Napendekeza Rais aliyechaguliwa akifia Madarakani, makamu wake ashikilie nafasi hiyo kwa siku 90 tu kisha uitishwe uchaguzi

Kwa taarifa yako watanzania wasingekuwa waoga, hata dhalimu ama ccm wasingekuwa madarakani.
 
Na kwa sababu sikumwomba ridhaa ya kufanya hiki nilichofanya, naomba anisamehe kwa sababu sitaweza kuweka hapa ID yake. Hivyo, ninaomba kuwajibika kwa huu uzi kama mmiliki wake kwa asilimia zote.
Mkuu 'kunguni', niseme unao uzito wa kutosha kabisa. Karibu sana JF.
Ninakubaliana moja kwa majo na hoja iliyowasilishwa; hasa hiyo ya siku 90 za mpito kabla ya uchaguzi.
Pengine inaweza kusemwa kwamba gharama za uchaguzi wa rais mpya, kwa kiongozi aliyebakisha mwaka mmoja, au mmoja na nusu amalize muda wake inakuwa ni gharama isiyokuwa ya lazima sana.

Kwa hiyo kunaweza kuibuka mapendekezo mbadala ya hizo siku 90 katika hali ya namna hiyo.

Huu utaratibu uliopo sasa ulitushangaza wengi ambao hatufuatilii sana matakwa ya Katiba hii tuliyo nayo. Sikutegemea kabisa kwamba Samia angechukua madaraka na kuanza kufanya kivyake, upya kabisa vikiwa ni kinyume na yale aliyokuwa akiyafanya aliyekuwa akimsaidia kazi.

Hapa inaonyesha wazi udhaifu mkubwa sana uliopo huko ndani ya chama. Hata kama Samia anatekeleza maagizo ya chama, lakini utekelezaji wa maagizo hayo ni tofauti kabisa na kinachojulikana kuwa msimamo wa chama hicho.

Ukweli hapa ni kwamba, CCM imepoteza kabisa sura ya kuwa chama cha siasa, kwa sababu kila kiongozi anayeingia madarakani anakichukua chama na kukifanya kuwa mali yake. Yote ambayo yangeagizwa na chama, sasa yanakuwa yanatoka kwa kiongozi mwenyewe.
Hizo kamati, sijui CC na NEC zipo kama mapambo tu, kama ilivyo kwa Bunge zima.
 
Inafaa IFIKIRIWE
 
Naunga mkono HOJA 🙏🙏

Ila Mungu atuepushe, Rais asife akiwa madarakani siku zijazo,

Imekuwa safari ndefu sana ya machozi na kuyumba Kwa Nchi .

Mungu ibariki TANZANIA.

Amen
 
Wenyewe huko huko CCM walishaona tatizo. Alaumiwe Mabeyo, aliyetaka utaraibu ufuatwe bila kujali ubovu ambao mhusika angeusababisha kwa taifa.
 
Hoja inakuja hio ajali ya kufariki akiwa madarakani ni nadra sana kutokea.
 
Napinga pendekezo lako. Wazanzibar walio na huruma hekma na busara nyingi watakuwa hawatawali.
 
Bila katiba mpya na tume huru ya uchaguzi sioni CHADEMA wakiunga au kutilia maanani hili suala.
 
Chuki tuu unafikiri waasisi wa nchi hii walikuwa wajinga kuweka hivyo?
 
Wenyewe huko huko CCM walishaona tatizo. Alaumiwe Mabeyo, aliyetaka utaraibu ufuatwe bila kujali ubovu ambao mhusika angeusababisha kwa taifa.
Ndio maana wajanja wengine wakashangilia, kwasababu walijua watamuendesha wapendavyo kama mdoli wao, na ndicho kinachofanyika sasa, Samia amegeuka kiongozi wa waarabu na wafanyabiashara wachache, badala ya watanganyika wote.
 
Well said Mkuu Kalamu.
 
Bila ya kubadilisha utamaduni na mfumo wa kupata viongozi, hata mkipiga kura kila siku mtalamba galasha tu.

Utaona huyu mbaya, utalia, atakuja mbaya zaidi yake.
 
Kufa kwa Magufuli tarehe 17/ 03/21 ilikuwa ni ukombozi wa pili kwa Tanzania baada ya kujikomboa kutoka ukoloni wa Mwingereza. Yule paka ni vizuri alikufa na muache aendelee kuoza huko Chato
 
Mwenye mada hii ni MasterGamaliel . Umeshindwa nini kum tag ili ashiriki kwa upana kuweka mawazo yake. Umemtenga makusudi ili kujenga mawazo yako yenye sumu

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…