Tatizo hawa wanaopewa nafasi ya kusimama kama Makamu wa Rais huchukuliwa kama wasindikizaji tu, watu wepesi wepesi, ili ku- balance gender.
Sasa bahati mbaya kwetu, huyu "mwepesi mwepesi" amejikuta ameingia ikulu kwa mlango wa nyuma, matokeo yake ndio haya, anatuthibitishia alivyo mwepesi kwa kuzigawa bure bandari zetu zote Tanganyika kwa wajomba zake.
Mimi naona sasa hili liwe funzo kwetu, kwani licha ya kubadili sheria baada ya kifo cha Rais aliyepo madarakani mambo yaende vipi, lakini pia, panahitajika umakini mkubwa sana wanapoteua jina la mgombea mwenza wa Rais, huyu ndie mshauri namba moja wa Rais, hatakiwi kuwa kilaza.
Kwasababu imeonekana huyu makamu anaweza kuingia ikulu bila kutarajiwa, sasa kama mtu asiyetarajiwa akiingia ikulu, huku upeo wake ukiwa unatia mashaka, matokeo yake ndio anakosa msimamo, anapelekwa hovyo na kundi analoliamini, na pale anapoamua kufanya jambo lake, basi ndio anakosea 100% huku akigoma kubadilika.