaa hata halijatumika, wanyonge watakosaje kuwepo?
Masikini hana faida
Tuchape kazi kuepuka umasikini
Usawa hauji kwa kuchati
Tuchape kazi wakuu
 
“Tuondoe hii habari ya sisi wanyonge, sisi wanyonge, inatulemaza, nataka niwaombe, tuondoke katika baadhi ya mambo, ukiambiwa tulipo na tunakotaka kwenda inahitaji muujiza wa ajabu sana
Inahitaji miujiza kwasababu hamtaki kukubali kuwa kukataa kwenu Katiba Mpya kwasababu za ubinafsi wenu ndio kunafanya maendeleo ya nchi kuhitaji miujiza!! Kama rasimu ya katiba ya WARIOBA itapitishwa wananchi watakuwa huru zaidi kushiriki katika maendeleo yao na pia kuwa na TAASISI zenye nguvu!!

Kukiwa na TAASISI zenye Nguvu kwa mfano, kusingetokea haya yaliyotokea kwa Samia kuwateua katika nafasi nyeti watu ambao walikuwa hawana intergrity kama ilivyothibitika katika utawala uliopita!! Isingewezekana kwa Rais kuwateua tena watu kama Mafuru, Muchechu na wengine ambao waliondolewa katika utumishi wa umma hapo awali!! Kwavile hatuna Taasisi zenye nguvu kuthibit uteuzi wa namna hiyo ndio maana haya yanatokea na wananchi have no recourse!!
 
Pande moja wanakataa unyonge, pande nyingine inapigania haki ya kuendelea kuwa wanyonge. Ukiwaambia habari za reform za katiba, haki, nguvu ya umma na mengine kama hayo wote wawili wanaungana na kuwa wamoja kuyakataa.
 
Inaweza kuondoka endapo kutakuwa na usawa kati ya wenye nacho na wasio nacho. Kama kuna matabaka, neno 'wanyonge' haliwezi kuondoka. Kama kuna tofauti ya maskini na tajiri, wanyonge watakuwepo tu.
Zab 41:1 Heri amkumbukaye mnyonge; Bwana atamwokoa siku ya taabu.

Mnyonge ni mtu anayetamani kutendewa haki pasipo masharti, lakini hana uwezo. Leo hii kwenye mitandao wanakata salio kablaa hata halijatumika, wanyonge watakosaje kuwepo?
Ok mnyonge!!
 
Ukweli mchungu, Africa yote ni wanyonge mbele ya mzungu!

Hatuwezi kujiamini kwa wazungu, na huo ndio unyonge, ila Magufuli tuu ndiye angalau alithubutu Kuwaita mabeberu mchana kweupe
Na ukiitwa mnyonge mbele ya muafrika tunaiitaje???
 
Hii ndo maana ya siasa za kubebwa. Kwa mwansiasa anayejitambua, anafahamu maana ya lugha kama hizo na comfort yake kwa wananchi. Kwa huyu anayepewa kwa sababu baba alikuwa mtunzi wa nyimbo, hajui amachoongea. He is just a devious politician.
Hiyo comfort ya kisiasa while in reality ni choka mbaya!!
 
Back
Top Bottom