Nashindwa kuelewa, hapa kuna upendo kweli au napotezewa muda?

Nashindwa kuelewa, hapa kuna upendo kweli au napotezewa muda?

Nilichogundua huyu mwenzangu ana dharau na kiburi sana, hajapiga simu anatuma tu msg, hataki kuongelea yanayoendelea yeye ni salamu tu, na mimi leo ndiyo mwisho wa kujibu msg zake, nimeamua hivyo.
Hamna kitu utamtafuta tena na utampigia sana!
 
NRNE
Habari za muda mrefu wana jukwaa, mimi msichana, niko kwenye mahusiano na mwanaume amenizidi miaka 15, yeye ana mtoto mmoja mimi sina.

Mimi nipo Dar, yeye yupo mkoani, tulipoanza mahusiano nilijua kwakuwa ni mtu mzima pengine, tutaenda sawa kwani na mimi huwa sipendi mambo ya hovyo. Lakini pia nilijua anaweza kuwa amechoka kukaa mwenyewe hivyo atanioa haraka tu (lakini hii haikuwa dhamira yangu kubwa)

Sasa kuna vitu huwa vinanikosesha amani mno, kwanza huyu mwenzangu unaweza ukaongea tu kitu cha tofauti kinaweza kuwa kidogo tu lakini atakishikilia na kukufanya ujione umekosea sana, hapo utaanza kuomba na misamaha ya kutosha. Lakini yeye ikitokea amekosea atalipindisha hilo kosa hadi lisionekane kama ni kosa.

Kama wiki kadhaa zimepita aliniambia ameenda kwao kusalimia, wakati yupo njiani tulikuwa tunawasiliana hadi anafika, sasa kama siku mbili mbele akaniambia ile siku ameenda alimpitia na mtoto wake ameenda naye, nikamuuliza mbona hukuniambia, akaniambia mambo mengi alipitiwa mh! Nikashangaa.

Wakati yupo huko huko akanipigia akaniambia yupo maeneo ya stendi, sasa sikusikia vizuri kumbe alisema kuna mzigo ameufuata nikamuuliza tena umesema umefata mzigo, akanijibu " hivi maswali yako unayoulizaga huwa unafikiriaga kweli" guys hii kauli iliniuma yaani ameniona mimi sina akili, nikamwambia haya baadae, nikakata simu nikatafakari kama siku tatu nikampigia maana na yeye alinikaushia, hakupokea simu, ila huku status whatsapp anapost, hizi si ni dharau jamani. Na yeye kakaa kama siku mbili tatu hivi akanitumia msg whatsapp " habari yako" na mimi sikuijibu ile siku nijibu "salama" after two days, akajibu kwa kureact akakausha, leo naona kanicheki normal, mimi nikampigia hajapokea.

Nashindwa kuelewa ni upendo gani huo wa kumkasirikia mpenzi wako, kwa vitu vidogo vidogo ambavyo mnaweza kueleweshana tu, wakati mwingine unaweza kukuta usiku ikatokea mmegombana hivi ukimpigia ili muongee muyamalize hapokei kabisa ila msg anajibu anasema hajisikii kuongea, hatakagi suluhisho, sasa najiuliza kama huku mwanzoni yupo hivi je ikitokea tukaingia kwenye ndoa huko si ndo atakuwa akikasirika na matumizi anasusa kutoa kabisa🤕

I'm not perfect, hata mimi nina madhaifu na mapungufu yangu, lakini huwa nina amini kwenye kurekebishana ila mwenzangu naona hilo swala hataki kabisa, niliplay part yangu vya kutosha kujishusha nimejishusha sana misamaha nimeomba mingi mno ila kwa sasa moyo umechoka kuvumilia haya mambo, maisha yanipe stress bado na mapenzi tena yanipe stress si nitajifia na presha.

Naombeni ushauri wenu, wakubwa zangu.
Ana mke wake huyooo. Kimbiaaaaa
 
Mkuu inaweza kupita hata miezi mitatu hatujakutana, hii inanipaga maswali japo ni kweli anakuwaga bize na kazi ila ananitisha sana
Nilitaka kupita kimya kimya ila nimeshindwa kwanza pole sana huyo mwanaume anaonekana ana mwanamke mwingine zaidi yako

Kingine hivi anavyokuonyesha alama zote hizo we mwenyewe huoni kama hakuna mapenzi hapo jamanii au ndio mapenzi upofu

Cha mwisho huyo shemeji sio mfupi kweli mana kwa gubu hao
 
Nilitaka kupita kimya kimya ila nimeshindwa kwanza pole sana huyo mwanaume anaonekana ana mwanamke mwingine zaidi yako

Kingine hivi anavyokuonyesha alama zote hizo we mwenyewe huoni kama hakuna mapenzi hapo jamanii au ndio mapenzi upofu

Cha mwisho huyo shemeji sio mfupi kweli mana kwa gubu hao
Siyo mfupi ni mrefu sana ila nashangaa wakati mwingine anakuwa na majibu mafupi
 
Hivi mfano unakutana na mtu nyie mnawasilianaga WhatsApp tu Hakuna normal calls wala sms ina maana usipokuwa na bando ndio hamuongei hivyo ukimuuliza why so anakwambia I hate calls

Mpnz wako kusikia sauti yake ni mpk mtake kuonana tena mpo mikoa tofauti

Ndugu yangu hapo nguvu ya kukabia kwa juu unaipata wapi
Aiseeh mnawezaje haya mauhusiano jamani ishara zote unaonyweshwa mwanaume hakutaki wewe ndio unafosi mahusiano jamani poleni sana
 
Punguzeni pupa kwenye mapenzi [emoji81][emoji81]
Mwanaume ukiwa unamjali sana anakuona huna pa kwenda na hujiamini km uko naye..!!

Wewe ukipata mpenzi acha kuwaza kumfurahisha ili umteke, acha kupatikana muda wote..!!

Sasa km wewe mwanaume hakupi pesa wala hakujali ila akitaka kitumbua chap unampelekea bila kusita..!! Si uchizi huo [emoji81][emoji81]

Unaacha kumuomba pesa kwa kujua atakupenda kumbe mwenzio anaona kajipatia bwambwa la bure [emoji1787][emoji81]
Anajua akikutajia ndoa unaloa anachomeka anakojoa anapita vile..!!
Wanaume wanataka kitu kisichopatikana kirahisi..!!
Mdogo wangu kazi ya ushauri unaiweza sanaa [emoji1787]
 
Back
Top Bottom