Nataka niachane na huyu Mwanamke bila kuathiri Watoto

Ukiacha watoto nyuma unaweza kuwakuta washakua mashog... Nibora uondoke nao
 
Asante FK U too
 
Wakuu.

Nimekaa na huyu mwanamke 5 years tumepata 2 boys. Ila sasa simwelewi kabisa dharau shazi hela unampa ila matumizi hayatimii.
Kama hili ndio tatizo kuu mbona kuna solution ? Fanya baadhi ya hayo matumizi na kama na yeye uwezo anao achangie kwenye kupata hayo matumizi...; Ila mara nyingi mambo mengi katika haya maisha huwa ni symptoms tu lakini kuna root cause (mfano kuchokana; na mtu ukishamchoka hukosi sababu)

 

Mkuu, malezi yenye "afya" ni wazazi kiwa mbali na watoto wao?
Yaani huyu bwana, akiwa mbali na watoto wake inaweza kuwa ni malezi yenye "afya" kwa mtoto/watoto?
 
Akiondoka nao ndo hawawezi kuwa mashoga wakiamua?
Ila fikra zenu waja, Lol
Mtoto wa kiume alielelewa na mama pekee anakua na tabia za kimama kudeka,akimuona mama anasuka na yeye anataka kusuka akifikiri nisawa,mama akiosha vyombo na yeye yupo,akiiona mama kavaa Dera nayeye anataka , mengine mtamalizia
 
Huyoo ni chaguo lakooo🎶🎶🔊
 
Mjomba, nakupa mfano hai.

Hali kama hiyo ilinitokea, jaapo mi nilitelekezewa mapacha wakiwa na mwaka mmoja.
Wakati mwingine, kuna mtu ukimuangalia, unajuta kufahamiana nae.

Lakini pia, ukiangalia huwezi fika popote ukiwa nae. Na mkiachana, kama ni mwanaume unaejielewa, unajiuliza watoto wanaenda kuishi maisha gani.

Na kuwahudumia, still ni yeye utatakiwa kumpa hiyo hela. Na kwa vile hamtakuwa pamoja, usitegemee atawajali kama inavotakiwa. Maana atajua ni wajibu wako.

Bado inauma, kulea watoto mzazi mmoja. Ila tu, angeweza kukuachia, ukawatafutie mtu akusaidie. Ila sasa, tatizo litakuja pale unapohitaji mwanamke. Je wa kuweza kuwalea una uhakika utampata?

Japo hata mwenyewe nikiwaza maisha yao, kichwa kinawaka moto. Ushauli mwingine ukipata huenda na m najifunza jambo.

Wangu nilifikia hatua ya kumuomba akalee watoto, alichonijibu ni kwamba niwalee na mimi ni baba yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…