Kuna mtu niliwahi kukaa nae Arusha alikua na bureau, alinipa mkasa mzima
Aisee Hio siku walipofungua bureau zilikuja defender na 'vyuma' yaani walichukua pesa zote hata coin haikubaki, na katika askari waliotelekeza amri hii na kupeleka pesa bot wengi walitajirika maana kama unavyotujua wabongo huwezi kunipa maburungutu ya pesa ambayo hayana hesabu nikayafikisha yote
Ila Hawa watu nao walikua wanaibia taifa sana pesa na wengi walikua wanatakatisha sana pesa chafu, kiufupi walijisahau sana jiwe akaamua kuwapiga ambush kiroho mbaya,
Hii nchi watu hawaelewi tu, hakuna watu hawapendi kulipa Kodi kama matajiri, ukishaona mtu ana bilion kadhaa bank asimilia 90 ya hao watu ni janja janja nyingi tu na kuibia serikali mapato
Swala la kuwanyoosha Hawa matajiri waiba Kodi sijawahi kumpinga magufuli japokua nilikua simkubali, ila la kudeal na Hawa wezi wa Kodi hapo Mzee nilimkubali