Nauli hizi za SGR nani atapanda? Kutoka Dar - Moro Tsh 24,000?

Yaani mtu alipe 60k kwenda Dodoma?!
 
Mkuu nenda na kwenye mabasi check zile free riders zilikuwaje. P
Pamoja na kuwa ni huduma baadhi ya maeneo lakini nauli ni kubwa kuliko mabasi na serikali inatoa ruzuku. Mkuu kwenye hii bei, na uwekezaji haviendani. Serikali itatoa ruzuku. Lakini vyovyote vile treni lazima iwe ghali kulipia hizi trillioni. Vinginevyo, tutazalisha kila siku ili tulipie deni la SGR
 
Let's get back to basics..., Initial investment ya mkopo utalipa tu, hata iweje..., kwahio hapo cost inayobaki ni operation cost ambayo ni on-going... (kumbuka price isipokuwa rafiki na watu wana alternative utakuwa unasafiri bodi tupu)

Kwa sehemu ya abiria wachache nenda na basi kwenye abiria wengi train ni chaeper sababu inachukua wengi kwa wakati mmoja hence kupunguza unit cost, pia kwa mizigo ndio cheaper zaidi hasa ukiongeza na gharama za uharibifu wa barabara...

Tatu kwenye miji mikuu ambapo kuna traffic congestion train inakuwa rahisi kwa mtu kuwahi kufika (kuzalisha mali) kwahio ni faida kwa nchi huyu mtu kuweza kumtoa point A mpaka point B..., na sio ajabu mtu akafanya kazi Dar akakaa Morogoro kwahio huyu mtu huenda hii isiwe one-off safari kwenda kumuangalia bibi bali ni everyday cost...; Kwahio kama wanaweza wakapatikana watu wa kujaza mabasi 6 kwanini kusiwe na train moja kwa bei bei ya chini ya basi ili wote hao waweze kuwahi makazini ?
 
Ilitakiwa mwanza to dar iwe 50k tu isizidi hapo, nasio huo upumbavu walio andika hapo wa dar to bahi
 
Hii nchi ya ajabu sana. Wenzao hizo tren wanaweka bei chini ili mtu aishi moro lakini anafanya kazi kila siku anaenda na kurudi. Sasa wenyewe nauli kubwa utafikiri sio kitu cha Umma.

Ona usafiri wa ndege ilibidi waiue fast jet ili wakabe wateja. Lakini wateja bado wakashindwa bei wayolikuwa wanapandia fast jet ilikuwa nafuu mara mbili kuliko ya Umma.

Miccm ina tamaa kukimbilia kushibisha matumbo yao. Hapo tayari kuna miccm imeshapanga safu ya watumishi kulifisadi huo mradi. Hapo hata tiket fek za baadhi yao tayari ziko kuchapwa
 
Baada ya kukamilika kwa reli ya kisasa ya umeme ya SGR, Leo yametolewa mapendekezo ya Nauli ili wadau waweze kuchangia maoni yao juu ya nauli hizo. Mkutano wa Kupokea Maoni ya Wadau kuhusu Nauli za Abiria kwa Treni za Reli ya Kisasa SGR utafanyika tarehe 19 Disemba, 2022 ukumbi wa Anatorglo - Dar es Salaam.

Awamu ya Sita chini ya Dkt. Samia Suluhu imekamilisha tayari kwa kuanza safari tukutane mji kasoro bahaari.

 
Kama Moro Ni elfu24 basi Dodoma angalau iwe elfu50
 
It's a matter of time kabla hujanielewa na suala la umeme wa Bwawa la Nyerere pale nilipokuambia tena na tena kwamba mnaosubiri umeme wa bei rahisi, MNAJIDANGANYA...

Na ile siku, kabla sijaamua kukuacha uendelee na fantasies zako, ulikuwa unatumia hoja hizo hizo "umeme ni huduma"... economies of scale!
 
Sasa ni zamu ya walamba asali na ambao hawafi
 
Kwa siku unajua wanaingiza sh ngapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…